Thursday, November 10, 2011

MTU KATI KWA WENYE NDOA NA WANAOINGIA..

wote manaoingia kwenye ndoa na walio kwenye ndoa nataka muelewe kwamba ndoa sio mchezo wa kuigiza kwamba script ikiisha mnarudi maisha ya zamani hapana.

ndoa ni mlima mrefu sana ambao kuupanda kwakwe unahitaji uwe umejipanga sana kukabiliana na lolote lile litakalokuja mbele yako, kwanza ukiangalia mtu huyu hamkukuzwa wote kila mtu kalelewa kivyake na maadili ya kwao kwahiyo tegemea mikwaruzano mikubwa sana kutokea.

na pili utakapojuwa matatizo ya mwenzako basi beba ulie msalaba wake kama wako mkiendelea kuyatatua wenyewe nyumbani na mnaposhindwa basi yapelekeni kwa wazee ama kwa watu waliokuwa kwenye ndoa miaka zaidi ya kwenu, hata siku moja usipeleke matatizo kwa watu ambao walishakuwa na ndoa halafu wakaachika kwani hawa ni sawa na asiyekuwa na ndoa maana atakusaidia nini wakati yeye yalimshinda???

ndoa nyingi zinaendelea kuvunjika kwa kuwaruhusu wasio na ndoa kutatua matatizo yetu kisa ni dada yako, mama yako, sijui shoga yako ebo... sasa ndio yale ukienda kumwambia mume wangu anamwanamke nje atakwambia na wewe tafuta mwanaume, ukimwambia mume wangu anarudi saa nane usiku utaambiwa na wewe rudi mkutane mlangoni, yani hamna ambalo atakushauri la kujenga ndoa yenu.

Tutafute watu wenye ndoa wanaoelewa uchungu unaopitia na tunaposhauriwa basi tujaribu kuyatekeleza japo mengine ni magumu huku tukimuomba MUNGU kwani binadamu ni nini mbele ya MUNGU??? yeye peke yake ndiye anayeweza kumbadilisha binadamu, wewe mwenyewe huwezi hata ukienda kwa mganga sanasana atakulia hela tu.


Reactions:

1 comments:

  1. mwanaume ama wanamke aliyevunja ndoa yake hawezi kukushauri lolote jema kwenye ndoa yako ni vizuri kufwata na wale wazee watu wazima wao wana hekima nyingi sana watatutalia vyema matatizo ya ndoa.

    ReplyDelete