Tuesday, August 16, 2011

NILITAKA KUFANANA NAO SASA YAMENIKUTA...

Rosemary,


mimi ni msichana wa kitanzania naishi dubai, nilivyopata kazi hapa dubai nilikuja kama mtanzania lakini ukiniona sasa ni kama muarabu, nilivyofika hapa nilitamani sana kuwa mzuri kama hawa wasichana wa kiarabu wa hapa ndipo nilipopata marafiki na kuzoea dubai nikaanza kutafuta vya kunipa hiyo rangi niliyoitaka.


kwasababu sikutaka kuwa kama chui kubadilika rangi sehemu chache yani pengine kuwa mweupe na pengine kuwa mweusi nikaamua kuliko kutumia cream za kunifanya mweupe ni afadhali ninywe vidonge ambavyo vitanibadilisha mwili mzima.


kweli vile vidonge vilinipenda sana nikapendeza mno yani ikafika kipindi mpaka watu wakanishangaa na kunitamani, kwa kunisifia kwao vile wala sikufikiria matatizo ambayo yangenisababishia baadae nikaendelea kuvitumia mpaka nilipokuwa mweupe pee, nikaacha ila baada ya miezi fulani huvitumia tena.


nimekaa huku dubai miaka sita sasa mpaka nikapata mkaka wa kunioa, tumeoana sasa ni mwaka na ninajaribu kweli kubeba mimba lakini hazikai na nikibeba ikifika miezi sita tu inatoka, nimebeba tatu na zote zimetoka nikaenda kumuona daktari wa akina mama ndipo aliponiambia vile vidonge nilivyotumia vya kunibadilisha rangi ndio tatizo langu linalonifanya mimba zisikae.


kwakweli iliniuma na kunichanganya sana kusikia hayo maneno ya daktari, nikaambiwa niache kabisa kuvitumia ili ile sumu iishe kwenye damu, cha kunichanganya zaidi umri unaenda mpaka hiyo simu iishe nitaweza kweli kuzaa!!!!!!! najutia niliyoyafanya kabisa


leo nataka niwashauri tu wanawake wenzangu katika urembo tuwe makini sana na vitu tunavyovitumia maana vingi hadhara zake huziona baadae na mara nyingi huwa tumechelewa hatuna la kufanya tena.

xxxxxxxxxxx
Reactions:

3 comments:

  1. Pole aisee! Ukitaka uzuri sharti udhurike. Ukitaka usidhurike basi sharti uyakubali maumbile uliyoumbiwa na muumba.

    ReplyDelete
  2. pole dada. wanawake mlio na masikio msikie

    ReplyDelete