Thursday, August 18, 2011

HUYU MTOTO VIPI JAMA...
kwanza kabisa nataka nimshukuru MUNGU kwa kuumba mwanaume na mwanamke tokea mwanzo kwani ni kwasababu ya hawa mpaka leo mimi na wewe tupo humu duniani tukiifurahia dunia..


sasa kabla ya siye kuwepo walikuwepo wazazi wetu waliotuleta duniani, jamani kunawakina fulani kwasababu walizaliwa kijijini na kuja mjini na kufanikiwa sasa yupo juu anawasahau wazazi wake na wengine kuwakosea heshima kabisa.


pombe isiwe kisingizio cha kumkosea mzazi wako heshima, kuna jamaa mmoja amenisikitisha kweli jana huyu kaka nasikiaga huwa analewa sana na hachagui pombe chochote kinaenda ilimradi tu imleweshe na kumpa stimu.


huyu kaka yeye bado anakaa kwa wazazi wake, na hapo kwa wazazi wake kuna duka la bidhaa za nyumbani ambalo kwa mapenzi baba yake amempa huyu kijana aliuze ili naye ajipatie hela za kujikimu.


cha kushangaza huyu kaka akilewa yani mpaka majirani watu wazima wamesikitika na kuchoka anagawa pesa za dukani ukija tu kama anakujuwa anakukatia, ukichukua vitu dukani wala hakudai anakuruhusu tu uondoke na mbaya zaidi baba yake akiimuuliza kwa nini anafanya hivyo kinachouma wengi anadiriki kumpiga baba yake mzazi!!!!!!!!!!!!


kwakweli watu wanasikitika sana na hili jambo na sio mara ya kwanza ya pili ama ya tatu, na cha kushangaza baba yake baada ya hayo yote bado anampa mwanaye majukumu ya duka kama kawaida.. jamani


heshima kwa kila mtu haswa wazazi ni kitu cha muhimu na cha bure ya dunia yasitufanye tujisahau na kuacha kuwa na utu.


Reactions:

0 comments:

Post a Comment