Wednesday, August 17, 2011

KUNITOA B.....R......A..... ISIWE ISHU...

Rose,


hivi wanaume saa ingine sijui wanafikiria sisi wanawake ni mchezo tu wa kuchezea.. mpaka nimeolewa nilikuwa bikra, na nilijikuta nipo hivyo kutokana na kulelewa kwenye familia ya dini kali hatukuruhusiwa kutoka na hata marafiki yani kwa ufupi tulikuwa tunafugwa sana hatukupewa muda wa kupumua hata hewa ya bahari.


mpaka naolewa mume wangu alinikuta mzima kabisa, na alifurahia sana kwakweli mwanzoni nilikuwa na enjoy sana ndoa yangu sasa tuna miaka miwili na ninahisi mume wangu sio mwaminifu maana ananifanyia vituko kibao, mara haendi tena mzunguko mrefu, siku nyengine uchovu unakuwa mwingi vitu tu vingi vya ajabu ambavyo mwanzoni havikuwepo nikimuuliza ananijibu tu hamna kitu na wakati mwengine anasema kwani wewe unahisi nafanya nini kwani umeshawahi kuwa na mwanaume zaidi yangu ukajua mwanaume anapobadilika?(mara nyingi sana husema hayo maneno)


sikutegemea kama hata siku moja ningefikiri kusaliti ndoa yangu lakini nahisi labda sasa ni wakati, maana anaona kwasababu sijawahi kuwa na mwanaume mwengine basi anauwezo wa kuchezea feelings zangu atakavyo (nimechoka kabisa)


yani wakati mwengine nawaza afadhali ningefanya lolote lile kabla sijaolewa hata kwa kutoroka kwetu ningepata bwana akanitoa bikra nisingeolewa nayo maana niliambia ni fahari kuolewa nayo lakini fahari hiyo kwangu imegekuka fimbo ya kunichapia.


ELIZA

Reactions:

4 comments:

 1. Mamie
  Hapo ujanja hakuna unahitaji umwombe Mungu akujalie hekima na busara ili maamuzi yoyote utakayoyachukua yawe na faida kwako wewe mwenyewe. Usifanye jambo ambalo unafikiri litamkomoa mwenzako kumbe laweza kukukomoa wewe. Wewe ni wa thamani sana kamwe usiruhusu mwanaume aharibu maisha yako kwani hajakuzaa na wala hajui uchungu wako. Tulia na mwisho wa siku utajua kitu cha busara cha kufanya chini ya msaada wa mungu. Mambo ya ndoa ni magumu kumpa mtu ushauri wa direct.

  ReplyDelete
 2. pole dada. sio mbaya ukipata mpenzi wa nje ila kumbuka kutumia kinga. kuna ukimwi. pia fanya kwa siri mumeo acjue. ndoa tamu japo ina matatizo

  ReplyDelete
 3. Mtoa maoni ya 2 km huna la kushauri utulie. Wewe mwanamke kwanza jifunze kumheshimu mumeo...nawe unapaswa kumwelewa mumeo kuwa huwa kuna kuchoka. Mimi ni mwanaume nimeoa miaka 4 iliyopita...kuna wakati nlikuwa naenda safari 1 tu hoi, miaka 2 iliyopita, ila tuligundua tatizo ni kuwa tulikuwa hatuongei vizuri na kusisimuana. Sasa nakushauri km ni wakristo mnunue vitabu vya namna ya kufanya tendo la ndoa. kuna kitabu kinaitwa "majibu ya ndoa yako" Cha Bruce & Caro...nunua hicho msome pamoja na mumeo. Kitawasaidia sana. Halafu ukiona mwenzio kafika haraka usimkatishe tamaa..mpe moyo ili ajione bado yumo. Sasa wewe ukilala pembeni ndo utamfanya mwenzio aumie moyoni na asikufikishe. Mimi nilikuwa hivyo sometimes...sasa hvi naenda hata 5 hadi wife wakati mwingine anaomba off time. Please don't do anything bad.

  ReplyDelete
 4. sijaona sababu ya wewe kujutia kuwa kwenye ndoa yako, kimsingi kama unaamini kuwa mmekulia kwenye maeneo yenye mazingira tofauti basi jua kwenye ndoa lazima mtakutana na mambo tofauti.
  sasa nakushauri suala hili si la kuchukulia jazba maana kama utakuwa na jazba inawezekana ikakufanya ujutie jambo au auamuzi uliouchukua.
  kwa nia ya kuwa na amani nakuomba kaa na mume wako, tafuta lugha nzuri ya kuongea nae juu ya jambo hilo hasa mkiwa faragha hapo utaweza kupata fursa ya kuweza kupatia ufumbuzi tatizo hilo.

  ReplyDelete