Thursday, March 24, 2011

UJAUZITO WA MIEZI SABA NA SIO WA MUME WANGU.....


maisha yangu ya ndoa yalikuwa mazuri na matamu sana kipindi cha mwanzo, mapenzi yalikuwa tele na ya moto lakini ikafika kipindi mume wangu akabadilika akawa kituko akawa mlevi mapenzi hana yani tunaweza kukaa hata miezi mitano hatujakutana kimwili akija nyumbani siku nyengine anatafuta ugomvi tu ili tupigane, na mara nyengine hata haachi hela ya matumizi nyumbani...

kwa muda mrefu nikawa namvumilia nikidhani atabadilika lakini wala hata wazo alikuwa hana, siku moja nikiwa kwenye hotel moja na rafiki zangu akaja mkaka mmoja mtanashati na rafiki zake wakajumuika nasi, huyu mwanaume akatokea kunipenda na kwamatatizo niliyonayo sikuona mbaya kama ningekubali kupenda na kupendwa tena...

nikamuadithia kila kitu kuhusu ndoa yangu, na akaahidi kunipa mapenzi kama sijawahi kupewa penzi tena, kwakweli huyu kijana kama alikuwa ameshushwa kutoka Mbinguni alinipa mapenzi mpaka nikamuona mume wangu kama kaka yangu.....

miezi ikapita siku moja nikagundua yakwamba nimepitisha siku zangu za hedhi, kwenda kupima nikagundua ya kwamba ni mjamzito na kwasababu hatukutani kimwili na mume wangu nikajuwa moja kwa moja ni wa mpenzi wangu wa nje, kwakuwa sikuweza kumuacha mume wangu ikabidi siku hiyo nilivyorudi nyumbani nimtomase mume wangu mpaka akajikuta juu ya kifua changu, na ndipo ikawa mwanzo wa kulea ujauzito ule.....

baada ya wiki mbili nikamwambia mume wangu kwamba mimi ni mjamzito alifurahi sana kwasababu hatukuwa na mtoto basi kwake ilikuwa furaha kubwa, moyoni mwangu nikijuwa sio sahihi kutokumwambia baba halisi wa mtoto huyu kwamba nina ujauzito wake....

kwakweli baada ya kubeba mimba mume wangu akabadilika zile tabia zake mbaya zote zikafutika akawa na mapenzi tele, yani wakati ukafika mpaka nikawa nashindwa kwenda kuonana na mpenzi wangu wa nje, nikaachana naye bila kujuwa nilikuwa nimebeba mtoto wake...

sasa mimba ina miezi saba, mume wangu anajisifu kila mara kwa ndugu na rafiki zake anatarajia mtoto, moyoni roho inanisuta sijamtendea baba wa mtoto huyu haki lakini nitakapousema ukweli mume wangu ataumia sana na sitaeleweka na jamii pamoja na ndugu zake.....

najuwa sijafanya mema itafanyaje sasa ama niseme tu ukweli?

Reactions:

37 comments:

 1. Mimi ni mwanaume. Kwa mazingira yaliyokufanya mpaka uchukue kazi za nje, siwezi kukulaumu maana ulikuwa unairidhisha nafsi yako japo haikuwa suruhu ya matatizo yako. Kosa ulilofanya ni kufanya mapenzi bila kondomu. Wakati mwingine kwa hili vilevile siwezi kukulaumu maana mwanaume ndiye mwamuzi wa iwapo kondomu itumike au la na hili linatokana na jinsi mwanamke alivyoumbwa. Na ndio maana katika ndoa (japo sitetei wanaume kutoka nje ya ndoa) ni bora mwanaume atoke nje kuliko mwanamke. Maana wao ni waamuzi wa kujilinda na haya.
  Kwa kuwa hukuwa na maamuzi ya kutumia ama kutotumia kondomu umepata mimba na hatujui kuhusu magonjwa mengine.
  Kutoka kwako nje hakujakusaidia ila kumeleta matatizo zaidi. POLE

  Nina kesi ya jirani yangu ambaye mtoto wake wa kwanza kati ya watoto watatu hakuwa wa mume wake. Mume amekuja kugundua baada ya miaka kama kumi. Ni vurugu tupu ndani hakukaliki.

