Monday, November 14, 2011

CHONDE CHONDE USHOSTI HUO UTAKUPONZA....

Nimegundua kwamba ndoa pia mara nyingi huvunjika kwa sababu ya mashosti tunaokuwa nao jamani wengine kweli mashosti wa ukweli wanakutakia mema na kwenye shida upo nao lakini shoga tambua sio anavyojifanya yupo karibu nawe ndio anakutakia mema kiukweli wengine wanafki laiti MUNGU angetuwekea vioo kwenye mioyo ndio ungegundua kama si watu.

Shoga yako unaweza mpelekea tatizo la ndoa yako ohhh mume wangu hivi wewe muangalie usoni atakavyolipokea, halafu subiri ushauri wake uone mnafki atakwambia mtafutie wmenzie huyo ama ndio kwavile mumeo anamfahamu basi ataneda kwake amjaze maneno ya uongo na umbea mumeo mara kutwa nyumba yawaka moto hata lije fire moto hauzimiki tuweni makini na mashosti.

Mashosti shoga kuwa makini nao ukimueleza jambo mara ndio unamuona ndio besty basi ni wanawake tulivyohodari kuongelea mambo mengine ya ndani kabisa mara ndio ukigombana naye anaanza kukutangazia kwa watu yule usimuone anacheka ............. na mumewe wala hawaeleweani kaniambia.............. haipendezi jamani.

Au ndio kisa umemuona fulani kafanikiwa wewe kama shoga badala umsifie hatakama hupendi moyoni unajuwa anastahili sifa zake unaanza kusonya na kumsemea mabaya kwani isingekuwa mumewe ama wazazi wake angefika hapo ama angepata hicho kitu, huo ni upashunaku mwanamke.

Mashoga wanaweza kuwa wazuri na ninavyosema mashoga sio wa kike tu hata nyie wanaume mnamarafiki wenu wa katibu angalieni siyo kila kinachong'a dhahabu vyengine shaba.

Reactions:

2 comments:

  1. Jamani hii ipo tena sana, mashoga hawa sio wa kuwaamini, shoga anamwambia matatizo yako kumbe mwenzio ndo kwanza anachekelewa, utamsikia oooh looh wako mwenzangu hafai wangu mie hawezi nifanyie hivo basi ilimradi kumponda wako umuone takataka umuache maana yeye huyo shoga akiwaona nyie mna raha yeye kinamkereta na kumsugua. Mkiachana burdaaaaani.akili kumkichwa na mashoga, chekeni yooooote lkn likija swala la mume sio la kutania. Binadamu sisi hatufai jamani, roho nyeusiiii kaa wapika sumu ptuuu...yarabi tunusuru na mashoga washenzi.

    ReplyDelete
  2. TumTum,

    Nilikumisije upo, naona umerudi kundini kwa nguvu zote karibu sana shosti. umeona mashoga walivyowanafki yani wao raha yao imuone mwenziye hafanikiwi si uchawi huu..

    ReplyDelete