Wednesday, March 30, 2011

PACHA WA MKE WANGU KAGEUKA KUWA MKE WANGU....


mimi na mke wangu tumeona ni miaka sita sasa lakini hatujabahatika kupata watoto, tumesubri sana nakutumia kila dawa tuliyoambiwa inaweza kutusaidia kupata mtoto lakini yote yamekuwa bila mafanikio...


baada ya mawazo mengi na hasira kunasiku nikajikuta nimeongea neno baya kwa mke wangu lakumfanya aondoke kwenda nyumbani kwao,kule nyumbani kwao pacha wake alikuwa mjamzito, na mama yake alikasirishwa sana na kitendo cha yeye kubeba mimba akiwa nyumbani....


baada ya mke wangu kurudi nyumbani kwasababu ya kutonipa mtoto, mama mkwe wangu akawa amekasirika sana ikabidi yeye na watoto wake wapange mchezo kuokoa ndoa ya mtoto wake...


ndipo ikabidi kikao kiwekwe cha kuniita mimi na wazee wangu kuomba msamaha, na mke wangu akarudi nyumbani(bila kujuwa yakwamba yule sio mke wangu bali shemeji yangu).. kumbe yule shemeji yangu alikuwa mjamzito wa wiki tatu, baada ya mwezi kukaa naye siku moja akaniambia hajisikii vizuri akitaka nimpeleke hospitali tulipofika ndipo tukagundua yakwamba alikuwa mjamzito...


kwakweli hata siku moja baada ya mwezi sikujuwa kama yule alikuwa sio mke wangu, maana hata simu walibadilishana, nilifurahi sana tena sana baada ya muda mrefu nami nitakuwa baba, miezi nane baadaye mtoto wa kiume akazaliwa, nilifurahi sana...


makubaliano yao nikwamba mtoto akizaliwa shemeji yangu akae kwangu mpaka miezi sita atakayomnyonyesha mtoto halafu kipindi atakapoweza kula vyakula vyengine arudi nyumbani ndipo mke wangu achukuwe mtoto ndio aje kwangu kwani hatakuwa anamnyonyesha tena, miezi sita ikapita shemeji yangu hakurudi nyumbani kwao kwani alinogewa na yale malezi aliyoyapata kwangu....


mke wangu kule nyumbani kwao hakuwa na amani alishachoka alitaka kurudi kwake na huku shem hakutaka kuondoka, basi mke wangu akachoka na kurudi nyumbani kwangu na kuniambia kila kilichotokea, na kwamba yeye hawezi kushika mimba kwasababu alikuwa na matatizo....


kwakweli nilipatwa na mshangao sana baada ya kujuwa mtoto niliyelea siku zote hakuwa damu yangu, nimemwacha shem na mwanaye arudi kwao lakini sidhani kama nitaweza kumsamehe mke wangu, kwanini anifanye nilale kitanda kimoja na dada yake nikijuwa ni yeye!!!!


nitafanyaje?


Michael

Reactions:

1 comments:

  1. Naomba nisaidiwe jamani, ninamkewangu ana ujauzito wa mwezi mmoja na nusu, ila kila siku anaumwa pia ninapoitaji "mambo yetu" anadai bado anaumwa, tulishaenda hospital kukagua afya hakukutwa ana tatizo zaidi ya ujauzito, ila bado nanyimwa "mambo yetu" mimi ni mwanamme ninapokosa nanii najisikia kama mgonjwa furani, naomba ushauri wenu nifanyeje?

    ReplyDelete