Monday, November 14, 2011

MKE WANGU ANITIA AIBU...

Dada Rosemary,

Leo naleta mada hii kwenu mnisaidie jamani maana najuwa hapa watu hujifunza mengi na hushauriwa mengi na watu pia leo mimi tatizo langu ni mke wangu ananitia aibu sana kwa ndugu na majirani.

Kwanza mke wangu hana upendo kwa ndugu yangu yoyote hata mama yangu mzazi yani hata mmoja akija utamsikia siku nzima analalamika kwanini waje, ikitokea ndio wamekuja kutoka kijijini kusalimia hata wiki yani hiyo wiki nzima nakoma maana nanuniwa nikimuongelesha najibiwa vibaya tena kwa dharau na mara nyengine mbele ya huyo mgeni wangu ikifika ya chumbani ndio hataki hata kunipa unyumba yani vurugu tupu mpaka namuuliza kwani wewe moyo wa huruma huna kwanini unakuwa kama na wewe hujazaliwa na binadamu na kuishi na ndugu? anachonijibu eti hapa ni kwangu na wewe na watoto wetu sio mtu mwengine maana kutwa hawaishi leo kaja huyu kesho yule keshokutwa utasikia mwengine anapita sitaki mimi nilikuoa wewe sio ukoo mzima.

Ukiacha tu kwamba hapendi ndugu zangu mke wangu huyu jamani hapatani hata na majirani zangu yani nimeshahama nyumba kama sita kwa sababu yake, kila mara anakuja kusutwa nyumbani mara tatu nimeshakuwepo akisutwa ukiacha hizo ambazo nazisikia kwa majirani, jamani hii si aibu, nimeshalipa faini kwa wajumbe mpaka nimechoka siku kagombana na mwanamke mwenziye mpaka kupelekana polisi. Nawasikitikia wanangu wasije kuwa wakubwa na kuaibika na hii tabia ya mama yao.

Aibu hii nitaibebea wapi ama nifanye nini arekebishike?

1 comments:

  1. Ukishakosa radhi ya mama yako, ukawa huna mbele wala nyuma huyo mke ataondoka na kuolewa na bwana mwingine. Wanaume wengi wana matatizo kama yako lakini wanachofanya ni kuwa na msimamo na kumueleza mke nafasi yake kama mke na nafasi ya mzazi, hasa mama. Ungekuwa ni muislamu ningekushauri umuite mtu mzima anayefahamu vizuri sheria ya dini inasemaje kuhusu wazazi, na pia jaribu kuwashirikisha wazazi wake kwenye hili.

    La sivyo kama uko very strong na unajiamini subiri siku wakija wazazi au ndugu zake na wewe uanze vituko kama vyake na pengine kuzidi. Tena asubuhi unaondoka huachi matumizi, unawanunia wazee wake, yeye mwenyewe humsemeshi akikuuliza kitu unamjibu kwa jeuri tena mbele ya ndugu zake. Hilo litatibu ugonjwa wake maana ndugu zake lazima watamuuliza na watakuuliza na wewe tatizo ni nini? Na hapo ndipo utakapowajibu kuwa hivi ndivyo mwanenu anavyomfanyia mama yangu nimetaka na yeye afeel ninavyojisikia akimfanyia mama yangu vituko. Lakini jiandae si unajua mtenda akitendewa?

    ReplyDelete