Jamani wimbo wa mwanamke usafi umeenea kila kona, ila wachahce wet undo wanaojua hasaa uswafi wa mwanamke, mwanamke usafi maana mwanamke kujikosha ukapendeza, mwanamke ukavaa nguo safi ukanukia, mwanamke ukalalia shuka safi, mwanamke ukapikia sehemu safi ilimradi cha mwanamke chochote kiwe kisafi, hata roho yako iwe safi hehehehehe kazi nakwambia.
Kufupisha story, mie naomba kushare na wanawake wenzangu kuhusu usafi wa mwili kwa leo japo kwa juu juu sitaki kuwachosha kuingia deep sana, nitakayoyasema haya na nyie muyaongezee na mengine basi ilimradi tubadilishane mawazo na kjiwe chetu hiki cha mwanamke nyumba.(rose mary ubarikiwe kutupa kijiwe hiki)
Kwa wanawake wa sikuk hizi sisi tulokua na majukumu kibao sio nyumbani tu hata inabidi tutoke tukatafute rizki huko nje huwa tunajisahau saaaana kwa kisingizio tuko busy, yes tuko busy wala sikatai lakini inabidi kwenye hiyo schedule ya ubusy tuweke ndani yake majukumu ya nyumbani.
Utamkuta mwanamke karudi kutoka kazini, siku nzima weee alikua kwenye mihangaiko, anarudi kafika kavua maviatu yake, mara huyo anaanza kukuruka kumtengea mr chakula, heeeh we vp? Na mijasho yako hiyo ya siku nzima kweli unamtengea mtu chakula, sura imemjaa mafuta (tena hasa wale wenye ngozi ya mafuta kaa mie hapa), shati ina kijasho jasho hata kama ulipaka body spray, au perfume au nini, u fresh wake si kama Yule aloingia akaoge akapaka tena. Basi na vunda lako la siku nzima unamtenega mr chakula, jamani haki kweli, we nenda hotelini, halafu mhudumu ana vumba, kweli hamu ya chakula utakua nayo? Au dada tu wa nyumbani na vumba lake huwa tunawatimua vibaya mno. Haifai wanawake wenzangu.
Mwanamke rudi kwako, ingia jimwagie maji( kwa bibi muhimu kupaosha lazima nalo hilo tulijeliongelea kwa mapana na marefu), wengine sie wagonjwa wa udi twajifukizaga (japo sio kila siku), toka mwenyewe msafi kamuandalie mr chakula kwa mbwembwe zooote, kitakachofwatia ni mada inayokuja!!!
We hebu tujaribu hili tuone kama mr. hali chakula kwa rahaaa zake.
Tum tum
0 comments:
Post a Comment