Monday, November 21, 2011

WANAWAKE..

Leo nataka kuongelea jambo moja ambalo sisi wanawake hulifanya bila kujuwa kama linawakera sana wame zetu.

Tunajuwa inauma sana mumeo anapokuwa amekukosea na maumivu na uchungu wake hauwezi kuisha mara moja kama wanaume wanavyodhani ama wanavyochukulia kwamba akishakuomba msamaha anategemea yameisha na uendelee na mapenzi kama mwanzo. Hawaelewi kama mwanamke akisema amekusamee ndio amekusamee lakini inachukuwa sana muda kufuta machungu yake moyoni.

Wanawake pale unapoamua kumsamee mumeo kwa kosa lolote alilokufanyia ambalo limekuumiza sana tusifanye kosa la kurudia mara kwa mara kumkumbushia, najuwa wanawake wengi hii ndio tabia yetu (hata mimi lakini najifunza kujirekebisha) nimegundua unapolirudia kwake mara kwa mara kwanza unakuwa umemsamehe kwa unafki halafu pili linakuzidishia uchungu moyoni na kukufanya uanze hata kumchukia mumeo na wajibu wako kama mke unakuwa unapotea huoni umaana wa kumhudumia tena vyema mumeo kama unavyotakiwa mwengine atakuvumilia lakini mwengine atatafuta pa kumalizia muda wake maana hatakai kurudi mapema maana anajuwa nyumba inawaka moto.

Narudia tena ni ngumu sana kusamehe na kusahau lakini ni rahisi sana kufanya hivyo ukiwa unataka kuokoa ndoa yako (kama kweli unampenda) na kuimarisha familia yako.

Tuache kukumbushia na kuchokonoa vitu ambavyo havitakupa amani.

Reactions:

1 comments:

  1. kusema la ukweli hili ni jambo moja gumu sana linahitaji uvumilivu wa hali ya juu, inabidi mtu ujicontrol sana hasira zako, na kila jambo mumeo analokosa usilichukulie kama vile "personal", take it easy ona kama kosa ambalo hata wewe unaweza ukalifanya. ukiwa hulichukulii kila swala kindanii na kuanza kufikiria ya kwako mwenyewe unakua rahisi hata kusamehe na kuweza kulisahau na kutoweka visasi ambavyo vinatuvurugia hizi ndoa zetu

    ReplyDelete