  USHAURI
  TRUTH WILL MAKE YOU FREE (Ukweli utakufanya uwe huru)
  Ni ngumu sana, ila mweleze ukweli kwa kutumia wajumbe watu wazima anaowaheshimu huku na wewe ukijiandaa kuachika, maana kusema ukweli wanaume hatuna uwezo wa kuvumilia hilo
  Huwezi kutoa mimba maana tayari anaijua, na zaidi katika hilo sikushauri japo dhambi ninazo, hiyo ni ni kuua.
  Jua kuwa wapo wengi wenye matatizo kama hayo, si wewe peke yako.
  Hata ukificha ipo siku tu atajua, ukizingatia ndiye mtoto wenu wa kwanza, ndugu zake lazima wajae kumwona na ndiyo wakute si damu yao patachimbika.
  La mwisho upo uwezekano huyo mwanaume hana uwezo wa kumrutubisha mwanamke

  ReplyDelete
 2. wewe kwanza nikupo pole kwa yaliyokukuta kwani mwanadamu hujafa hujaumbika mimi ninachokushauri usijekutoa hiyo siri kwa mume wako yakuwa mimba uliyokuwa nayo sio yake usjaribu pls kwani maji yameshamwagika yazoeleki tena na tena kitanda hakizaii haramu na huyo aliyekupa ujauzito usimwabie ya kwamba mimba ni yake kwasababu anaweza kukudai mtotowake ikawa tabu kwako wewe zidisha mapenzi tu kwa mume wako aendelee kuwelewa yakuwa mimba ni yake na hii iwe siri yako usimwambie mtu mwingine kwani binadamu hana siri endelea kumwomba mungu akusaidie kwa kipindi hiki kigumu kwako na majaribu

  ReplyDelete
 3. Duh kweli UKIMWI HAUWEZI KUISHA YAANI MTU ANATOKA NJE YA NDOA NA ANAACHIA MZIGO PEKU PEKU?? NADHANI TANZANIA BILA UKIMWI INAWEZEKANA TU KAMA WANAWAKE WATA ELIMISHWA VYA KUTOSHA KUHUSU MAGONJWA SIO TU MTU ANA WASIWASI NA MIMBA TU UKIMWI JE?? MIMBA UTATOA NA UKIMWI??? AU NDIO UTAKIMBILIA LOLIONDO??

  KWAKWELI IWE FUNZO HATA KWA WANAWAKE WENGINE KAMA UNATATIZO NA MUME WAKO KWANINI MSIONGEE KULIKO KUTAFUTA WA NJE?? KWANI NI WAZI KUTOKA NJE YA NDOA SIO SULUHU ZAIDI YA KUJITAFUTIA MAGONJWA!! MIMI KAMA MWANAUME NIKIJUA HIO KITU NAKULIMA TALAKA UKAOLEWE MBELE HUFAI HATA BURE.NIMEONGEA KAMA MSHAURI (MWANAUME) NINAYE CHUKIA KUTOKA NJE YA NDOA KWASABABU ZISIZO MBELE WALA NYUMA.

  SOMETIMES MNALAUMU WANAUME BURE ETI KAKUCHUNIA KUMBE MWENYEWE UMEJISAHAU UKO MCHAFU HATA HUMVUTII TENA AU UNATOA MAPENZI NUSU NUSU.HII IWE FUNZO KWA WANANDOA WOTE MTU KAMA UMEOA/MMEOANA LAZIMA MJUE KUTIMIZIANA HAJA ZENU NI LAZIMA UNLESS MMOJA WENU ANA TATIZO LA MSINGI KAMA KUUMWA NA MENGINE.KILA MTU ANA HISIA KAMA WEWE UNATOKA NJE NA YEYE ATATOKA COZ NAYEYE ANA HISIA KAMA WEWE.NA USIKUTE ALIKUA ANATOKA NJE AKIDHANI HUZAI KUMBE PENGINE TATIZO NI LAKE, ONA SASA ULIVYO NA MIMBA MAPENZI YAMERUDI.HII MADA IMENIBOA KAMA KUNA ALIYE UZIKA ANISAMEHE TU BURE MIE NACHUKIA SANA CHEATING KTK MAHUSIANO

  ReplyDelete
 4. we ungejua mi nilivofurahi, wanaume mmezidi kutufanya sie tuna moyo wa chuma na nyie wanyama basi shughuli ndo hiyo dada lea mwanao angali tumboni na akija duniani kitanda hakizai haramu mwaya!

