Dada Rose,
natumaini u mzima, dada mimi nimeolewa na nipo kwenye ndoa mwaka wa tatu sasa, mume wangu kabla ya kunioa alikuwa anaishi na wazazi wake lakini akaniambia baada ya kunioa angeama kuelekea kwake ambapo ndio anamalizia ujenzi wa nyumba yake, na kipindi cha uchumba wetu hakuwahi hata siku moja kunipeleka anapojenga kila mara nikimwambia ananiambia yupo busy mara visingizio vingi kwakuwa hatukukuwa tunaishi wote sikumata muda wa kuwa king'ang'anizi.
baada ya harusi yetu kwakuwa nyumba ilikuwa haijaisha baada ya honeymoon ikabidi tukakae kwa wazazi wake kwa mwezi mmoja, ndipo nikagundua alipokuwa anajenga mume wangu ni nyumba ya nne kutoka kwa wazazi wake!!!!!!!!!!!!!!!! nilishangaa, nikawaza sijui maisha yatakuwaje kuishi na wakwe na nimeshaolewa naye na siwezi kurudi nyuma.
nyumba ikaisha tukahamia kwetu tukawa tunaishi tu vizuri, ila kilichokuwa kinaniboa mara sijui ndugu zao gani wamekuja kutoka kijijini wanakuja kulala kwetu, ikitokea shughuli ya familia lazima wageni wa kulala wiki wawepo nyumbani yani sasa imekuwa nyumba ya ukoo wakishajaa kule kwa wakwe wanaletwa kwetu kwakuwa ndio karibu!!!!
sasa mwaka wa pili ya ndoa yetu mikimiki ikaanza kila nikipeleka matatizo kwa wake mama mkwe ananiambia wewe vumilia tu huyo ndio mumeo halafu wala hawayatatui kila mara ni hivyohivyo siku moja yakanizidi ikabidi niyapeleke kwetu wakaitwa kikao yakaongelewa na kukuta mtoto wao ndio mwenye matatizo basi ile kuambiwa kuomba msamaha tulipotoka pale mama mkwe mpaka leo hii haniongeleshi.
juzi mume wangu kaja kakasirika ananitukana nimemsema vibaya mama yake kwa shoga zangu eti wameenda kumwambia wakati ni uongo yani yule mama watu wanavyoniambia ananichochea mambo mengi kwa mume wangu ili aniache, na mume wangu namuona kweli kabadilika kila siku ananiambia umenitukania mama aliyenileta duniani utaisoma jeuri yako!!!!!!jamani
kwahiyo namsikilizia tu siku ambayo atanifukuza kwa kumuachia mama yake kuvunja ndoa yetu, jamani wanaume mnapoamua kuoa kaeni mbali sana na wakwe na sio kwa mwanaume tu hata wanawake pia.
Fatma
Fatma, kama ndio jina lako kweli, basi wewe kama mtoto wa kiislam rejea kwenye mafundisho ya dini yako na uangalie yanasemaje kuhusu mama. Labda nikwambie kwa kifupi tu kwani nawewe siku moja utakuwa mama kwa hiyo ni vyema ujifunze haki za wazazi katika uislam na hasa mama ni zipi. Mke ana haki zake, na wazazi wana haki zao.
ReplyDeletePili mshukuru sana mumeo kwa kuwajali wazazi wake na pia kumjali zaidi mama yake, hii itawafanya watoto wenu kujifunza jinsi ya kuwajali na kuwathamini wazazi kutoka kwenu. Tukirudi kwenye dini ni amri ya Allah Subhana wataala kuwatendea wema wazazi wawili. Na "pepo ya mumeo iko miguuni kwa mama yake", hatakiwi hata kumguna tu mzazi wake ni makosa makubwa sana. Anatakiwa kuhakikisha wazazi wake wanakula vizuri kabla yake yeye mwenyewe. Utajifunza mengi kupitia Quran na hadith kuhusu uzito wa mama, tena aliulizwa mtume SAW kuhusu baba na mama nani ana nafasi zaidi akajibu mama, akaulizwa tena akajibu mama, mara ya tatu akajibu mama, mara ya nne ndio akajibu baba.
Tukija kwenye tatizo lako inaelekea una katabia ka uchoyo kwani ndoa za kiafrika ni wewe, mume na familia, hao wageni wanaokuja kwa sababu maalum na tena wanakuja kulala kwenu iwapo tu kwao na mumeo kumejaa wanakukera nini? Je ndugu zako hawaji nyumbani kwenu? "ukipenda boga upende na ua lake" sio wewe nduguzo waje lakini wakwake wakija roho inakuuma. Na hili ni tatizo la wanawake wengi sana na si lako peke yako, na linatokana zaidi na choyo na ubinfsi.
Mimi ndugu za mume wangu wanaingia na kutoka na wapo wenye matatizo na wako ambao hawana matatizo kama ilivyo kwa ndugu zangu mimi mwenyewe wako ambao wako ok na wako wenye kupenda vijimameno na kuzua tafrani. Na sichagui yupi wa kumsaidia awe wa kwangu au wa mume wangu kutokana na jinsi mtu mwenyewe anavyojiweka kwangu. Cha msingi ni wewe kubadilisha attitude yako kwani ikiwa hupendi wageni haijifichi inajionyesha wazi wazi kwenye sura na matendo yako. Badilika watreat wageni na ndugu za mumeo kama nduguzo uone na jinsi wazazi wa mumeo watakavyobadili na wao mtazamo wao kuhusu wewe. Kimsingi ungekuwa mke wa mwanangu ningemwambia "badilisha kizingiti cha mlango wako hakifai". Subira
jamani wanawake tuna shida gani? mimi nimeolewa jamani nianze kusema hivyo kwahiyo haya ninayochangia nipo kwenye ndoa. Nikuulize wewe dada ulitaka uishi wewe mwenyewe na mumewo tuuu? kwani wakati anakuchumbia hukuona kama ana ndugu? au ndo unataka kuleta tabia za magharibi za kuishi wenyewe na kusahau Afrika we have extended family? Jifunze kuishi na watu hususani mama mkwe embu wapende mawifi na mashemeji, unataka wakija mjini au watu wakapange guest na nyumba ipo? Jifunze kuwe na mawasiliano mema na mama mkwe, wewe unataka kijana amwache mama yake na asimpende? jirekebishe
ReplyDelete