Friday, April 8, 2011

RAFIKI WA BABA YANGU ANITAKA KIMAPENZI....

Kuna baba mmoja ambaye ni rafiki mkubwa sana wa baba yangu tokea siku nyingi nimekuwa nikimuona huyo baba lakini hata siku moja sijawahi kumuona mke wake wala watoto wake, kumbe yule baba tabia yake ni kuwa tu na mwanamke kimapenzi halafu basi hakutaka kuoa wala kuwa na watoto..

Mpaka sasa nimeshakuwa msichana mkubwa bado namuona huyu baba kwa sasa atakuwa na miaka hamsini, nilipokuwa natafuta kazi huyu baba alihakikisha nimepata kazi anapofanya yeye shirika kubwa tu hapa nchini nilijuwa anafanya hivi kwasababu ya kumuheshimu baba yangu kumbe sikujuwa alikuwa anataka niwe karibu yake ili anipate kihurahisi..

kwa furaha niliyokuwa nayo kupata kazi nzuri wala sikufikiria kitu kama hicho mpaka aliponitamkia wazi baada ya miezi sita ya kuajiriwa, na chakushangaza anasema anataaka kunioa na anataka nimzalie mtoto, jamani yani baada ya kushangaa imeniudhi sana kwasababu huyu ni kama baba yangu nimekuwa nikimuona....

sasa maisha yangu hapa kazini yamekuwa magumu ukiangalia yeye anauboss basi amani hata sina nashindwa kumtukana nitakuwa namkosea heshima niliyoijenga kwa miaka 26, nikimwambia baba yangu urafiki wao wa muda mrefu wa shida na raha utakufa na baba yangu ataumia roho sana kujuwa anachofanya huyu rafiki yake...

nifanyaje?

Reactions:

4 comments:

 1. POLE SANA DADA INATAKIWA KUWA JASIRI MWELEZE UKWELI MWAMBIE YEYE UNAMWONA KAMA BABA YAKO MWAMBIE HILO HALITAWEZEKANA MWAMBIE HATA KAMA UKACHA HIYO KAZI UKARADHI KWANI RIZIKI NIPOPOTE ALAFU MWAMBIE AKIZIDI KUKUFUATA UTAMWELEZA BABA YAKO USIKUBALI KUUZA UTU WAKO KWA AJILI YA KULIPA FADHILA YAKUTAFUTIWA KAZI HUYO BABA ANAPEPO YA NGONO NDIO MAANA MPAKA LEO HANA MKE MIAKA YOTE HAJAMWONA WAKUMUOWA AJAKUOWE WEWE AMBAYE NIKAMA BINTI YAKE NAMBAYA ZAIDI NI RAFIKI WA BABA YAKO HUYO BABA ANALAANA

  ReplyDelete
 2. Kimbia mbio, kazi utapata kwingine. Huyo ana magonjwa tayari.

  ReplyDelete
 3. Nakushauri pia toka hapo kazini kazi zipo nyingi tu ndugu yangu. Huyo baba ni balaa kweli jamani kaazi kwelikweli!!!

  ReplyDelete
 4. Ndugu!!!!! nimeshangaa mm toka unakuwa anakuona leo anakutaka?? mwepuke kabisa anza kutafuta kazi sehemu nyingine kama elimu yako ndogo fikiria kurudi shule mdogo wangu.

  ReplyDelete