  ReplyDelete
 5. Dada ulilofanya si la maana kubeba hiyo mimba ungejitahidi sana kama umeamua kutoka nje kutumia kinga kwa hali yoyote ile. Ila wanaume wana maudhi nao lakini kilichotakiwa hapo ilikuwa ni uvumilifu, busara, hekima na kumtafutia mahala ukaongea nae kujua tatizo ni nini si kwenda kinyume kama ulivyofanya. Hukumtendea haki Mungu wako na mume wako pia. Nashauri hiyo mimba usiitoe wewe zaa tu mengine yatafuata kila kitu kina mwanzo na mwisho wake. Acha tamaa ya haraka haraka. ujue kuwa "haraka haraka haina baraka kamwe"

  ReplyDelete
 6. I'm afraid to say that, NO WOMAN I WL TRUST IN THS WORLD EXCEPT MY MOM! I hate cheating and i cant cheat

  ReplyDelete
  Replies
  1. how sure areyou,kwamba na wewe ulizaliwa ndani ya ndoa? kitanda hakizai haramu.

   Delete
 7. wewe dada inaonyesha uliikuwa mkorofi kwenye ndoa. nasema hivi kwa sababu mwanzoni umesema hivi

  "tunaweza kukaa hata miezi mitano hatujakutana kimwili"

  Baada ya kupata mimba ukfanya hivi

  "kwakuwa sikuweza kumuacha mume wangu ikabidi siku hiyo nilivyorudi nyumbani nimtomase mume wangu mpaka akajikuta juu ya kifua changu..."

  kwa kuzingatia maneno yako mwenyewe ni kuwa inawezekana ulikuwa unamnyima. ingekuwa yeye anakunyima, siku ulipomtomasa asingeitikia. ulishindwa nini kuongea naye?

  nawaaasi wanabloggers wenzetu walio katika relationship na ndoa. tujitahidi kumtimizia mwenzenu raha za kimwili na inapotokea tatizo ongea. kutoka nje si suruhisho.

  aidha, kama utaamua kutoka nje please please please tumia condom, narudia tumia condom!!!

  ReplyDelete
 8. ficha ukweli ili kulinda ndoa yako. siri baki nayo rohoni. kumbuka kitanda hakizai haramu

  ReplyDelete
 9. siri pekee ndio itakayokunusuru, usimwambie mumeo wala huyo mwenye mimba maana utakuwa mgeni wa nani kama mumeo akikutimua? hautapokelewa kwenu wala kwa wakwe. POLE SANA SANA SANA SANA

  ReplyDelete
 10. huyu mwanamke ni mjinga tena ni mjinga hasa wewe, si ungeondoka kabisa kuliko kufanya hivyo? kosa sio kutoka nje, kosa ni kurudi ndani mjinga kweli wewe kumbe ndo maana kila siku utasikia wanawake wanapigwa hadi kufa.. sasa unafikiri akijua kama ana panga atakuacha? nani anataka hiyo fedheha, we unatakiwa UACHIKE TUU, tena unasema mlikutana hotelini tena mara kibao angekufumania ungekuta umeshatangazwa kwenye matangazo ya vifo mjinga mkubwa wewe labda nisikujue, ole wako, mi sikushauri lolote mjinga mkubwa, wanawake wengine ni kama mashetani unaweza kazaa paka hivi hivi unacheza na watu wewe unamdanganya mume wako hivyo... toka hapa.

  ReplyDelete
  Replies
  1. wewe NDO MJINGA TENA HUNA HEKIMA. unamtukana ya nini UNAMJAJI KAMA NANI??/ wewe huna makosa??? nani ambaye hakose?? jifunze kuutumia huo mdomo vizuri kwa kutia watu moyo na si matusi wala kukatisha tamaa kama uwezi kaa kimya. loo wa ajabu sana wewe mtu. ungekua mungu ungeua watu. Mwache mungu amhukumu uyu dada na sio wewe.

   Delete
  2. Kweli kabisa! Hakuna mtu mwenye mamlaka ya kumuhukumu huyu mwanamke, ni Mungu pekeyake. Hayo matusi yako yanaonyesha jinsi gani ulivyo wewe-mkatili.Huyu mwanamke anajua amekosa, anaomba ushauri sio matusi yako.

