Monday, November 7, 2011

MIPANGO YA NYUMBANI INAPOHARIBIKA KABLA...

mimi ni mwanaume na ninakaribia kumuoa mchumba wangu wa mwaka na nusu sasa, kwakweli ninafuraha ila tatizo ni moja tu ya kwamba kati yetu ni mmoja tu ndiye anayefanya kazi na ni mimi, yeye yupo chuo mwaka wa kwanza.

sasa basi najuwa nijukumu langu yeye akiwa kama mchumba wangu na baadaye kuja kuwa mke wangu la kumuhudumia kwa kila jambo na kubwa ni la kifedha lakini anachonishangaza mchumba wangu huyu ni mbovu sana katika matumizi ya hela.

yani anapenda kwenda shopping mara kwa mara ananguo karibia sijui ngapi lakini kila wiki lazima anunue nguo, viatu sijui pafyum na vitu vingine kibao nikimuuliza kwa nini asiwe ananunua mara moja kwa mwezi ananiambia yeye ni mwanamke na kujiremba na kuvaa upya ni jukumu lake sio kama sisi wanaume unaweza kusubiri mpaka mwisho wa mwezi.

kwakweli nahisi kama hathamini nguvu zangu katika kutafuta hela za kutusaidia sisi pamoja na familia yetu baadaye, naogopa kama hapa hatujaoana ni hivi hayupo responsible je tukijaoana itakuwaje matumizi ya hela si ndio yatakuwa mara mia zaidi hata kama akiwa anafanya kazi bado nitakuwa na jukumu la kutoa hela kwake na kwa watoto wetu.

je kunasehemu ambapo ninaweza kupata counselling pamoja naye kuhusu matumizi ya hela katika familia?


2 comments:

  1. wanawake wengine ndio wako hivyo Kaka,ndio maana kabla ya kuoa wanaume tunatakiwa tuangalie vitu vingi kwa mwanamke,labda ameona unazo na je anakupenda kwa dhati?uangalie vitu vyote hivyo na labda hukuwahi kumwambia tangu mapema na mna umri gani?tuelezee zaidi,kama counselling utapata hapa tu,

    ReplyDelete
  2. Kaka pole sana...Sijui ulikuwa unamtreat vipi huyu msichana kabla ya yeye kuingia chuoni. Kama ulimpa kila kitu au ulimuonyesha kuwa pesa si tatizo kwako basi noana dada kanogewa na pesa.
    Pili huyu dada kwa sasa yupo chuoni na pale kuna competition kubwa sana, inawezekana na yeye anataka kujiweka katika level fulani ya maisha na hii ni hatari sana. Kwakuwa huyu mwanamke unampenda sana nakupa ushauri u jaribu kumpunguzia pesa unayompa. Kwa mfano kama ulikuwa unampa laki moja kwa mwezi mpe elfu hamsini.Akianza kukomplain muelezi hali halisi kuwa hapo ndo mwisho wako.Itakubidi ufanye hivi kwa mda mrefu mana huu ndo wakati wakujua kama anakupenda kwa dhati au ni kwa sababu ya pesa zako.Inakubidi uwe makini kwa sababu hata spending yako ya nyumbani ni lazima uibalance vizuri. Maisha kwa sasa ni magumu sana na un necessary spending is unacceptable.Kama huyu dada hataweza kuelewa basi nakushauri kabla ya kumuoa umtafute ndugu yake wa karibu hasa mmama aweze kumpa somo mwanaye otherwise you will be introuble.Huyu ni binadamu na anaweza kurekebishwa.Watu wengi sana hujisahau pale wanapoona wameridhika na maisha.Huwa inakuwa ngumu sana kwa watu kufocus na kuangalia maisha ya mbele yatakuaje.I wish you the best...

    ReplyDelete