Monday, June 6, 2011

MSIFIE MWENZA WAKO INALETA RAHA JAMANI...

hivi hii ni sana kwa wadada, hivi wewe huyo mpenzi wako uliye naye ameshawahi kukusifia yaani namaanisha kila kitu mwili wako, uzuri wako wa sura na wa kwa sita kwa sita, ama tembea yako au kitu chochote kile ulichokuwa nacho, je baada ya kusifiwa unajisikiaje ama kama yeye hajawahi kukusifia pia unajisikiaje?


jamani wenza hebu kuwa huru na mpenzi wako hebu msifie pale anapokuwa na kitu kizuri ama anavyofanya vizuri, utakuta kuna wababa wengine wala hawana mda wa kuwachunguza wanawake zao kama labda alivyovaa kapendeza wewe humsifu, labda kajipamba vizuri umuone wewe humsifu, mwili wake kauweka vizuri wewe humsifu macho tele barabarani ndio unajuwa kuwasifia ila yule mpenzi wako wala huoni unadhani kitakachotokea nini pale atakapotokea kijana kutwa kumwagia masifa mdada japo hata moja kila siku.....ATAHAMA


wanawake wengi tunapendwa kusifiwa wanaume na jamani kunawanaume wanajuwa kutega kwa misifa hehehehehehehe loh we acha tu, yani mpaka kishangazi cha mwilini jamaa anakiona na kukisifia na wakati mpenzi wako wa kila siku wala usikute hajawahi kukiona hii si aibu...


jamani mapenzi yanataka vitu vidogovidogo kama hivi kuyaweka imara hebu tujaribu kuwa makini kwenye hili, maana kama wa nje akianza kumsifia mpenzi wako zaidi yako inakuwaje ndio nguvu zote zinahamia kule ukija ndani unaonwa kama kituko..

Reactions:

1 comments:

  1. ni kweli wanaume wengi wakishaowa hawana muda wa kumuangalia mke wake wala nini sasa atajua umevaa nini hawezi kuona matokeo yake dada inataka moyo, utasifiwa na mtu mwingine yeye hana habari. kujirekebisha msifie mwenzako kunogesha mapenzi na nyumba yenu pia

    ReplyDelete