Thursday, November 3, 2011

WIFI TUHESHIMIANE....

Dada,

mwenzenu jamani limenikaa kooni naona linanikaba nimeamua nilitapike kabla sijafa kujifanya uvumilivu kuvumilia ndoa mwisho nitakuja kufa kwa mapresha bure miye sijui watoto wangu nitamwachia nani.

nipo kwenye ndoa muda sasa, wakati wa mwanzo nilikuwa naheshimiana na kupendana na mawifi zangu sna, lakini zaidi nilipatana sana na wifi yangu mmoja anakaa sinza ameolewa na ana watoto wa nneanakaa kwenye nyumba ya kifahari na kwakweli kama uwezo anao.

nilipoolewa mume wangu na mimi mara nyingi tukawa jumamosi tunaenda kuwatembelea siku nyengine kama tunachelewa kuondoka kwa vile ni mbali basi tunalal huko huko yani imeshatokea hivyo kama mara tatu hivi wala mimi sikuona kama ni kitu kibaya mpaka nilipoona vinazidi na kuanza kukataa kwenda akawa anaenda mwenyewe kwa nguvu.

miaka mitatu sasa ya ndoa yetu namshangaa mume wangu na huyu dada yake wala siwaelewi kabisa, maana siku hizi mume wangu kila jumamosi ananiambia anaenda kwa dada yake na analala huko mpaka jumapili jioni ndio anarudi nyumbani ananiacha mimi na mwanangu yani sasa hivi ndio mtindo wake kila jumamosi lazima akalale kule jamani hii nini?

kitu chengine kilicho nishangaza zaidi wifi yangu anamnunulia mume wangu boxers jamani kweli wewe hata kama unamapenzi ndio mapenzi gani kwa mdogo wako mpaka ukamunulie chupi wakati anamke yani hii si dharau ama huyu wifi ananitafuta nini mimi? mara siku nyengine mdogo wake anapoenda kwa huyo dada yake jumamosi anarudi na nguo mpya zake kibao kama shopping ya laki sita ama saba hivi kafanyiwa na dada yake yaaaani mpaka nashangaa, sawa basi namuuliza hata kama dada yako anakuonyesha mapenzi si anajuwa kama umeoa ndio hata kusema shika hili dira, na hiki kiatu cha mtoto kawapelekee ndio dharau gani ama kwa vile siwezi kwenda kukununulia?

jumamosi iliyopita wifi yangu akanipigia simu ananiambia eti anaenda kwenye harusi mumewe hataki kwenda kwahiyo ataenda na mume wangu, yani ananipa taarifa sio kuniomba nikampigia simi mume wangu na kumwambia eti hana la kusema na kweli akaenda na dada yake bila aibu.

sasa juzi ananiambia yeye na dada yake wanasafiri kwenda zanzibar wiki moja, yani ndio nimechoka kabisa lakini nikifikiria huyu ni dada yake baba mmoja mama mmoja na hivi vituko anavyonifanyia kweli analala na kaka yake au nadhani atakuwa anamuunganishia shoga yake mume wangu maana huyu wifi yangu ni lishangingi tu la hapa mjini wenye mume na bado wanakuwa na serengeti boys kisa wana hela za kuwatunza.

wazazi wangu sijaawaambia hili lakini kaka na dada zangu ndio wanaojuwa na wananiambia niondoke na niwaeleze wazazi maana wazazi wa mume wangu walishafariki. naombeni ushauri wenu wenzangu maana naona nimevumilia naona naumia tu mwenyewe.

Mwavita


Reactions:

6 comments:

 1. pole dada ulieomba ushauri yaani huyo wifi yako ni fisadi haswa inaonekana huyo wifi yako anamkuadia mume wako kwa lishangingi mwenzie haingii akilini mume wa mtu aache mke wake nyumbani akalale kwa dada yake tena sio mara moja wa bahati mbaya alafu amfanyie shopping hadi nguo ya ndani haitaji kwenda kusoma chuo kikuu kujua mume wako ametafutiwa lishangingi na wifi wako lakufanya shirikisha wazee wa kanisa kama wewe ni mkiristo pamoja na wshenga na ndugu wakaribu kweli ukishangaa ya musa utayaona yafirauni pole dada dunia ya sasa ndivyo ilivyo mambo ni mengi sana

  ReplyDelete
 2. wifi yako ana wifi mwingine na ndiye anayekwenda ZNZ na mumeo wewe mwambie twendeni wote watatu uone kama atakubali.

  ReplyDelete
 3. Fuatilia kwa makini dada, Huenda mumeo anatembea na dada yake coz hivyo vitu huwa vipo. Uwe makini, utagundua kitu kati yao, dont punic, wala ucmgombeze mumeo.

  ReplyDelete
 4. nakupa pole dada yangu, hapo unatakiwa kuchukua hatua mapema bila kuchelewa, maana ukimwi unapiga hodi mlangoni, mbane mme wako siku moja umuombe mtoke out na umuhoji kwa kina lazima tu utajua ukweli wa ndani ukimbana atakwambia tu! tena huenda akasema kuwa dada yake ndio anamtafutia mwanamke ila yeye hataki lakini hapo atakuwa amekubali na kukwepa kitu fulani, basi mpaka hapo utajua kuwa ameshakutenda au la. Chukua hatua sasa.

  ReplyDelete
 5. Ukifuata ushauri wangu utakuja kutoa ushuhuda hapa.
  Izoo hapa.

  ReplyDelete
 6. Pole sana, kwakweli huyo wifi yako hana adabu, mi na kushauri ukaongee na wazazi wako na kama inawezekana hata washenga waitwe.Kama alivyo pendekeza mwenzangu hapo juu, kanisani unaweza kwenda ili kupata ushauri wa kiroho. Mamii ukumbuke kusali mana haya yote ni majaribu.Kama inawezekana mwite huyo wifi yako mkalishe chini na mumeo uwaeleze kuwa hupendezwi na hayo yanayoendelea kati yao..ni kifo tu kitatenganisha ndoa yenu na si binadamu..

  ReplyDelete