Monday, October 24, 2011

NIMESIKITISHWA SANA....

wapenzi wasomaji wangu kuna jambo limenisikitisha sana ambalo limetokea week end hii kwa mdada aliyekuwa anaingia kwenye hiki chama chetu cha ndoa, roho imeniuma nimeamua nije kuwasimulia ninyi pia na kutaka kuwashauri watu kuwa na msimamo katika mahusiano yao na kujua kusoma nyakati.

kuna dada mmoja yeye ni mwalimu na mchumba wake ni mfanyakazi katika bank moja hapa mjini, wapenzi hawa wamekuwa katika uhusiano kama miaka kumi sasa na ndipo wa kamuua kuoana mwaka huu ambayo harusi yao ilikuwa jumamosi ya juzi.

wakati wote wa uhusianao wao, mwanamke yeye anasema hakuwahi hata siku moja kutoka nje ya uhusiano wao, lakini kumbe yule kaka alikuwa na mwanamke wa mje ambaye mpaka jumamosi anaoa walikuwa wameshakuwa pamoja kwa miaka minne!!!!huyu dada anasema wala hakuwahi kujua maana mwanaume hakuwa na dalili zozote ambazo zinaweza kumuonyesha ya kwamba alikuwa anatoka nje, wala hakuwahi kubadilika katika mapenzi hata siku moja na hata kama wakigombana yani hakubadilika alikuwa vile vile kama alivyoanza naye mwanzao kwahiyo hata siku moja huyu dada hakujuwa kama huyu kaka alikuwa na mwanamke nje.

sasa kumbe huyu kaka alivyoanza kupanga mipango ya kumuoa huyu mchumba wake wa miaka mingi akamuarifu yule kimada wake kwamba mimi nataka kuoa, kwahiyo nitakuwa busy katika kupanga harusi ukiona siwezi kuwa na wewe muda mwingine ujuwe mipango imenibana, huku kimada akamueleza huyu jamaa ya kwamba hutaoa, kama huwezi kunioa mimi basi hutamuoa huyo mchumba wako labda hunijui. akawa anamwambia kwanini ampotezee muda halafu amuache kwenye mataa, huyu kaka akamueleza sinilikwambia mwanzo kwamba nina mchuma na ukanielewa sasa unabadilika nini lakini nasikia huku kimada akaweka msisitizo ya kwamba kama haolewi yeye basi hata huyo dada mwengine hataolewa.

yule kaka anasema alivyoona vile akaamua kuendelea kupanga mipango yake ya harusi huku hakumwambia kitu chochote yule mchumba wake, na yule dada kumbukeni hajui lolote kama mwanaume ana mtu pembeni, basi kwa vile yule kaka hakutaka matatizo hakwenda tena kumuona yule kimada zaidi ya kumpigia tu simu huku kila akiongea naye bado anasisitiza hataoa kama hamuoi yeye.

alhamisi iliyopita ndio ilikuwa send off ya huyu dada, asubuhi alikuwa mzima kabisa, akaenda salon kupambwa bado alikuwa mzima, mara alivyomaliza kupambwa akasema jamani najisikia vibaya, mara akaanguka, wakamkimbiza hospital, kufika akapimwa kila kitu hana anachoumwa, mara yule dada akaanza kulala mika anaumwa miguu, miguu ikwa miguu mpaka akashindwa kutembea (jamani inauma!!!) akawa analia anasema akisimama miguu inamuisha nguvu kwahiyo mpaka amuegemee mtu ndio akokotwe kutembea.

kumbuka hii ni siku yake ya send off sherehe haikuweza kusimamishwa maana watu walikuwa wameshaanza kufika ukumbini, masikini ikabidi apelekwe hivyohivyo akagoma kuingia ukumbini akawa analia kwa uchungu maana kila mtu alikuwa analia sasa maana hamna anayejuwa liliotokea ghafla tu wakati mtu alikuwa mzima, basi taarifa ikapelekwa ukumbini wakaadithiwa kilichotokea salon mpaka hapo alipo bibi harusi maaba watu walitokwa na machozi ya huruma lakini mc aliwashauri bibi harusi atakapoingia wajitahidi kuchangamka na kufurahia ili asijisikie vibaya.

