Thursday, August 18, 2011

HILI NALO SASA......

Rose,yani ndoa hizi jamani kasheshe, yani mume wangu ananifanyia vituko vya ajabu ambavyo sielewi kwanza yani akitaka nikampe mzigo, sio kwamba ananiomba kimapenzi maana wote tunajuwa lile tendo linataka kuandaliwa yeye ananilazimisha kwa maneno ya ajabu kama wewe k.....a twende ukanipe hiyo k.....a yako!!!!!! kweli haya ni maneno ya kumwambia mtu unayempenda?


haya isitoshe sio hiyo tu kwakuwa mimi nafanya kazi kwenye kampuni binafsi utakuta wakati mwengine kama kazi bado nyingi ama kunakuwa kunakazi zinazonipaswa kuchelewa kutoka ofisini yani nikifika nyumbani tu inakuwa matatizo makubwa sana, maana mpaka naona aibu kuandika utakuta mume wangua kabla sijaenda kuoga huniambia nilale kitandani na kuanza kuninusa k.....a yangu aone kama inanukia m.....o yani yeye huisi ninavyochelewa kutoka basi nilazima nitakuwa kwa mwanaume tu.


yeye anamtindo wa kulewa na kutokurudi nyumbani hata siku tatu lakini mimi wala simwambii kitu ila miye ndio naonekana muhuni na kupewa manyanyaso mpaka ndoa naiona imegeuka kuwa shubiri.


nimfanyaje huyu mume wangu maana naona hata aibu kupeleka hili swala kwa wazazi wake ama wangu nitaanzaje kuwaeleza?


mama Ibra

Reactions:

2 comments:

  1. Pole dada. Jitahidi kusugua goti kumuomba Mungu wako. Hakuna lisilowezekana kwa Mungu.

    ReplyDelete