Friday, October 21, 2011

MUME WANGU, MUME WANGU, MUME WANGU......

Dada Rosemary,,

natumaini u mzima pamoja na familia yako, nakushukuru sana kwa msaada unaotupa wote tulio na ndoa na hao wanaotaka kuingia kundini.

tatizo langu leo ni moja ambalo ninaomba wenzangu wanisaidie, nimeolewa nina miaka ishirini ya ndoa na tumejaliwa kuwa na watoto wa nne, mume wangu alikuwa anafanya kazi kwenye kampuni moja ya wazungu hapa jijini, ikatokea kashese pakaibiwa na wote kwenye kitengo chake wakakamatwa na kuwekwa segerea wakati uchunguzi ukiendelea kufanyika.

kwa kweli ilikuwa ngumu sana kwa familia yangu maana ndugu zangu walinicheka na kunisema wakawasema watoto wangu kwamba ni watoto wa mwizi na mambo mengine mengi lakini mimi sikujali nilichokuwa nafanya ni kumuomba MUNGU tu ukweli utoke kwani mume wangu aliniambia hakuiba basi nami nilimuamini.

muda wote akiwa jela nilikuwa naenda kumsalimia, nampelekea chakula na kumpa moyo kwamba siku utatoka mume wangu, akakaa ndani miaka mitatu ndipo alipotolewa baada ya utafiti kuonyesha kwamba hakufanya wizi na mwizi mwenyewe kukamatwa.

kwa kweli ilikuwa furaha sana kwangu na familia yangu maana baba amerudi nyumbani, basi kule ofisini kwake wakamrudisha kazini na kwa kuomba msamaha wakamlipa mume wangu millioni kumi, kwa kweli tulifurahi sana maana tulijuwa zitatusaidia sana.

kumbe nilijidanganya mume wangu baada ya kupata zile pesa akabadilika mpaka nikashangaa yani nyumbani halali na akilala anakuja saa kumi za usiku mwezi wa tatu huu tokea ameanza kazi hajawahi kula nyumbani hata siku moja sijui anakula wapi, cha kushangaza nikimuomba hata hela ya kununua nyama hanipi anasema tule matembele.

kunakipindi ndio akaja nyumbani kanunu unga karibia kilo saba, na mchele kilo tatu, mboga ndio anataka tule matembele hamna mboga nyengine, mpaka nifanye biashara ndio nikipata hela ninunue mboga na matumizi mengine ya nyumbani, yani amesahau kabisa nilivyokuwa namletea chakula kizuri jela na kumuomba MUNGU atoke yani katoka amekuwa balaa.

sasa juzi akaja mtu kuniambia mbona mume wako anakesha bar akiwa na mwanamke wanakula nyama choma na kuwapa ofa watu wengine??? kwa kweli sikuamini nikamwambia kwamba siku atakayokuja tena wewe niambie nie kujionea mwenyewe.

kweli siku hiyo nikaambiwa nikafunga biashara yangu na kwenda kujionea yani kama MUNGU sinia la nyama choma linashushwa tu na mimi na tia miguu, hasira ilinipanda ghafla nikajikuta nachukua lile sinia na kumwaga ile nyama chini na kuikanyaga isiliwe tena sijui nguvu nilitoa wapi nikamkunja mume wangu bahati mbaya akaniponyoka na kukimbia, na yule mwanamke wake naye akakimbia baada ya kuona vile, watu ndio kuja kunituliza baadae nikaenda nyumbani.

mpaka leo naandika hivi hajarudi nyumbani na sijui kaenda wapi, sasa nawauliza ndugu zake hii ndio ndoa nyumbani haudumii anaenda kumuhudumia malaya wake, jamani huyu mwanaume nimfanye nini mimi maana naona hata ndugu zake hawanipi mawazo ya kueleweka.

Reactions:

4 comments:

 1. Pole sana kwa maisha yaliyokusibu mpaka sasa.
  Mpaka hapo ujue hujaolewa na mwanaume ila umeolewa na MVULANA.sasa kama aleti chakula nyumbani,pamoja na matumizi mengine kuna taratibu za sheria za kufuata.ila kabla ya hapo unatakiwa uchunguze kwa makini kwann afanye hiyo?
  pia kabla sheria zungumzeni kama wanandoa halafu baadae kama itashinikana peleka hili jambo kwa wazazi/walezi wa ndoa yenu. kama ikishindika tumia sheria, Asante.

  ReplyDelete
 2. Mama,mimi ni mwanamume nimesikitika sana na habari yako,mimi kwa ushauri wangu,tulia ulee watoto wako,chochote unachopata wewe angalia watoto wako hiyo 10m itaisha na itapoisha akili ndio itamrudia na kukumbuka familia yake maana huko watamkimbia na kumnyooshea kidole,msubiri hapo ndio ita ndugu ama kama hapo juu alichosema,pole sana mama.Jagger

  ReplyDelete
 3. pole sana,huyo mume atarudi tu,kwani hao vimada wamempendea hela na sio yeye.siku zikimuishia atarudi nyimbani.ingawa ni ngumu na inakuuma,wewe endelea ku focus na biashara zako.bila shaka watoto wako ni wakubwa,huyo baba analeta mfano mbaya kwa watoto wake.mimi matatizo kwenda kuyaongelea na ndugu huwa naona tabu mno.kwa miaka ya ndoa yako,nina amini wote ni watu wazima,mnaweza mkayamaliza wenyewe

  ReplyDelete
 4. Pole sana mama tulia nyumbani na watoto wako atarudi tuu huyo ila cha msingi kwanza nenda kaw bos wake na pili nenda kwa rafiki yake umwekee ushahidi unajuwa ndugu zake itakuwa wamempa maneno ya uongo kwavile hawakukupa msaada wakati yeye akiwa ndani hivyo walikuona mwanake jasiri hukuwajali unajuwa ndugu ukiwa na shida hawana msaada ila sasa wamemwona jamaa ana chenji wamemshika masikio ukienda kazini kwake viongozi wake watamwita na watamwonya najuwa wazungu wana hekima na kama wewe ni mke wake wa ndoa kihalali ila kama kimyumba sidhani miaka 20 muwe hamjajulikana hata kwa padri hapana fuata ushauri wangu utafanikiwa na usiende kwa hasira pale kazini kwake jifanye mjinga mimi ni mwanaume sijapendelea alichofanya mwanaume mwenzangu.

  ReplyDelete