Tuesday, November 15, 2011

NI MKE, NI DADA WA KAZI..

Dada Rosemary,

Mimi ni mwanamke niliyeolewa lakini ndoa yangu hata raha siioni kama nilivyotegemea wakati naingia kwenye ndoa, nilijuwa itakuwa yenye furaha, upendo tutazaa watoto yani tutakuwa na raha kama tupo mbinguni lakini kumbe nilikuwa najidanganya mume wangu huyu mwaka wa kwanza baada ya kunioa amekuwa mchungu kama shubiri ule utamu wake wa asali aliokuwa nao zamani nauota tu kwenye ndoto sasa.

Mwaka wa pili huu wa ndoa simuelewi kabisa huyu kaka na wala sielewi nafasi yangu kwenye doa hii ni kama mke ama dada wa kazi, maana hanithamini, wala sitakiwi kushauri lolote anachotaka yey ndio kiwe hivyo, anarudi usiku wa manane na mara nyengine anarudi asubuhi yani vituko kwakweli haviishi nikimuuliza kwanini anafanya hivi hamna lolote la maana analonijibu.

Nataka kutoka kwenye ndoa yangu hii maana naona nateseka tu sipati faraja, ila naogopa kwanza ni mjamzito wa miezi sita halafu jamii itanichukuliaje nimeolewa mwaka pili nimeachika naombeni wazo kutoka kwenu nahisi kuchanganyikiwa.

Reactions:

1 comments:

  1. Pole sana, kuna njia nyingi za kutatua matatizo ya ndoa..kwa upande wangu naona hivi, kama inawezekana nenda kawaeleze wazazi au ndugu wa mwanaume wale ambao unaona wanaweza wakakaa chini na kuongea na mtoto wao. Ikishindikana unaweza nenda kuongea na viongozi wa dini ili upate ushauri wa kiroho. Mamii kuvunja ndoa si kutatua tatizo..ndoa ni uvumilivu na katika hili lazima uwe na PhD ya uvumilivu...wenzetu wanasema hivi.."LOVE IS NOT A PLACE TO COME AND GO AS WE PLEASE"..Na pia watu wengi hupiga goti kupata wachumba na pindi wanapofanikiwa husahau kabisa kumshirikisha Mungu katika maisha yao hasa baada ya ndoa..Sasa basi ningependa kukushauri uanze kumuomba Mungu wako...Yeye husikiliza sala za kila mtu na wala habagui..Usikate tamaa kwani hivi ni kama vijimambo tu...Mungu akatungulie katika kipindi hiki kigumu

    ReplyDelete