Tuesday, November 8, 2011

NAKUTAKIA MEMA JAPO ULINISALITI...

Dada Rosemary,

kweli nimeamini kwamba nyie wanawake mna roho ngumu sana, yani ni wepesi sana kuwa na huruma na niwepesi sana kufanya yasiyo na huruma, sikutegemea kama mpenzi aliyesema ananipenda sana angenisaliti bila hata roho ya huruma.

nilikuwa na mwanamke mmoja nilipokuwa chuo, tulipendana sana, na kila mtu alijuwa hilo haswa marafiki zangu wale wa karibu, kwa muda wote niliokuwa chuo mapenzi yalikuwa matamu sana japo kulikuwa na kipindi ambacho mikwaruzano ilikuwepo lakini tulifurahia sana urafiki wetu.

nilipoondoka kwavile yeye alikuwa mwaka wa chini yangu akabaki chuo, tukawa tunawasaliana na kwavile alikuwa hostel basi nikawa naenda kumsalimia, akifunga tunakutana mitaani, kumbe mwenzangu wakati yupo chuo akaanza uhusiano na mwanaume mwengine pale chuo kwa siri uhusiano wao ukaendelea mpaka akapata mimba yani hata kuhisi ana mtu nje sikuwahi kumhisi maana nilijuwa tumeshibana.

kuna kipindi akawa hataki kabisa kuniona muda mrefu unapita hatujaonana, nikimuuliza ananipa visingizio vingi sana, basi sikuwa na lakufanya siku hiyo ndipo akaomba kukutana nami na kunieleza kwamba anaujauzito na anampango wa kuolewa na huyo mwanaume, yani niliaikia kama nimemwagiwa maji ya baridi kwani yeye ndio alikuwa tegemeo langu la kuwa mke, na sio hilo tu nilimuamini sana nikajuwa anajitunza kumbe anatunza mtoto wa mwanaume mwengine.

kweli wanawake nyie hamna roho ya huruma, mnapopata mtu wa kukupenda mnachezea upendo mnataka hao wa kuwadanganya mara kwa mara mnabaki mkilalamika kila leo, jirekebisheni sio wakati wote sisi wanaume ni wabaya.

Dickson

Reactions:

2 comments:

  1. Dickson pole sana..haya yote ni maisha..just let it go..YOU DO NOT DESERVE such kind of a person....Nakuomba usiwe judgemental hasa kwa wanawake kwa sababu kuna wanaume kama wewe tena wengi tu ambao walishatoa mapromise mengi kwa wasichana na baade kuwadamp. Things happen for a reason and neither a woman or a man can stop them from happening.Life goes on and i do believe you will find someone who will truly love you. But if you continue with such an attitude(being judgemental) u might loose the one who is ready to love you.

    ReplyDelete
  2. Dickson, hivi hujawahi kusikia wanaume wanaofanya kama alivyokufanyia huyo binti. Hayo yote ni maisha, Sahau, songa mbele. Yupo ambaye yupo kwa ajili yako anakusubiri.

    ReplyDelete