Tuesday, November 8, 2011

MWANAUME.....

wanaume wanaopita kwenye blog hii nataka niwaulize swali hivi mtu unakuwa anafikiria nini ama anatarajia nini pale unapopata mpenzi halafu bado anasoma kama secondary wewe unachukuwa jukumu la kumsomesha kipindi chote mpaka chuo, na kumuhudumia mahitaji yake yote kipindi chote hicho labda miaka sita na kuendelea na tatizo lake lolote unalibeba wewe na wala sio mchumba tuseme umemlipia mahari utamuoa atazilipia huko mbele kwa njia nyengine, na wala sio mkeo labda useme nikimsomesha na kumgharamia atawatunza watoto wetu wakati sipo hivi mnakuwa manfikiri nini?

halafu umeshafanya vyote hivyo mwanamke baadaye kapata kazi akapata mwanaume huko kazini kwake kamchanganya akili na sasa anataka kumuoa, anakuja kukueleza wewe unachukuwa uamuzi gani????

wanaume nimeona mwenzenu aliyekufa kwa ugonjwa wa moyo kwa jambo hilo kumtokea, hebu kabla ya kufanya hayo take a minute and think really deep anastahili yote hayo na atakuwa na wewe baadaye atakapofanikiwa...

Reactions:

0 comments:

Post a Comment