Monday, September 26, 2011

KISINGIZIO HIKI MMMHHH.....
katika kila nyumba mikwaruzano lazima iwepo, kutokuelewana lazima kuwepo na kuchukiana pia mara nyengine lazima kuwepo pia kwani mnapokutana kila mtu anatoka familia yake na malezi yake aliyopewa huku na mara zote malezi haya hayalingani hata kama mlikaa jirani toka udogoni mpaka mkaoana.


kwa upande mwengine maisha ya ndoa siku hizi ni kama mchezo wa kuigiza, yani tumeruhusu kuamini tamthilia za tv zetu, tumewaamini sana wa mexico maana hawa kwa mapenzi wanayoigiza mpaka mtu unajiuliza hivi huyu mwanaume/mwanamke alizaliwa ama alishushwa kwajinsi alivyojaa upendo kwa mwenza wake, lakini tukumbuke ile ni story tu sidhani kama maishani mwao kweli huwa wakamilifu kama tunavyowaona.


na hamna kitu kibaya katika ndoa kama kumfananisha mwenzio na mtu fulani, labda hupendi mwili wake ulivyo, ama ni mshamba ama anakoroma maneno kama haya ya kejeli huumiza sana na kubakiza kivu la uzuni sana katika moyo pale unapojuwa mtu unayempenda anakudharilisha hivyo hata kama mpo wawili tu peke yenu.


na kitu chengine watu wote wanaosaliti ndoa zao baada ya wenza wao kujua sijui ni kwanini lakini kila wanapoulizwa husema shetani tu ndiye aliyewaponza, na wanawake wengi huwa wanapenda sana kulipiza kisasi hapo nao ndio husikia "inamaana shetani huyo kakuona wewe tu, mimi hajaniona?" na wengi baada ya hapo nao utakuta wanatoka nje ya ndoa yao. nao husema shetani kawapitia.


lakini je tunaporuhusu shetani atuingilie kwenye ndoa yetu anayepata hasara ni nani??? maana mwanaume atapata raha pengine na mwanamke atapata amani pengine mwisho wa siku matokeo yake pindi mnapokutana kimwili hamna mwenye hamu na mwengine na mara nyingi wala hamtaruhusu ile hali ya kukutana kimwili itokee.. ndoa inakuwa ndoano


je tunapoamua kumkataa shetani na tamaa zake, na kumkubali MUNGU na maagizo yake ndoa zetu zitakuwaje, wewe mama utakapokubali kwamba MUNGU ndiye aliyenipa huyu mwanaume anayekoroma usiku mpaka nashindwa kulala, mwanume ambaye hanifikishi kileleni (na siku hizi kunastyle kibao unazoweza kumfundisha mwenzio mpaka akufikishe),mwanaume ambaye ni mlevi..........


na wewe mwanaume inakuwaje pale unapomuweka MUNGU na kukubali mwanamke aliyekupa labda mvivu, hajui kuvaa, anaroho ya uchoyo ama hajui mchezo vizuri (nawe ukamfundisha nini cha kufanya ile mfurahie) ukampenda jinsi alivyo hata kama kanenepa kwa sababu ya kuzaa watoto(angewatoa leo ungeitwa baba......)


yani tamaa zetu tu ndio zinatunyima baraka zaidi kutoka kwa MUNGU na tamaa hizi zinatupa hasara, uchungu na mwaumivu, Magonjwa ya zinaa na haziwapi watoto haki ya mapenzi ya wazazi.


ukiwa baba, mama, mume, mke, na wachumba wanaoingia kwenye ndoa tuache huu mpango wa kando na kusingizia shetani kukuponza, wewe ndio umejiponza mwenyewe kuingia kwenye mtego wa shetani. (hata vitabu vya dini viliandika kuna maisha mema na mabaya uamuzi ni wako utaishi maisha yapi).

Reactions:

3 comments:

 1. wanaume ndo vinara wa kumsingizia shetani pale wanapofumaniwa. si wanawake tunalipiza kisasi tu, tena ni waaminifu kwenye ndoa/mahusiano. Mama N.

  ReplyDelete
 2. teh teh teh, chezea mama mizizi umenifurahisha sana kwa hii mada, jamani tutakuja uana haswa ukiangalia siku hizi magonjwa kibao mwanamke akimsingizia shetani mwanaume naye akimsingizia shetani basi huyu shetani bala bala haswa ati.

  anna(mutoto wa mjini)

  ReplyDelete
 3. Mada ni nzuri sana, Nakupongeza kwani imezungumzia hali halisi ya maisha. Sasa hivi tusidanganyane eti mwanaume ndiye anayeanza kutoka nje. Ukweli ni kwamba wanawake walio na asilimia kubwa za uaminifu ndani ya ndoa ni wale walioolewa wakiwa mabikra au na mabwana waliowatoa bikra. Kwa hao walioolewa na watu ambao hawakuwatoa bikra wanakuwa na asilimia chache za uaminifu coz hatujui waliachana vipi na mpenzi/wapenzi wa zamani? Ikiwa waliachana pasina ugomvi wowote na walikuwa bado wanapendana., siku ya kukutana hawa watu wasipokuwa na hekima na busara na imani kwa Mungu, wanaweza wakaanza tena, eti wanakumbushia.
  Kubwa ninalotaka kusema ni kuwa, hakuna wa kulaumiwa hapa, wote wake kwa waume tunapaswa kuwa watiifu na waaminifu kwenye ndoa zetu. Tukumbuke ahadi kemkem tulizopean kabla ya ndoa. Tukumbuke pia viapo vyetu vya ndoa na tuyafanyie kazi yote. Ndoa yenye amani ya nje na mioyo ni ile ambayo wanandoa wanapendana, wanajaliana, ni waaminifu, wanavumiliana mapungufu yao na kuoneana huruma ktk kutendeana mabaya.
  NasriMada ni nzuri sana, Nakupongeza kwani imezungumzia hali halisi ya maisha. Sasa hivi tusidanganyane eti mwanaume ndiye anayeanza kutoka nje. Ukweli ni kwamba wanawake walio na asilimia kubwa za uaminifu ndani ya ndoa ni wale walioolewa wakiwa mabikra au na mabwana waliowatoa bikra. Kwa hao walioolewa na watu ambao hawakuwatoa bikra wanakuwa na asilimia chache za uaminifu coz hatujui waliachana vipi na mpenzi/wapenzi wa zamani? Ikiwa waliachana pasina ugomvi wowote na walikuwa bado wanapendana., siku ya kukutana hawa watu wasipokuwa na hekima na busara na imani kwa Mungu, wanaweza wakaanza tena, eti wanakumbushia.
  Kubwa ninalotaka kusema ni kuwa, hakuna wa kulaumiwa hapa, wote wake kwa waume tunapaswa kuwa watiifu na waaminifu kwenye ndoa zetu. Tukumbuke ahadi kemkem tulizopean kabla ya ndoa. Tukumbuke pia viapo vyetu vya ndoa na tuyafanyie kazi yote. Ndoa yenye amani ya nje na mioyo ni ile ambayo wanandoa wanapendana, wanajaliana, ni waaminifu, wanavumiliana mapungufu yao na kuoneana huruma ktk kutendeana mabaya.
  Nasri

  ReplyDelete