Tuesday, September 27, 2011

UNAAMBIWA KUA UYAONE YA DUNIA..

kuna mada moja niliyoandika kuhusu kituko cha yule shoga anayetembea na kujinadi kwa watu sasa jana nimepata mkanda mzima kwamba ni hivi..


kuna kaka mmoja tunafanya naye kazi na nirafiki yangu mkubwa, lakini kunawakati nilikuwa najiuliza mbona huyu kaka mara nyingi sana anapenda kutupa offer yani baada ya kazi tunaenda sehemu kukaa halafu mida ya saa tano ama sita ndio anarudi nyumbani kwake yani mara nyingi sana ndio ratiba yetu.


sasa jana tulivyotoka nikaamua kumuuliza kwanini inakuwa hivyo kwani hujaoa urudi kwa familia yako mapema? akaniambia hajaoa na nyumbani huwa hapendi kurudi mapema kwani panamkosesha raha kwa kero za baba mwenye nyumba yake, ebo!! nilishangaa sana maana nimezoea mama wenye nyumba ndio wanakero nilishangaa kusikia kwamba baba mwenye nyumba anamkera nikataka kujuwa kwa nini.


kwanza nikamuuliza kwani huyo baba hana familia akaniambia atapata wapi na yeye ni shoga!!!!
nini... sikuamini, akaanza kuniambia kwamba hapendi kuwahi kurudi kwa sababu yule kaka anamsumbua sana yani anamtaka kimapenzi, akishajuwa tu amerudi nyumbani lazima atakuja ajiongeleshe pale huku akimpapasa na kero nyengine kibao sasa hili jambo linamkera na kumkosesha amani.


akiwepo nyumbani wakati wa weekend yule kaka mashoga wenzake huja na kukaa kizingitini basi wanapiga story za kike za umbea kuhusu mabwana zao na kupeana style mpya za kumkamata mwanaume na utasikia wanacheka kiumbea mara taarabu haziishi yani mpaka unashindwa kukaa kwa amani.


akachoshwa na kuamua kufanya uchunguzi kwa majirani kuhusu yule kaka ndipo alipoambiwa kwamba hiyo nyumba kwanza yule kaka hapangishi mtu mwenye familia, mchumba ama mke na wapangaji wake huwa hawakai mda kwa vituko vya huyo kaka hata wao wanamshangaa yeye kukaa miezi hiyo miwili.


kwahiyo sasa ameamua kuhama ndio anatafuta nyumba sehemu nyengine kwahiyo mpaka apate atakuwa wa kukesha kwenye makumbi ya starehe ama ofisini mpaka huo usiku.


Reactions:

3 comments:

 1. hata huku singida kuna mama nyumba yake huwa anapangisha tu wanaume ambao hawajaoa halafu ukiamia anaanza kujipendekeza kwako ama anamuunganishia mtoto wake wa kike.

  ReplyDelete
 2. haki kwa wote kuwa chochote mtu atakacho, kwani hujasikia marekani mwanamke kajigeuza mwanaume na baadaye kubeba mimba na kuzaa? sasa unashangaa nini? ushoga ni dhambi tena tunatakiwa kuikemea lakini mtu akiamua utamzuia?

  ReplyDelete
 3. Habari za siku.
  Kama mwanablogu kutoka Tanzania,nakuomba kushiriki kuchangia Mchakato wa KUFUFUA JUMUWATA(Jumuiya ya Wanablogu Tanzania).

  Tafadhali naomba ufungue hii kurasa ya
  http://blogutanzania.blogspot.com/
  kisha upendekeze jinsi ya kufufua JUMUWATA.
  Ahsante
  Luiham Ringo.

  ReplyDelete