baada ya kumbembeleza sana bibi harusi mtarajiwa akakubali kuingia ukumbini, akishikiliwa na matron na mama yake mzazi aliingia huku watu wakishangilia, wakicheza ili kumchangamsha, basi sherehe ikaendelea lakini yule dada aliketi tu kila kitu chengine akafanya matron, kama kupeleka keki kwa wakwe na wazazi wake na mengineyo. kwa kweli watu walijitahidi sana kuchangamsha hii sherehe wakati wa chakula ulipofika ilibidi bwana harusi mtarajiwa ndio aende mbele kumchukuwa mke wake wakali na sio kama utaratibu wa kawaida wa bibi harusi kumtafuta mumewe wakale.

basi wakamaliza kula wakati wa zawadi yule dada akaketi kwenye kiti kupokea zawadi zake, na yeye mwishoni akasema anazawadi ya kumpa mumewe mtarajiwa, ndipo akapewa kipaza sauti na kuongea kwa kweli hapa ndio kila mtu mwenye moyo usio wa chuma alipotoa chozi, yule dada akamshukuru sana mumewe na kumwambia anampenda na kumuomba msamaha kwa ghali iliyotokea kwani wote walitaka kufurahia sana siku yao lakini janga hilo likatokea na juu ya yote akamwambia anaujauzito, jamani watu walipiga vigelegele huku machozi yakiwatoka watu walilia jamani hata wanaume machozi yaliwatoka.

yule kaka akaenda kumkumbatia mkewe mtarajiwa akilia machozi kama mtoto, yani bestman akamtuliza lakini wapi alishindwa kujikaza yakawa yanamtoka tu na analia mpaka watu wakawa wanashangaa mc akasema aachwe tu alie atakaponyamaza tuendelee jamani yule kaka alitokwa na kiliao, kumbe alikuwa na lake moyoni.

ndipo akaomba kipaza sauti na kuhadithia story kamili kama nilivyowaambia, kaka wa yule dada wakaenda kutaka kumpiga shemeji yao yani ghafla hali ya hewa ikachafuka, jamani palikuwa pata shika nguo kuchanika, kwahiyo yule dada kalogwa??????? sasa kinachofwata ni nini??????? harusi inafungwa jumamosi ama akatibiwe kwanza????????

bado natafuta habari kamili nitawajulisha soon nikizipata.

hiyo picha hapo juu ni yangu nimeamua tu kuiweka kunogesha story.......


4 comments:

  1. huu ni unyama aisee, hivi kwanini tunashindwa kuwa waaminifu katika mahusiano yetu, ona sasa yanatokea kwasababu ya tamaa zetu, yani roho imeniuma sana. ingekuwa ni mimi huyo mwanaume sijui ningemfanya nini. hii ni aibu kweli dunia imefika mwisho, na nyie wanawake mnachezewa sana na mnajidharilisha sana unajuwa mtu anamchumba bado unamtaka, na sisi wanaume tupunguze umalaya tutakufa sio kila sketi unayoiona ni mwanamke wengine majini.

    ReplyDelete
  2. HAYA DADA MAMBO YA SIKU HIZI NI MAN TO MAN kwaani mambo ya vinyumbavidogo mbaka kwa wachumba pole sana ila mungu atamsamehe huyo dada na ampe nguvu

    ReplyDelete
  3. Ukweli nimeumia sana, pole mpenzi na Mwenyezi Mungu akutie Nguvu upate kusimama imara akuepushe na hizo nguvu za giza.

    Wanaume mnatuua kwa tamaa zenu, tafadhali kueni waaminifu katika mahusiano yenu. Mwenyezi Mungu ampe adhabu huyo dada aliyemtenda mwenzie asiye na hatia, kwani adhabu hiyo ilimstahili mwanaume wala c mwanamke mwenzie asiye na kosa.

    ReplyDelete
  4. Hapa mwanamme ndio mwathirika katika vita hii ya wanawake wawili wanaomtaka. halafu hii habari ya kuwa huyu dada hajawahi kufanya ni wimbo wa wanawake wanaodhani watu watawaamini. ifike mahali wawe wakweli. kwa kweli kama kungekuwa na namna ya kumwepuka mwanamke hakuna mwanamme angemsogelea mwanamke, maana ni kiumbe asiyekubali kosa kabisaa hata umshike red hand na mwanamke anayeingilia mahsiano ya mwanamke mwenzake anayelaumiwa ni mwanamme hata kama wote wanaona alivoshawishiwa. utasikia oo mbona hakukataa!! Ebo!! Ama kweli mwenyezi MUNGU ametupa mtihani mkubwa mmno wa mwanamke. Tuome MUNGU wasijemroga huyo mwanamme.

    ReplyDelete