   Delete
 11. Hapana!! Sidhani kama kumtukana huyu dada ndio suluhisho,tena unathubutu kusema"SIKUSHAURI LOLOTE MJINGA MKUBWA'' duh ungekuwa MUNGU wewe duniani kungebaki mazingira tu!maana hata wanyama waharibifu ni wengi MUNGU angetufutilia mbali!
  Ni hivi dada yangu,maadam umetambua hilo ni kosa basi Neema ya MUNGU ipo juu yako,na kwa kosa ulilofanya ninahisi kilio chako sio mimba tu! Hakika hata ukimwi unao!mwanaume wa kukuona ghafla kakupenda!? ukamuachia mwili wako auchezee utakavyo,mmmmh wangapi anawaona kila siku eti ukajiamini umefika mahali sahihi?
  USHAURI wangu,Fanya toba mbele za MUNGU ahidi kutokurudia tena!ukipata amani moyoni basi mpende mumeo na usimwambia chochote. Nenda kapime ukimwi na mumeo ijulikane huenda ukawa umeathirika na mumeo ni mzima hapo ndipo pakuweka wazi uovu wako na ujiandae kuachika ama huna ukimwi hiyo ni salama yako maana utakuwa umeomba Toba ya kweli kwa MUNGU(zab.65:2-3) maana utakuwa umemuepusha mtu asiyekuwa na hatiya,maana inaonyesha wazi mumeo alitaka mtoto na kukosa kwake ndo kukampa mawazo mpaka akawa mlevi,kweli pole kwa kuwa hukutumia hekima kuinusuru ndoa yako.MWANAMKE MPUMBAVU HUIBOMOA NYUMBA KWA MIKONO YAKE,neno la MUNGU ni kweli na uhakika.Zingatia hayo

  ReplyDelete
 12. Pole sana kwa yaliyokukuta .wanaume ndio walivyo , alihisi wewe una tatizo na ndio maana aliamua kuwa mlevi na kuendelea na mambo yake maengine.huenda ya kutatafuta watoto .Kilichotakiwa ni kuwa mvumilivu tu .kutoka ndio ya ndoa yako sio suluhisho ,Umemkosea mumeo na kumuaibisha pia .Umemkosea Mungu pia. Ushauri we fikiria sasa namna ya kuishi maisha .haijalishi maisha yatakuwa magumu kwako kiasi gani .cha msingin uwe na amani.Andaa makao yako mapya uondoke hapo kwa mumeo .tafuta tu namna ya kumjulisha kwamba mtoto aliyebeba sio wako.ila usimwambie ana kwa ana.maana nauhakika ukijifungua ukambambikia mtoto amabaye sio wake itakukosesha amani maisha yako yote .na yeye and ndugu wakishtukia ndio soo zaidi.Muombe Mungu akusamemhe uendelee na maisha yako tu .baada unaweza kutafuta namna ya kumjulisha baba wa mtoto. Sidhani kama ni sahihi kuendelea kuishi na mume wako ukiwa na mimba ya mwanaume mwingine

  ReplyDelete
 13. Dada kwa kweli unatuweka mashakani sisi wanaume ambao hatujaoa, sasa kwa nini usingeongea vizuri na mme wako? alafu samahani kama nitakuwa nimewakwaza wanawake. kusema kweli mimi ni mwanaume na nimetembea na wanawake zaidi ya kumi na tano mpaka sasa, ni mooja tu ndo alinilazimisha nitumie kondom nae nadhani baada ya siku mbili tatu angeniachia peku peku, mimi toka nibarehe sijawahi kutiana peku, sasa huwa nawatania kama nataka kuingiza peku na wao wanaachia tu, hawakuulizi kondom ziko wapi? yaani huwa nashindwa kuelewa kama akili iko sawa sawa, tena wengine ni wanachuo na uelewa wanao, tena kuna mwanachuo mmoja akaniambia inamaana bado huniamini mpk tutumie kondom mpka leo? Sasa wewe dada kama ungetumia kondo yasingekukuta haya, kusema kweli wanawake mnakeraaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa, jitambueni sio mnapelekwa kama mazoba tu! wewe dada maji yameshamwagika wenzako wamepata somo sidhani kama watarudia ujinga kama wako, wewe subiri mpaka ujifungue ndo umwambie mme wako baada ya muda flan, ukimwambi sasa imekula kwako. Ni hayo tu.
  Ni mimi Izoo

  ReplyDelete
 14. Balaa kweli kweli haya usaliti mkubwa umefanya dada yangu au aunt yangu.

