Friday, November 11, 2011

HUYU MUME VIPI JAMA...

Dada Rose,

wenzangu wa blog hii naomba msaada wenu yani mume wangu hata simuelewi yani wanaume sijui mkishaoa huwa mnatatizo gani, yani kila mwanamke lazima awe analia na ndoa yake sijui vipi.

mume wangu jamani ana magari matano yote kayafanya tax na bodaboda tano lakini jamani huyu kaka sijui ana roho mbaya ama vipi nashindwa kabisa kumuelewa yani hata kusema ampe mkewe gari hata moja ama aninunulie langu wala hasumbuki halafu cha kunishangaza anawaambia madereva wake hata mke wangu akipanda humu lazima alipie.. jamani hii si balaa

inaniuma sana nikiona wenzangu wamenunuliwa gari na wame zao, yani hapa nilipo nina mimba ya miezi mitatu lakini napanda basi mwennzenu, ndio nikitaka kuchukuwa tax lazima niilipie hiyo ya mume wangu wakati mwanaume hata hela hanipi, wala nyumbani haudumii kila kitu nafanya miye huu si wazimu? na mwisho wa wiki hela zake akipata wala kusema mke wangu hii unywe soda ama ya kupika nyumbani hamna jamani huyu sijui anamatatizo gani. mpaka wakati mwengine najuta kuolewa naye nataka tu kuondoka maana huu ni utumwa ama mimi tu ndio naona utumwa?

Rukia


3 comments:

  1. pole sana dada,ila je kuna lazaidi la hili uliyotuambia hapa?

    ReplyDelete
  2. Rukia unajua kweli haki zako za ndoa ni nini? Kama ni ndoa ya kiislamu hizi ni haki zako za msingi, kama hujui ingia Alhidaya ukasome ni nini mume anatakiwa amtimizie mke wake na kama asipotimiziwa hayo mke ana haki ya ama kudai talaka au yeye mwenyewe kujivua kwenye hiyo ndoa (Khula) au kiufupi kutoa talaka. Na mojawapo ya masharti hayo ni chakula. Sasa kama hata chakula hanunui na uwezo anao wewe unapata wapi energy ya kufanya nao tendo la ndoa mpaka na mimba umebeba bila ya kula? Nimeuliza swali kuonyesha simple logic ya wajibu wa mume kununua chakula cha familia yake, na kuna hatari kubwa ambayo wanaume wengi huwa hawaioni. Kukosa kutimiza mahitaji ya chakula majumbani mwenu hupelekea baadhi ya wanawake wengine kuzini na wanaume wa sokoni, buchani na hata wa magengeni.

    Nyie wanaume msiotimiza wajibu wenu, unarudi jioni unakuta chakula kiko mezani hujui kimetoka wapi au kimepatikana vipi yet unakaa kitako na kula bila hata ya kufeel remorse? Pengine mwanaume mwenzio kampa mkeo hicho chakula kwa ujira wa ngono je? Subira

    ReplyDelete
  3. duh,hii kali kwani uko hukumuona tabia zake kabla hamjaoana?ama ndo nyie mnaokimbilia kuolewa,

    ReplyDelete