Sunday, November 20, 2011

TUACHE VISINGIZIO...

Natumaini wote ni wazima, leo nataka kuzungumzia swala la uzazi, na hili ni kwa wale ambao wameoana miaka mingi na mpaka sasa hawajabahatika kupata mtoto kwanza nataka wote tutambue ya kwamba mtoto hupewa na MUNGU, binadamu hufanya tu lile tendo lakini MUNGU ndiye anayeamua nani ampe mtoto,, wajinsia gani na kwa wakati gani.

Kama wewe ni mama mkwe unapitia kwenye hii blog na mkweo hajapata mtoto na kutwa unamsimanga imefikia mpaka kumshauri mwanao atafute mwanamke mwengine azae naye jamani juwa haipendezi na unajuwaje kama sio mwanao mwenye matatizo kutwa kumnyanyasa mtoto wa watu

Na wanaume kisa mkeo kachelewa kupata mtoto ndio unaanza visa mara unachelewa kurudi ukiulizwa unajifanya nyumba inaboa hamna makelele ya watoto, hivi unamshtumu mwenzio wewe umeenda kujichunguza kama huna tatizo maana wanaume wengi hufikiria wanawake ndio wanamatatizo na huwaacha na baadae husikia hao wanawake waliowaacha wamezaa baada ya kuwa na wanaume wengine.

Moja ya jukumu la ndoa ni kubebeana aibu, sio kuwekeana matatizo yenu barabarani, maana hata kama nyumba ina watoto pasipokuwa na upendo na amani kwenu nyie kwanza utaipenda bado nyumba hiyo?

Reactions:

3 comments:

  1. Asante sana...message imemgusa kila mtu.

    ReplyDelete
  2. Kweli kabisa tatizo wanaume huzani kwamba wanawake ndio pekee wanamatatizo ya uzazi na kuanza kutafuta vya nje hata kwenye vitabu vya dini ibrahim na mkewe sarah hawakupata mtoto kwa muda mrefu mpaka sarah alivyokuwa na umri wa miaka themanini lakini hatukuambiwa kama mumewe alimdharau ama kumfanyia vituko bali tunaambiwa abrahamu alimpenda sana mkewe mpaka saraha akawa anajisikia vibaya ndipo alipomshauri mumewe kulala na msichana wa kazi ili apate mtoto, na baadaye tunaona Mungu alimbariki sarah na uzee aliokuwa nao lakini alipata mtoto, kinachotakiwa kufanyika ni maombi sana kwani Mungu humpa mtu mtoto kwa wakati wake yeye.

    ReplyDelete
  3. watu husahau kuolewa ni sheria ila kuzaa ni majaaliwa.

    ReplyDelete