Sunday, November 13, 2011

MDOGO WANGU UNATAKA UPEWE?

Jamani hii ni kali kweli kuna watu wanaweza kufanya hivi kwa kaka yako wa damu?

Rosemary,

Natumaini wewe ni mzima na familia yako, sasa dada leo naleta mada hii kwenu mnisaidie na mnieleze kama hii ni haki huyu mdogo wangu wa kike anavyonifanyia.

Yani kila mwanamke ninayekuwa naye yeye hamtaki, anaipa maneno ya kuhusu kila mwanamke nitakaye kuwa naye, na mara nyingi nimekuwa nikimsikiliza na kujikuta na achana na kila mwanamke mara kwa mara. Sasa nimepata mwanamke ambaye ninampenda kwa mapenzi ya ajabu yani nataka yeye ndio awe mke wangu lakini kama kawaida mdogo wangu ameshaniambia mambo machafu kibao kuhu yeye na kunisisitiza nimuache nitafute mwengine.

Kilichoniuma zaidi na kujua kama siku zote alikuwa ni muongo ni juzi nilisafiri kwenda zanzibar kwasababu mwanamke wangu anakaa kwao nikamuomba twende wote bila kwetu kujuwa, basi wiki nzima nikawa naye kule siku ya tatu baada ya sisi kusafiri akanipigia ananiambia kaka yani hapa ninavyoongea na wewe namuona wifi kakumbatiwa na mwanaume anambusu na kumshikashika!!!!!!!! kwakweli yani nilitamani kumtukana.

Nilichomwambia mimi mbona wifi yako ninaye hapa mara akaniambia labda nimemfananisha lakini kama yeye kweli kabisa, mmmhhh ndipo nikaanza kuhisi yote aliyokuwa ananiambia nyuma kuhusu wanawake zangu ni unongo sasa ananifwatafwata nini???

Tulivyorudi kaanza kumfanyia mwanamke wangu vituko mara akipita amsonye, mara azungumze maneno ya kwamba haolewi mtu hapa, yani na kero kibao mpaka mwanamke wangu sasa anataka tuachane, hataki kuolewa na mimi anasema kama uchumba tu ndio hivi je akiolewa si ndio itakuwa balaa.

Nikamuomba anipe muda kidogo nitamjibu basi mimi nikamuandikia barua ya mapenzi mdogo wangu kwamba nipo tayari kuwa naye kimapenzi na nitamtimizia haja zake maana nami siku nyingi nilikuwa na hamu ya kukutana naye kimwili sema nilikuwa sijui la kufanya mpaka alivyonionyesha anataka, yeye baada ya kusoma hiyo barua akakasirika na kuipeleka kwa wazazi ikawa kesi ya hali ya juu.

Baada ya kuitishwa kikao na ukoo kwanini yametokea hivi eti anasema wasichana wote wa kaka sijaona hata mmoja anayemfaa sijui anatoka nao wapi ndio maana sipendi awe nao, sasa unatake? kama kaka ameamua kuoa aoe tu hayo ni maisha yake lakini kama mdogo wake nitamwambia!!!!

Hivi huyu ananitaka nini mimi?

FrancisReactions:

1 comments:

  1. wewe ndo mwenye uamuzi wa kuoa, na ni mtu mzima kwa nini ushikwe masikio? kwa nini mtu akuamulie maisha yako?. kama huyo mdogo wako unaishi nae mrudishe kwa wazazi wako. waambie umeshindwa kuishi nae. kisha muombe msamaha mwanamke wako umpose mfunge ndoa

    ReplyDelete