  ReplyDelete
 15. pole sista nafikiri upweke na kutokuongea kati yenu kumaliza mzizi wa matatizo yaliyowakabili kumepelekea yote hayo. Wote mna makosa hakuna aliyetaka kusimama katika nafasi yake kuinusuru ndoa yenu ndio maana yamefikia hayo. Sikulaumu sana kwani hayo ni mapito tu lea mtoto huyo na mumeo pia tafuta ushauri kwa wataalamu wa saikolojia pia watumishi wa MUNGU watakusaidia sana. Pia tubu hiyo dhambi isije ikakuumiza.

  ReplyDelete
 16. WAPUMBAVU KAMA HAWA WAKO WENGI SANA, NAWACHUKIA SANA WANAWAKE WA AINA HII....

  ReplyDelete
 17. koma weee hata wanaume mbona wanazaa nje kwani wao hiyo haki kawapa nani mxxxxxx

  ReplyDelete
 18. Dada nakushauri ondoka bila kuaga kaanze maisha yako kimya kimya na Mungu wako atakusaidia , ukishahama mjulishe mumeo kuwa umekimbia kwa kuwa una mimba ambayo si yake hapo unaweza sasa kumtafuta yule aliyekupa hali hiyo kama atakuelewa vinginevyo hapo kwa mumeo subiri uje unyongwe

  ReplyDelete
 19. wewe mwanamke wewe unawezaji toka nnje ya ndoa na kufanya mapenzi bila zana? kiukweli hapo umelikorogaaaa kabisaaaaaa yani hakuna msada na huyo mumeo unafikiri atakaa hadi lini bila kujua kama sio mtoto wake?POLE SANA

  ReplyDelete
 20. WANAWAKE NDIO WALIVYOO WANADANGANYIKA KIRAHISI SANA PLS ENYI WANAWAKE KUWENI WAVUMILIVU KATIKA NDOA ZENU KWA TABIA HIO HATUTAFIKA DADA MWOMBE MSAMAHA MMEO

  ReplyDelete
 21. pole sana dada yangu. hayo mambo yanatokea sana

  ReplyDelete
 22. Mie nimwanaume lakini ni vema ukausema ukweli japo utakubidi uondoke hapo home kwenu. kwani kwa kwakumficha huyo mmeo ni hatari sana atajua tu kama unamwamini Mungu basi tegemea kupata mtoto ambaye atafanana kweli kweli na baba yake mzazi. Hapo umechemka. Ubaya wote wa mumeo utaubeba wewe kwa asilimia zote. pole sana.

  ReplyDelete
 23. Pole sana dada tunza siri yako usimwambie yeyote yule, hayo ni ya kawaida katika dunia hii.

  ReplyDelete
 24. nimeipenda hiyo kosa la kutoka nje ya ndoa ni kwa mwanamke tu ila mwanaume akitoka yeye ni rijali safi sana mbona sisi kina mama mnatuacha ndani mnaenda kuzaa nje ya ndoa na sisi tunavumilia na mtalea watoto haramu mpaka mbadilike siku zote siri ya mtoto ni wa nani anajua mama

  ReplyDelete
 25. Upuuzi mtu huo, huyu demu alipaswqa kujiheshimu licha ya kutoka nje ya ndoa. Kwani angetumia kondomu raha asingepata? Kuna utafiti fulani wa Mpango wa Kudhibiti Ukimwi Tanzania unaoonyesha kuwa wanadoa hawapendi kutumia kondomu hata pale wanapokuwa nje ya ndoa zao. Ni funzo, tujifunze!

  ReplyDelete
 26. wewe sio mjinga shosti kwa yeye alitumwa abadilike tabia bila kukueleza shida ninini sasa dia we chuna zaa mwanao liache lijue mwanae kwani siri ya baba wa mtoto anaijua mama wala usikonde

