Friday, June 24, 2011

NIMEONDOKA KWA MUME HOUSE GAL ANG'ANG'ANIA...

ndugu zangu hiki ni kisa nadhani cha kushangaza sana, mimi na mume wangu tumetokea kuwa na matatizo makubwa ambayo yamenisababisha kuondoka pamoja na mwanangu, siku ambayo nilikuwa naondoka nilimpeleka kwanza mtoto shule halafu nikaenda kazini baada ya kumaliza kazi jioni nikamchukua mwanangu nikiwa na kila kitu changu kwenye gari na kuelekea kwa wazazi wangu ambapo nipo mpaka leo..

cha kushangaza msichana wangu wa kazi ambaye nilimleta kunisaidia kazi za mtoto yeye amegoma kuondoka nami, yani amesema anabaki nyumbani kwangu wakati mimi boss wake nimeondoka pamoja na mtoto sasa huko kwa mume wabngu yupo yeye peke yake hamna mtoto mwengine huyu msichana anataka nini?????

nilijuwa labda ni utani baada ya muda atakuja lakini mpaka leo bado yupo na mume wangu wao tu wawili kwenye nyumba na sasa hata hanisikilizi mimi tena akidai boss wake ni mume wangu sasa boss ni mume wangu na sio mimi tena jamani mbona ananishangaza ama alikuwa anamtaka mume wangu?????

namshangaa kweli sijui hata nimfanyaje.

Reactions:

6 comments:

 1. achana naye mpuuzi huyo yeye anafikiri yeye ndio atayawezaa au ndio kaonwa ni mzuri saana aolewe naye?its just a matter of time ataondoka bila hata ya kuambiwa au ndio atafukuzwa kama mbwa...vitoto vya busk bwana vinadanywa vinakubali kitaondoka na maradhi au mimba sijui kwanini vinababaika na njemba za watu,halafu inawezekana pia alishaanza kuhusiana na mumeo muda mrefu bila ya wewe kufahamu.muache mpenzi dunia duara na ndiyo itakayomfunda

  ReplyDelete
 2. umekosea kuondoka na kumuacha hapo ndani, fanya uwezalo atoke kwa lazima, huyo anatembea na mumeo na ndo alofanya wewe utofautiane na mumeo.

  ReplyDelete
 3. Yaani mdau hata kama umeamua kuachana na mumeo for good huyo binti nenda kamtoe hata ikibidi kwa winch hiyo ni dharau ya hali ya juu. Fanya hima kamtoe haraka sana. Ebo! Yaani H/girl abaki na mume wangu dharau gani hiyo. Hao ndio wanakuja toka vijijini na mahirizi kuvuruga nyumba za watu.

  ReplyDelete
 4. kila kitu hufanyika na kusundi lake. mwashie Mungu afanye kulingana na uamuzi wake hukutakiwa kuondoka ulitakiwakuomba na kuamini Mungu ni mweza yote. yapo mambo km hayo lakini MUNGU ANA KUSUNDI LAKE. dadangu vumilia Mungu yupo atakuwezesha atakupa ushindi yeye ni mweza yote.

  Nitakuunga mkono kuomba , hiyo pepo ya usherati itoweke katika jina la Yesu.

  ReplyDelete
 5. Tufikiri kwa mapana ndugu zanguni. Je, huyo house girl ndiyo aliyemkosanisha huyo Mama na Mumewe? Kabla hajaamua kuondoka kwa mumewe palikuwa na dalili zozote za uhusiano baina ya house girl na huyo Baba? Inawezekana huyo mama ndiyo alikuwa chanzo cha matatizo na alipoamua kuondoka huyo mume akaona hakuna haja ya kutafuta mtu mwingine wa kumsaidia shughuli za nyumbani na hivyo akaamua kumwambia huyo house girl aendelee kuishi pale nyumbani kwa maana nzuri tu na siyo wafikirivyo wengi. Tusipende kuhukumu kabla ya kusikiliza pande zote zinazohusika. huyo mama ajichunguze kwanza!

  ReplyDelete
 6. Wewe umesusa mwenzio anakula, kinakuuma nini?

  ReplyDelete