Wednesday, April 13, 2011

MAMA MWENYE NYUMBA YANGU ANAMTAKA MUME WANGU...


Jamani kweli nimeamini nyumba za kupanga zinamatatizo, hapa nilipopanga mama mwenye nyumba yangu ananiletea kasheshe mwenzangu kila kukicha ananipa vituko kibao mara nikipita ananifyonya, mara ananikagua nikipika (maana tunapikia nje majiko ya mkaa) mara mbona mboga imefanya hivi unatakiwa ufanye vile mara kwanini unapenda kupika chakula hiki kila mara yaani ananiingilia mpaka nilikuwa na shangaa nikawauliza wapangaji wenzetu wengine kama na wao huwa anawafatilia hivi lakini wala haikuwa hivyo....

Mara nikifanya usafi sehemu ambayo tunatumia kwa jumuia anapachafua mara nakumwaga maji kwa makusudi yani jamani vituko kibao, mara nikivaa nguo mpya anasema kimafumbo mara siku moja nikiwa chumbani navaa, nikijiandaa ili nitoke na mume wangu yeye mume wangu akatangulia kwenda nje yule mama alikuwa amekaa barazani ambacho kipo mbele ya dirisha langu ndipo nikamsikia mama mwenye nyumba akimuadithia shoga yake aliye kuwa amekaa naye nje kwamba "yani huyu kaka nimetokea kumpenda, yani nikimuona roho yangu inatakasika nitafanya lolote nimpate" sindipo nikaamua kuchungulia nje nione mwanaume gani nikashangaa kuona hakuna mwanaume yeyote aliyekuwepo nje zaidi ya mume wangu...

nilipatwa na butwaa na mpaka sasa nashindwa hata kuongea na yule mama vizuri nyumba naiona chungu natamani tuhame, sijamwambia mume wangu nataka kwanza ushauri nimshawishije tuhame kwasababu huyu mama kashadhamiria kufanya lolote mpaka ampate mume wangu...

Reactions:

5 comments:

 1. Mmmhh hapa inabidi utumie busara kwa kweli...je huwezi kumwambia mumeo ukweli?

  ReplyDelete
 2. tafuta mda mwafaka, kaa na mmeo,msimulie yale uliyoyasikia yakisemwa bila kubabaika,halafu msikilize mmeo atakachokushauri kwanza.

  ReplyDelete
 3. Dada ningekuwa mimi nasema ukweli tena haraka. Dunia imeharibika sana siku hizi. Mtajalogwa ndoa yenu iwe historia. Tafuteni nyumba mahali pengine. Nadhani hata kama mumeo ni muelewa ukimwambia muhame ataku support. Hawa wamama aged wakishika mmeo umekwisha shoga. Mtalogwa nyie fanya haraka muhame!

  ReplyDelete
 4. hee, mwambie mume wako ili ajilinde, kama hajui huyo mama anaweza kumpa mitego kama ya chakula etc na akaweka hata madawa mumeo akala ikawa tabu, mwambie mumeo halafu jiwekee confidence hasa kama una umri mdogo, yani jiweke kwenye hali hata katika maongezi na majirani kwamba mumeo unamdhibiti na we ujiweke katika hali ya kutoingilika kirahisi. Yani uwe mama flani hivi ataogopa huku unangoja kodi yako iishe uondoke. pia simama katika maombi kwa imani yako.

  ReplyDelete