  ReplyDelete
 27. maisha ni karata tatu jamani!sababu ya kumtukana mdada huyo hata siioni,ninani aliyemsafi chini ya jua?haijalishi mwanaume ama mwanamke kila mtu anamchango kwa matatizo ndani ya ndoa,hilo tukubali tusikubali,sikuzote wanawake/wanaume ni wakandarasi wa matatizo yetu wenyewe na kwa namna fulani yakituzidi hutafuta usaidizi au tukiwezakuyakabili juu kwa juu tuu,wanawake huweza sana kuvumilia na kuitafuta suluhu,ila kwa wenzetu wanaume suluhisho lao kwao ni moja tu ni kuescape na kujitoa kabisa,na daima wao huwa hawakosei na wapo sahihi sikuzote za maisha yao hata kama ni kitu kisicho na manufaa kwao ama hata kwa familia hiyo,baada ya madhara baadaye hukumbuka!
  Nadiriki kusema haya sababu na mimi ni mwanadnoa na mshauri wa mambo ya ndoa pia,na nimekutana na mikasa kadhaa pia,
  Ninachoweza sema kwa huyo dada,atulie mpaka ajifungue na alee kiumbe chake na mpenzi mumewe,kwani kila jambo linawakati wake,nilazima siku itafika na kila kitu kitakuwa wazi na hapo hatatumia jasho,mtoto atakuwa na nuru itapevuka na ukweli utadhihirika na mumewe atatambua na kila mtu atafunguka,kwani yote haya tunasema tu,je kati yetu nani anaujua ukweli?kama anatudanganya na hii stori aliyotueleza tunajuaje?UKWELI HALISI ANAO YEYE NA MUMEWE!!!!!.....Siye wengine tunashauri tu kwa kile tlichokisoma,lakini pia ni somo kubwa sana kwetu wanandoa.
  Napita tuu.....
  ma immu

  ReplyDelete
 28. heee dada hongera kwa ujasiri, lakini kwa salama ya ndoa yako na furaha bibi, nyamaza kimya muombe mungu akupe nguvu na akusamehe kwa dhambi hiyo, mana wanaume hawa unaweza mwambia akakuua kabisa, kwa mwanamke ni rahisi kulipokea mumewe akizaa nje, ila yeye si rahisi kukubali wwe kuzaa nje ni kama umemtukana, na baba mtoto ukimwambia nae anaweza kuja mtaka mwanae hivvyo jikaushe, hiyo sura ya mtoto huko huko mbele ya safari ukiulizwa wasema mie sijui labda kama ulibadilishiwa hospitali, ila jitahidi na mumeo na uzae nae pia, yawezekana kipindi anakukasirikia, labda nduguze walimwambia huzai akawa anakufanyia vitimbwi, akijua si yake na nyumba utahama.

  ReplyDelete
 29. nimecheeeeeeeeka maana hawa wanamme bwana wao ukimnyima cku moja tu balozi atajua ka umemnyima sasa anakunyima miezi mitano anakojoa wapi hebu nami nitafute wakunikojoza akomeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee lea mwanao mtoto huwaga ni wa mama @

  ReplyDelete
 30. mdada pole kwa yaliyo kukuta mpenzi ivi hyo mpumbavu anayemtukana huyu binti akili zake zinamtosha ama ni punguani.....wanaume wengi ndio wanaosababisha hali kama hizi zitokee ndani ya nyumba muombe mungu wako akusamehe hyo dhambi ila tunza siri yakko mpenz.

  ReplyDelete
 31. Kwanza kimeshatokea na c wakati wa kumlaumu ila binadamu hujifunza kutokana na makosa, na c vyema kutumia lugha za matusi coz katika damu na nyama hakuna mkamilifu hata iweje bible inasema damu na nyama haviwezi kuurithi ufalme wa mungu unafikiri kwanini? kwa maana twajua ya kuwa Torati asili yake ya rohoni, bali mimi ni mtu wa mwilini, nimeuzwa chini ya dhambi. Maana cjui nilifanyalo, kwa sababu lile nilipendalo silitendi, bali lile nilichukialo ndio ninalolitenda. lakini kama nikilitenda lilo nisilolipenda, naikiri ile sheria ya kuwa ni njema. Basi si mimi nafsi yangu ninayetenda hilo, bali ni ile dhambi ikaayo ndani yangu. (Rum. 7:14-17) muombe mungu sana akuepusha kuyafanya ambayo baadae unayajutia twapaswa kumuombea sana amevifanya kwa ujinga wake na kila mtu hapa tukianza kujichambua wenyewe kwa wenyewe tutajikuta sisi ni wa kosaji zaidi yake na ndio maana yesu krito alikufa kwa ajili ya wenye dhambi hilo twapaswa kulitambua na kumbuka bible inatuasa amchukiaye ndg yake ni muuaji mammy nimepewa mamlaka ya kukusamehe dhambi zako zote na kuanzia sasa uko huru hati yako ya mashtaka nimeifuta kwa neema mammy usiogope mungu alijua hilo. amani ya kristo itawale ndani yako nikiomba na kuamini katika jina la yesu AMEN.

