Tuesday, March 22, 2011

SIKUJUWA MAMA YANGU MDOGO ALIKUWA NA UHUSIANO WA KIMAPENZI NA MUME WANGU....


mama yangu mdogo ndio mtu niliye baki naye duniani baada ya wazazi wangu kufariki yeye ndiye aliyekuwa ananifanyia kila kitu na kunipa kila ninachohitaji ukizingatia hana mtoto bali mimi wa dada yake, mama yangu huyu kweli anauwezo na tunahishi maisha mazuri silalamiki kila ninachokitaka ananipatia haijalishi ni ya gharama kiasi gani...

nikapata mpenzi mkaka mmoja mtanashati yani hakuna sehemu ambayo nimeshaenda na mpenzi wangu wanawake wasimtolee macho ukiacha uzuri wake kwakweli kaka huyu anajuwa kujitunza kwa mavazi, manukato na afya, siku moja nikamleta nyumbani kwetu kumtambulisha kwa mama yangu mdogo nilidhani litakuwa jambo jema kumbe nilikuwa nampelekea fisi mfupa....

kama walivyomtamani wanawake wengine ndivyo alivyomtamani mama yangu, akamuomba namba ya simu akidai atakuwa akimpigia kumjulia mkwe wake hali, kumbe ikawa anamtongozea kwa hela zake alizokuwa nazo na kwa usumbufu wa mahaba kwa darling wangu mpenzi wangu akashawishika...

mipango ya harusi ilpoanza mama yangu alijitoa sana na kuhakikisha harusi inafungwa haraka kumbe bila kujua mbinu yake alitaka nitoke haraka pale nyumbani ili nisije kuwagundua, pesa ilivyombaya kumbe mpaka shemeji zangu walikuwa wanajuwa halafu wasiniambie mpaka siku moja nikakuta message ya mapenzi kwenye simu ya mume wangu kutoka kwa mama yangu ikimwambia anatamani akampe raha kama anavyompa kila wakati wakikutana...

nilishtushwa sana nilipomwambia mume wangu ninajuwa kama anauhusiano wa kimapenzi na mama yangu akaniambia sasa ametaka mwenyewe kwanini nimnyime??? yani hata hakuona aibu, huyu mwanaume sijui vipi ananitia kichefuchefu...

siwezi kumfwata mama yangu na kumuuliza maana nitagombana naye na haitakuwa vizuri maana yeye ndio tegemezi langu sasa nitafanyaje ama nimuache mume wangu waendelee tu na mapenzi yao?

Mwanahawa

Reactions:

3 comments:

  1. aaahhh! hii sasa kali kweli nionavyo mimi hapa ni kuwaacha kama tegemezi lako ni mama basi fanya hivyo au muulize mume wako kama anampenda kweli mama yako?

    ReplyDelete
  2. duh hapa utu hakuna, huyo jamaa muachie mama aendelee kupewa raha na huyo unaye muita mume hata hajakuoa bado hajatulia hata hio ndoa ukiolewa naye itakua 50 yako 50 ya mama mdogo.Sad!!!!

    ReplyDelete
  3. Kimbiaaaaaaaaaaaaaaaaaa! Acha huyo mume akale pesa ya mama yako. Kama unakazi yako na kujilisha ondoka sasa hivi, hawa wataleta matatizo makubwa kwenye maisha yako baadae. Uwiiiiiiiiii

    ReplyDelete