Thursday, November 10, 2011

MWENZA ANAPOKUKOSEA...

kwanza nduguzanguni nataka wote muelewe hakuna moyo unaoweza kuona uchungu na raha kwa wakati mmoja, namaanisha nini, unajuwa wanaume wanataka kupandikiza kitu kwa wanawake kwamba wao wanaweza kufanya lolote na kutegemea wake zao kuwasamehe muda wote nitatoa mfano...

utakuta umeolewa na mtu ambaye sio muwazi anachotaka yeye kifanyike ndio hivyohivyo, yani labda ameenda kazini halafu anarudi saa nane usiku kwa tegemeo lake yeye anataka akifika nyumbani umpe pole ya kazi (ebo kazi gani hii mpaka sa nane usiku mlinzi???) umuandalie maji aoge na umtengee chakula....yani ndani ya akili yake hawazi kama wewe mkewe unamoyo sio chuma kwamba kitendo cha yeye kurudi usiku mara zote kinakukera na lazima pachimbike akija na hapo ndipo wanaume wanapoanza kuleta dharau kwenye nyumba na kuishi ilimradi siku ziishe.

sasa inapofikia hapo unafanyaje, hapo ndipo wanawake nao wanapoanza kuonyesha tabia zao mbaya na kuanza kuwaadhibu wame zao, ndio tunasikia yule bwana kalala hakuamka tena, mara tunasikia kamwagiwa maji ya moto kwenye uume na sasa tunasikia nchi gani mwanamke kamkata mumewe uume (jamani hii ni dhambi na ni unyama)..

kisa cha kumfanyia mtoto wa mwanamke mwenzio hivyo ni nini??? nimetoa mfano kwa wanaume lakini pia kuna wanawake pia wanafanya visa kibao kwa waume zao na wengine hata kuwapiga wame zao.

kama mwenza wako anakukosea, kwanza muelewe huyu ni mumeo ama mkeo usitake ukamfanyia kitu cha kumdharilisha kila akipita wa mcheke kovu kawekwa na mkewe, najuwa inauma sana hata miye nimepitia lakini tafuta njia nyengine ya kumpa adhabu isije kesho mapenzi yakawa motomoto ukaanza kujilaumu.

biblia inasema wanaume na muwapende wake zenu (kwahiyo wake muelewe lolote lile mumeo atakufanyia hata kama linaudhi hata akilala nje siku ngapi sijui MUNGU alishawawekea wakati wanaumbwa kwamba ni lazima akupende wewe na hata siku moja pendo haligawanyiki mara mbili huko kwengine ni akili tu inamtuma sio moyo).

biblia pia inasema wanawake muwatii wame zenu, (kwahiyo kaka hatakama mkeo akikutukana, akikuita majina ya ajabu akijuta kuolewa na wewe juwa hayo yote yanatoka akilini moyoni MUNGU alimuwekea utii wa ajabu ambao huuwezi kuupata kokote zaidi ya kwa ubavu wako).

Reactions:

3 comments:

  1. Nimeguswa, point za nguvu. Mungu atusaidie.

    ReplyDelete
  2. Nkwelikabisa mimi mume wangu alikuwa anarudi asubuhi,au anarudi mapema ikifika saa tano uck anaishia, inaumaje?lakin siku moja nilimkalisha chini nikamwambia aseme nini ambacho kinamfamya awe hivyo, je hao anaotoka nao toka ameanza kutoka kuna faida gani aliyopata, na kama namkera aniambie akaishia kuomba msamaha wa machozi,na mpaka sasa tupo saafi kabisa, ila yote haya yanawezekana kwa kusugua goti mbele ya MUNGU, na usiwe na papara kwenye maamuzi

    ReplyDelete