  ReplyDelete
 32. dada yangu nakupa pole ila mimi sikulaumu hata kidogo kwani jamani wanaume wengi wanatutesa nakuchangia sisi kufanya hivyo mimi mume wangu ni zaid ya wako hajali nyumbani ni pombe wanawake ninao wajua ni zaid ya 3 tuna mtoto mmoja ni mkorofi hutafuta ugomvi ka wako akija akupige kwa kweli ni hali inayokatisha tamaa sana jamani,mimi hulia zaidi ya mvua inyeshayo na kuna wakati nilikua na mimba ya first born ndo alikua hajali kabisa sina mahusiano yoyote nje ya ndoa,zaidi kwa ajili ya kuumizwa moyo hua hata sikumoja sijawai kumtamkia nataka tufanye mapenzi nae mimi hua simkatalii akitaka nampa hata mara3 kwa siku akitaka mi nampa ila mimi sijawai kumwambia namhitaji hua namuacha akitaka yeye kwa sababu ya mambo anayonifanyia yanauma sana jamani ungepata watu wanao mjua Mungu kikweli wangekupa moyo wal usingeona haja ya kutoka nje ya ndoa zaid hua namuombea sna abadilike kwani wanaonaga kututesa na kunyanyasa wanawake ndo maisha kisha baada ya kusolve matatizo ya ndani na kuishi kwa amani na mke wako wanaume hukimbilia kwa vimada maisha hayo hua yanamwisho na starehe ya mdhambi ni ya muda mfupi namuombaga Mungu anipe uvumilivu tuu baada ya kujifungua mtoto hali ilikua hivyohivyo sasa mtoto anamiaka miwili ndo kidogo anaweza kununua hata pampas ya mwanae na mtoto ni copy right na yeye aibu akitaka kutoka nae mtoto hana nguo nzuri ndo huenda kumnunulia nguo ni mume mweny mshahara wa zaid ya 3mil mimi alinioa nilipomaliza chuo nikahama dar kumfata yeye si kua na kazi kwakweli niliona cha moto hayo mateso umenikumbusha mbali sna ila nilimuachia Mungu mpk sasa,nasikia amezaa nje ila yeye anabisha bisha kwa kweli wanaume wanatuumiza sana wanatupenda tukiwa tumependeza ila wakituoa kutuhudumia hakuna,pole dada ulikosa nguvu ukatetereka na kujisahau nje si kulaumu hata maana nayajua maumivu yako,kua tayari kwa lolote ila sasa kwa hali yako tulia lea mwanao kaa kimya pia anza kumuomba Mungu sana amini kunafaraja sna ukimtegemea Mungu,mlilie Mungu ni suluhisho la matatizo yote.wanaume hawajuai wanajipandia laana tupu na malipo ni hapa hapa duniani mimi mume wangu mambo yake sasa Mungu anamlipa ungekua mvumilivu ungeona jinsi Mungu anavyowalipa zaid ya manyanyaso uliyoyapitia sasa jifunze kuomba sna na kumtegemea Mungu tubu na Zaburi 51 kama ni mkristo,badilika anza upya moyoni mwako Mungu atakusamehe mengine yoote mkabithi Mungu atakutatulia tuu maaana hakuna mkamilifu hata mumeo alikukosea pia.

  ReplyDelete
 33. Haya mambo bwana we yasikie tu, nipo kwenye ndoa mwaka wa 6 sasa, ni mara moja tu mke wangu aliwahi kuniambia anataka tufanye mapenzi, kwa kipindi chote hicho ni mimi ndio naomba kufanya, inafika wakati unachukia maana hili ni swala la pande mbili isiwe kama una mburuza,

  ReplyDelete
 34. kaka hapo juu nakupa pole yaani kwa mtindo huo nakupa pole, humkolezi nn?yaani miaka sita kaomba mara 1 mkifanikiwa kuwa na miaka 50 ya ndoa atakuwa kaomba mara 8 heeeeeeeeee hiyo noma

  ReplyDelete