Thursday, June 30, 2011

MUME WANGU HAPENDI KUTATUA MATATIZO YA NDOA YETU..


mimi na mume wangu tumeoana miaka kadhaa sasa mingi ya kujuana yapi mabaya yetu na yapi mazuri yetu, cha kushangaza ni kwamba pale matatizo huwa yanapotokea na haswa bila kumsingizia mume wangu mengi huyasababisha yeye ninapojitahidi kutaka kuongea naye kuhusu matatizo yetu hataki kunisikiliza akidai ya kwamba yeye anaona hamna tatizo lolote na anafurahia ndoa yake kama ilivyo, wakati kiukweli matatizo tunayomengi sana mpaka yanatuelemea..

licha ya yeye kukataa kunisikiliza pindi ninapotaka kuongea naye kuhusu matatizo yetu, basi namuambia tuchukue hata siku moja tuyaongelee tukiwa hatujalewa maana tukiwa tumelewa hatutaelewana lakini yeye hataki wala hanielewi yani maudhi yanazidi mpaka sasa kiukweli ananiboa ile mbaya hata kumtamani simtamani tena.

mimi bado msichana mdogo amenipita miaka mingi mno, bado nahitaji mapenzi ya mwanaume na attention lakini yeye hanipi, nimebembeleza lakini sieleweki..yani hanitimizii kabisa nimeamua kugeukia pombe kama mpenzi wangu mpya na huko ndipo nimekutana na kijana anayetaka kunichanganya akili kwa mapenzi na attention kibao ambazo nahitaji.. nahisi kuvutiwa japo najitahidi nisimsaliti mume wangu lakini hamna raha yeyote ninayopata nikiwa na mume wangu zaidi ya kero zake za pombe, na kuchelewa kurudi nyumbani kunitunza..

nahisi kuhamisha pendo..

Reactions:

2 comments:

  1. Hilo ni tatizo la kuolewa na mtu alokuzidi sana umri. Hataki kukusikiliza kwa kuwa anakuchukulia kama mtoto kwa hiyo huwezi kuwa na cha maana cha kumwambia. Ila mambo ya kutembea nje ya ndoa siungi mkono hata siku moja. Yamekushinda omba talaka yako kaanze upya, siyo kucheat

    ReplyDelete
  2. Ni kweli, kwenye relationship mkishaanza kukosa cha kuongea, basi tena ni hatari. Dada kama haiwezekani omba talaka ukaanze maisha upya. Si vizuri kucheat.

    ReplyDelete