watu husema fainali uzeeni humaanisha nini? je ni kwamba mtu anapofikia uzee hutakiwa kukaa na kutafakari aliyoyafanya ujanani na ni yapi yalikuwa faida kwa familia yake na yapi yalikuwa hasara amuombe MUUMBA wake msamaha na kumalizia uzee vyema???????
sasa basi inakuwa vipi pale mtu anapofikia uzee kwa umri na mwili lakini bado akawa na mambo ya ujana, hii kama wewe ndiye mtoto wa huyu baba utafanyaje story ikiwa hivi....
baba yako mzazi alifariki mkiwa mmezaliwa wa tatu na wewe ndiye uliyekuwa wa mwisho tumboni mwa mama(miezi miwili) ndio baba akafa kwahiyo hujawahi kumuona baba yako wala baba yako hajawahi kukuona, halafu baada ya wewe kuzaliwa na miaka miwili baadaye mama akampata mzee mwenzake ambaye na yeye alikuwa kafiwa na mkewe lakini anawatoto wakaamua kuwa pamoja ili kumalizia uzee..
kwahiyo wewe unakuwa unamjuwa yule kama ndiye baba yako kwani alikuwa anakupa huduma zote za mtoto mpaka ulipoanza shule yeye ndiye aliyekuwa anakupeleka yani mlipendana sana kama baba na mwana wa damu, ndipo ulipofika miaka kumi mama alipokuambia ukweli kuhusu yule kuwa baba yako wa kambo.
baada ya maswali ya hapa na pale ukaelewa lakini bado ulikuwa na mapenzi sana na yule baba, miaka ikaenda mpaka ukawa unajitegemea na yey na mama yako wakawa wameshakaa miaka 20 pamoja, wakaamua kuwa na kampuni yao wakaajiri watu wengi tu na kampuni ikawa inafanya vizuri tu jijini lakini kasheshe zikaanzia....
pale baba yako huyo wa kambo kumpenda secretary wake na kutangaza naye ndoa, huku akiwa yupo na mama yako, na huyu secretary na yeye ndio anajifanya mapenzi motomoto na kuanza mpaka kumletea mama yako dharau wakati yule baba alivyoanza kuwa na mama yako alikuja na nguo zake tu akaishi kwenye nyumba ya mama yako mpaka wakaanza kupata hela nyingi na kufungua biashara nyingi huyu baba utamfanyaje ama huyu kimada wake utamfanyaje na baba amekomaa anataka kumuoa na ukiangalia ni mdogo sana kwa mama yako manaweza kulingana umri?????
HAYAKUSU! Full stop.
ReplyDeleteMaana mambo ya mama yako na mumewe wewe hayakuhusu chamsingi ni kuhakikisha kuwa interest za mama yako ziko covered, mfano uhakikishe mali zake ziko kwa jina lake na kama aliachiwa urithi wenu kutoka kwa baba yenu ni wakati wa kwenda kuweka caveat nyumba zake zisibadilishwe majina kama hamjachelewa. Otherwise mambo yao ya mapenzi hayakuhusu, wewe shughulikia haki zenu za msingi legally basi.