Tuesday, April 19, 2011

NINAMTAFUTA KWA MUDA MREFU SIJAMPATA.....

katika maisha yangu nimeshawahi kuwa na wanawake wengi, lakini nakuwa nao tu ilimradi na mimi nionekane kwamba nina mwanamke nami nionekane ni mwanaume kati ya wanaume, na ninakuwa nao ili kumaliza shida zangu za mwili lakini hata siku moja sijapata msichana nimpendaye...

ninao kutana nao ndio wanamvuto na mvuto huo ndio unaonipeleka kwao kama sura, miguu, hips na bambataa, na chakushangaza mimi hupenda wanawake weupe, wembamba na mrefu lakini kila mwanamke ninayempata mimi ni mweusi na sio wembamba na wala sio warefu...muda unaenda sasa mpaka naona labda MUNGU hakunipangia kuwa na mwanamke kama huyo...

wazazi wangu wananimbia umri unaenda inabidi sasa nioe na niwe na watoto wangu wasife bila kuwaona wajukuu wao,lakini mwanamke ninayemtaka mimi sijampata nitaoa nani sitaki kuoa halafu nizeeke na mwanamke ambaye sijamfurahia labda tu nilipenda bambataa lake ama sura yake...

marafiki zangu wananiambia nikioa nitajifunza kumpenda mbele ya safari, na wengine wananiambia kosea kila kitu lakini sio mke kwasababu hilo ni agano la milele, naombeni ushauri wenu nioe tu ama niendelee kusubiri? labda nitampata

3 comments:

  1. Nenda kwenye internet uweke profile yako, watakutafuta!!!!!!!!11

    ReplyDelete
  2. Acha usanii, kama una vigezo vyako ambavyo umeweka kwa nini unatoka na wanawake ambao hawana sifa ambazo unaziitaji? Nyie ndio mnaowapotezea muda wasichana.

    ReplyDelete