Tuesday, June 14, 2011

SHEMEJI ANIANDIKIA MESSAGE MUME WANGU AKASIRIKA...

jamani ndugu zangu hebu naombeni mawazo yenu, mume wangu ananuna kisa mdogo wake ameniandikia message ikisema, wanawake husifiwa wakiwa wajawazito wanapongezwa na kushikwa tumbo lakini kwa nini mwanaume hasifiwi kwa kushikwa uume??? mume wangu ameiona na kukasirika anadai ni lazima nitakuwa na uhusiano na mdogowake wakati hamna kitu kama hicho... mpaka leo haniamini nifanye nini na anashindwa kumuuliza mdogo wake ama anatafuta tu sababu ya kugombana na mimi?

Reactions:

3 comments:

 1. Inaonekana kama ni kisingizio tu cha kukununia. Au pia muite shemeji yako na pia yeye mume wako na muulize shemeji yako mbele yake na uone nini atajibu... kaaazi kwelikweli

  ReplyDelete
 2. Huo ndio wivu wa mapenzi, kaeni pamoja muongee...na kama inawezekna muhusiheni huyo shemeji...lakini mkikaa wawili kwa upendo mnaweza mkayamaliza

  ReplyDelete
 3. Sikia dada yangu. Kama una utani na huyo shemeji yako ni afadhali usihusishe maneno ya namna hiyo. Maana sisi wanaume tuliooa tunamuamini zaidi mama aliye tuzaa tu kuwa ndiye salama kubaki na mke wangu. Pia mweleze shemeji yako asiandike meseji za hivyo kwako na mwambie kuwa meseji zote za hivyo wewe humpa mumeo. Jambo hili litaisha. Pia bro namsihi apotezee jambo hilo kwa sasa kama utachukua hatua hizo. vinginevyo utaishia pabaya hata kama hukuwa na nia mbaya.
  Shemeji pia namshauri mambo ya namna hiyo amwandikie girlfriend wake na si wewe.

  ReplyDelete