Monday, November 14, 2011

TABIA YAKO WEWE MAMA IKOME..

wanawake nimegundua wanaume wanalalamika sana kuhusu mama kuwa mvivu kwenye nyumba, jamani biblia inasema MUNGU alimuumba mwanaume na kwenye ubavu wake akamtoa mwanamke awe msaidizi wake. sawa yote haya ya ndoa yanakuja ili wewe mama ukawe msaidizi wa mumeo sio unakaa unauza sura tu hapana, mtanisamehe nakuwa mkali kwa hili.

Kama unauwezo wa kuweka msichana wa kazi basi shukuru MUNGU na usimfanye huyu msichana wa kazi ndio mama mwenye nyumba maana wengi tunajisahau mara zote msichana wa kazi ndio amuhudumie mumeo eboo kwani kamuoa yeye, yule ni msaidizi wa nyumba na sio mumeo!!!!! maana wanawake tumejiachia hata maji mumeo akitaka mpaka umuite dada kila siku ampe kwani wewe hujui raha ya mumeo ni wewe kumtengea chakula... sasa wote mnafanya kazi dada apike chakula hata mkirudi nyumbani unashindwa kumpakulia mumeo chakula na hiyo pia afanye dada mara dada kainama shati limepanda baba kaona shanga akazitamani na wewe kiuno chake cheupe mkilala kitandani ukapapasa huji baba nani mamam nani inahusu..

wewe goti ama kumkaribisha baba kwa sauti ya mahaba huna utasikia baba fulani chakula tayari haya dada kijijini wamefundishwa kila unapoongea na baba goti mpaka chini na kwasauti nyororo sio papara kama fisi kaona nyama. ndoa nyingi wanaume wanalala na wasichana wa kazi sio kwasababu hawawapendi wake zao nikwasababu mama jukumu lako la kuwa mke unampa msichana wa kazi.

Kuna kama kufua nguo, kuogesha watoto, kuosha vyombo sijui usafi wa nyumba hivyo muachie dada lakini kumtengea mumeo, kumuwekea maji ya kuoga, kufua nguo zake za ndani zote ni zako mama(maana sikumoja nilimsikia mama mmoja anasema yeye mpaka nguo za ndani za mumewe sijui kaptula za kuvaa ndani ya suruali anampa dada eti zile sio chupi) hapana mnajidanganya zile unafuwa wewe mama sasa unataka dada asikie harufu ya mumeo? harufu asili ya mumeo unatakiwa uijuwe wewe mama sio dada.

Siku moja rafiki yangu ananiambia karudi nyumbani alikuwa ameanika nguo za ndani za mumewe kwenye kamba anamkuta msichana wa kazi na chupi ya baba anainusa huku akiikumbatia kwa mahaba ebooo!!!! eti nikamuuliza akanijibu nilikuwa nahisi inanuka sabuni nikataka niiweke kwenye maji, pumbafu kabisa na yeye akaridhika na jibu lake. kwanza unashika chupi ya mume wa mtu kwa mpango gani inanuka sabuni inanuka nini sijui inakuhusu nini na anafuwa mke wake, hawa ndio wale wadada wanaotamani wame wa mabosi zao ndio wakitekenywa kidogo tu hao wamefika.

Wanawake kueni makini tambua mipaka ya dada na umuwekee aelewe na wewe utambue mipaka yako, mumeo alikuoa wewe akitegemea ndio tegemezi na msaada kwake basi tambua wajibu wako.


Reactions:

1 comments:

  1. Tena akome akomae kabisa. loooh hatuoni haya si wanawake, mwanaume sio ndugu yako yule mpaka akustahamili hivo, ulivompata wewe na wengine kibao anaweza wapata cha muhimu ni kujitahidi kumuweka hao wemgime awaone takakata sio tena ndo unaitanuuuua unaona ndoa ndo kikomo.......... likikuchoma lako hilo na ujirekebishe.
    TUMTUM

    ReplyDelete