Thursday, November 3, 2011

HII NAYO VILEVILE TU...

Dada Rose,

habari za muda huu natumaini wewe na familia yako wote ni wazima, dada kuna siku ulishawahi kutoa mada moja inayohusu dada mmoja aliyetoa sana mimba kabla hajaolewa na sasa ameolewa amebahatika kupata mimba japo yupo bedrest muda mrefu, kwakweli watu walimshauri vizuri na ndio maana nimeona na mimi nitoe tatizo langu ambalo limenisumbua kwa muda mrefu ili niweze kusaidiwa.

katika usichana wangu mpaka naolewa dada sikuwahi hata siku moja kutoa mimba, nilikuwa najiheshimu sana na kuogopa sana wazazi wangu wangenifikiriaje kupata ujauzito kabla ya kuolewa, sasa basi namshukuru MUNGU nimeolewa na kaka huyu ananipenda sana kwakweli.

kasheshe ni kwamba mimba hazikai jamani, yani nimeshabeba mimba mara tatu ikifika mwezi wa nne mimba inatoka, ndoa yangu sasa inamiaka saba na mimba ya mwisho niliiibeba miaka mitatu iliyopita, na kinachonichanganya zaidi muda wote huo mpaka leo hata hiyo ya kubeba na itoke sijaipata sijui imekuwaje mwaka wa tatu sasa.

watu wananiambia eti labda kwasababu nin amawazo sana ya kutaka mtoto ndio maana mimba hazishiki je hii ni kweli? na kwanini mimba zitoke wakati enzi na usichana wangu sikuwahi kutoa mimba????????

naombeni wenzangu wa kijiwe hiki mnifahamishe ama kama mnamjuwa hata daktari pia mnielekeze mwenzenu.

Salha.

2 comments:

  1. Dear Salha, Pole sana hiyo hali hata mimi ilinitokezea na niliambiwa kama fuko langu jepesi, basi zimetoka mbili halafu ya tatu nikaanza kubleed nikapewa bedrest alhamdulillah nikapata mtoto na ya mtoto wa pili na watatu pia full bedrest hata kwangu nilihama nikahamia kwetu ili tu zitulie, hata kufagia nisifagie, hata kitanda nisitandike na bwana ndo kabisa asiniguse basi alhamdulillah nnao watoto watatu na dawa za mabibi za kuchemsha pia zinasaidia. Kila la kheri. Amua mtoto ndo kila kitu katika maisha. Aisha R. Suleiman - Zanzibar

    ReplyDelete
  2. Dada pole sana...Nakushauri uende hospitali kupata ushauri zaidi.Wanawake wengi huwa wana haya matatizo na kwa jinsi ninavyofahamu wengi wao huwa wanaweka appointment na GYNECOLIGIST...lakini pia usiache kusali Mungu ni mwema na anajibu maombi..

    ReplyDelete