Thursday, November 3, 2011

MAPENZI NI KITU GANI.....

leo nilikuwa naongea na rafiki yangu akanieleza jambo moja ambalo sikumficha kama nitakuja kuliweka humu nanyi mchangie kumpa mawazo zaidi kuhu yeye na mumewe...

rafiki yangu huyu ameolewa kabisa ndoa ya kiislamu na kama wengine wote mapenzi mwaka wa mwanzo huwa ni matamu sana mpaka wakajaaliwa kupata mtoto wa kiume ambaye sasa ana miaka mitatu, mtoto huyu ni rafiki sana wa baba yake.

sasa anachoshangaa ni kwamba mwanaume siku hizi amebadilika sana, ukizingatia huyu dada sasa ni mjamzito wa miezi nane, yani kwanzia mimba ina miezi mitatu huyu baba amebadilika amekuwa kituko cha aina gani sijui.

kwanza kila akija nyumbani yeye mkali yani anamajibu ya shombo tena ya samaki ana gubu kama mwanamke, halafu kila anapoombwa hela yeye siku zote hela hana, hajali kama nyumbani mmekula ama la, yani anasema hata haelewi amekuwaje na chakushangaza zaidi hata siku moja hajawahi kumpa mkewe hala thumni ya kwenda clinic ama hata tu kumuonyesha mapenzi na kwenda naye.

mbaya zaidi huyu baba anakataa kumpa mkewe hata hela ya kwenda kujifungua, anamwambia hatamuhudumia kwa chochote na wala hajali chochote kuhusu huyo mtoto anayekuja, na huyu dada akimuhoji kwanini unamfanya huyu mtoto kama sio wako anamwambia kama unataka nikuhudumie nenda kwa wazazi wako mkoani nitakuwa nakutumia matumizi huko ebo!!!!!!!( huyu mtoto kwani alikupa wazazi wako).

kwakuwa huyu dada amekataa kwenda mkoa kujifungua huyu baba kamwambia kwamba yeye anaondoka anasafiri kwa muda mrefu sasa huyu dada anasikitika huyu mwanaume hana utu wakati anajuwa hana msichana wa kzi atakapoondoka na ndio anategemea kujifungua huyu mtoto wa pili atafanyaje mwenyewe??????

huyu rafiki yangu akaniambia halafu sijui kwanini anaendelea kumvumilia wakati mwanaume hana lolote, kwanzi nyumba na kila kitu ndani ni cha mwanamke mpaka simu anayotumia mwanaume ni mkewe kamnunulia, na huyu kaka kazi hana misheni town tu hata hela asubuhi mara nyngi mkewe ndiye anayempa halafu bado analeta jeuri, siku akipata dili likimchanganyia ndio aje na hela nyumbani siku nyengine zote mkewe ndiye anamuhudumia.

akitaka kuachana na huyu kaka anamuonea huruma mwanaye kwani anampenda sana baba yake hajui tu kama baba yake baba jina.. maana yeye anasema ndio maana wanawake hutoka nje ya ndoa kwa maudhi kama haya hata matunda hamchumi chumbani kila mtu mzungu wa nne kunamapenzi tena sibora angoje kujifungua atafute wake wa pembeni wa kumliwaza.

kwakweli namuonea huruma sana na ukiangalia anatumbo tu kubwa la kujifungua hana hata hamu ya kurudi nyumbani anapokuwa kwenye mizunguko yake.


2 comments:

  1. Jamani wanawake wengine wanayaweza, uislamu uko wazi kuhusu suala la ndoa. Mwanamke wa kiislam unatakiwa uhudumiwe chakula, mavazi na malazi, na lazima mume akupe unyumba na hayo ni masharti ya ndoa, kinyume cha hapo mwanamke una haki ya kujivua kwenye ndoa (khula). Yaani unakwenda kwa kadhi au huko Bakwata unaeleza hali halisi kisha unatoa kiasi cha pesa kurudisha mahari kama sikosei (huko kwa kadhi au Bakwata watakuelekeza vizuri) kisha mwanaume anaitwa anapewa hiyp pesa akiipokea ndio umejivua kwenye ndoa yako. Na hata kama hakuipokea wakiona hali ni mbaya bado watakupa talaka yako uendelee na maisha yako.

    Kingine bidada usithubutu kutoka nje ya ndoa, kwenye uislam adhabu yake ni kubwa sana kwani huna sababu ya kutoka nje ya ndoa wakati una uwezo wa kuivunja hiyo ndoa. Mwanamke au mwanaume wa kiislam aliye kwenye ndoa akizini adhabu yake ni kupigwa mawe mpaka afe. Kwa kuwa nchini kwetu hawafuai sheria ya kiislamu lakini hiyo haimaanishi kuwa dhambi yake na adhabu yake kwako imefutika. Achana na mawazo hayo wakati una option ya kutoka kwenye hiyo ndoa, ukizingatia unaweza kusimama kwa miguu yako miwili.

    Ukitoa mguu wako kwenda kwenu mwenzio anaingiza mwanamke mwingine ndani ya nyumba, inaelekea hiyo nyumba ndogo inampelekesha akuache sasa ndio anatafuta visa hivyo, haingii akilini huduma za afya nzuri zilizopo Dar uziache uende mkoani.

    Kuhusu mtoto kumpenda baba yake hicho ni kisingizio chako mwenyewe unakitumia ili kujistify ujinga uanaouvumulia, unaona aibu tu kusema ukweli kuwa unampenda sana huyo Gume gume.

    ReplyDelete
  2. Pole sana ndugu yangu...sasa ni hivi hamna kwenda Hiyo hela ya kusafiri iweke vizuri itakusaidia wakati wa kujifungua..huyo mume wako mwache asafiri akapunge upepo..akishaenda huko akaona hamna mtu wa kumsaidia akili itarudi kichwani..wala usivunje ndoa,hiyo nyumba ni yenu wote.. take your time and enjoy ur life with your children..naamini kabla ya ujauzito ulikuwa unafanya kazi na pesa ulikuwa unapata...jikaze kisabuni hizi shida zote zitapita..

    ReplyDelete