Monday, October 31, 2011

RAHA TULIZIPATA WOTE...

Dada Rosemary,

natuma hii story kwenye email yako ili unisaidie, naomba usionyeshe email yangu kwani utanifanya nifukuzwe shule maana wanafunzi wengi humu shuleni wanasoma blog yako na wengine mashoga zangu kwahiyo ukionyesha email watajuwa na nitafukuzwa shule kabla ya kufanya maamuzi.

mimi ni msichana wa kidato cha sita, nimekuwa na uhusiano wa kimapenzi na mume wa mtu kwa miaka mitano sasa, huyu baba ananihudumia sana kwakweli sitaki kumuita buzi langu kwakuwa namuheshimu maana kama ni hela ananipa sana za kunikimu nikiwa shuleni maana nipo hostel, ananifanyia shopping kila week end na simu kutwa ananiwekea hela nipate kuongea naye, kwa kifupi nafurahia sana uhusiano wetu.

siku zote hizi nikiwa naye huwa natumia vidonge vya uzazi wa mpango kwahiyo tukikutana kimwili sipati mimba maana tuliacha kutumia condom baada ya kuzoeana sana, muda wote huo wala sijawahi kushika mimba na wala hatukuwahi kuachana.

sasa mwezi uliopita nilipitisha siku zangu za hedhi mara ikafika mwezi nikajuwa labda ni vile vidonge ninavyotumia maana siku nyengine naweza pitisha hata miezi miwili sijapata siku zangu, miezi minne sasa sijaona siku zangu ndipo nilipoamua kununua UPT na kupima na kujikuta nina mimba, na wala sina mwanaume mwengine zaidi ya huyu mume wa mtu.

kwakweli nilishtuka maana nipo shuleni nitafanyaje maana wazazi wangu wakijuwa wataniua, ama kunifukuza nyumbani, nimempigia tuonane, alipokuja nilipomwambia nina mimba sikuamini macho yangu alivyonigeukia, yani kama sio yeye akaniambia nikaitoe nikamwambia naogopa akaniambia basi kama unaogopa kwanzia leo usinijuwe, na hiyo mimba sio yangu na wala hatujawahi kufahaminiana, tena usinisumbue maana nitakufanyia kitu kibaya, jamani!!!!! nilihisi naota sikuamini kabisa, nikambembeleza kwahasira akaondoka mpaka leo wiki ya tatu sijamuona wala kusikia simu yake.

napafahamu wanapoishi najishauri niende nikamfanyie vurugu huko na mkewe ajue kwamba alikuwa na mwanamke na ni mjamzito, lakini nasifikiria nikienda sindio naweza kuanzisha skendo mpaka wazazi wangu wakajuwa, nafikiria pia kutoa lakini naogopa dhambi ya kuua, na pia naogopa naweza kufa nikitoa nimechanganyikiwa kabisa mdogo wenu naomba ushauri wenu.

xxxxxxxx

Reactions:

8 comments:

 1. Siku hizi si mnaruhusiwa kusoma baada ya kuzaa, kwa hiyo mimba ni kubwa sasa na utaificha mpaka lini? Cha kufanya omba ruhusa uende nyumbani kwenu kamueleze mama yako mzazi usimfiche hata kitu kimoja na mhusika umtaje wala usimfiche.

  Tena wala usiende nyumbani kwake anaweza kukushtaki umeenda kumfanyia fujo. Waache wazazi wako wadeal nae maana wao ni mtu mzima mwenzao, na akikuta wazazi wako ni kama mie naona angeozea Segerea kwa kumpa mimba mwanafunzi. Ningehakikisha anafungwa ili iwe mfano kwa wengine kwa sababu yeye ni mtu mzima alipaswa akuongoze wewe na ujinga wako wa kitoto. Sasa kakae kitako ulee mwana huyo na shule utamalizia na mtoto mgongoni!

  ReplyDelete
 2. kuna wanaume wabaya,miaka yote hiyo 5,anakuhudumia kumbe rohoni mwake,hana mapenzi na wewe ni ame ku use tu.umemjua true colour yake ulivyomwambia una uja uzito wake.kwa nini bi dada ulikubali kuwa na mume wa mtu?au kwa kuwa anakuhudumia?ukiitoa,unaweza kujuta baadae.mtafute mtu mzima yoyote yule,aongee na wazazi wako,umuelezee situation yako, na huyo bwana mkomoe,sio yake yaendelee,wewe akuharibie yako tu.nina uhakika,akikuacha wewe atatafuta mwengine,na atamuharibia kama alivyokuharibia wewe.make sure mke wake anajua hiyo issue.

  ReplyDelete
 3. kusudi hua hayambiwi pole! Kama ungali tuliza akili yako ktk masomo yasingeli kukta ayo chamsingi na chasecondary wajuilishe wazazi wako kua unamimba nandio matunda ya hosteli ayo urudi kwenu ukalee mimba yako hadi utakapo jifungua utakua na akili ya kimaisha mana kama funzo ndo umeshalipata ilo mkikatazwa watotot waskuizi hamkataziki unaona kama unapitwa na wakati sasa wakati ndo ushakuwacha kabisa na tumbo ndo linazidi kukua bwana wawatu kaingia mitini....waeleze ukweli wazee wako

  ReplyDelete
 4. Duh nina binti na mimi nawaza ikinitokea hivi kama baba sijui nitamfanyaje,sikia wewe binti ushauri watu wameshakupa hapo juu,heshimu ushauri wao na mimi kama mzazi ingawa inauma,wewe nenda ukazae utarudi shule,acha kumfuatilia huyo baba wa watu,nimependa ushauri wa mtu hapo juu tafuta hata shangazi yako akaongee na wazazi wako,

  ReplyDelete
 5. pole mdogo wangu kwa mkasa huo, mm nna hasira na hyo bwana yeye hakujua mwisho wa cku kitakachotokea? watu km hao ni kuwaharibia tu coz kwa kosa hlo ni jela miaka 30,so fanya 2 mpango wazazi wapate taarifa coz mimba huwa haifichiki hta cku moja, plz usitoe hiyo mimba ingawa na shule ndo hyo dah mtihani huo, pole sana ila naamin umejifunza kuwa tamaa ni mbaya mdogo wangu

  ReplyDelete
 6. daaa kweli mshika mawili moja humponyoka!!!! hivi ni kwa nini nyie wanafunzi msitulie? ni nini kinawawasha? ona sasa uko form 6 unapata mimba kilichokushinda kuvumilia ni nini? pamoja na kwamba nishatokea hilo la kutokea wala usisubutu kutoa mimba nenda kawaeleze wazazi uanze kumwambia mama nae atamwambia baba yako, wwanaweza kukuelewa, then utajifungua na kuendelea na masomo baada ya kujifungua

  ReplyDelete
 7. Shosti wee pole....Mume wa mtu sumu au hujui hilo..sasa kwanza nakushauri usiitoe hiyo mimba kwa sababu the moment you decide to tamper with pregnancy anything can happen...and am telling u my dear u will live to regret 4 the rest of ur life..pile waambie wazazi..mimba ni 'CNN LIVE'...haifichiki...wao watajua ni jinsi gani ya kuhandle hii issue kwa sababu bado upo mikononi mwao ni ngumu lakn inakubidi ujikaze na useme ukweli....pole sana

  ReplyDelete
 8. please wasiliana nami kwa namba 076712084 tuma msg nitakusaidia jitahidi

  ReplyDelete