Friday, March 18, 2011

MKE WANGU KANIPA UKIMWI....


japo mapenzi ni mazuri ndugu zangu nataka tu kuwapa ushauri kabla ya kuamua kuwa na mtu ama kuoa ni vizuri kwenda kupima na kujuwa afya zetu, maana mara nyingi huwa tunajisahau tukisha kuwa na mtu miezi miwili tunakuwa tumezoeana hatuwi tena makini kutumia kinga na baadae mapenzi ya kituzidia tunapooa tunasahau na tena kwenda kupima..

nilipofikiria kuoa niliamua kwenda kuchunguza afya yangu ili nijue ninaposimama kama ni namaambukizi ya Ukimwi ama la maana huko nilipotoka ni parefu, nikashukuru MUNGU nilipopata majibu ya kwamba nilikuwa mzima, ndipo safari yangu ya kutafuta mke ilipoanza...

nilipompata msichana wangu niliyejuwa siku atakuwa mke wangu tukaanza kutumia kinga lakini baada ya muda wa kuzoeana tukaacha na tulipotaka kuoana mchungaji alituuliza kama tumepima tukamwambia ndio tukijuwa ndani ya mioyo yetu hatujapima, tukaoana sasa ndoa yetu ina miezi sita...

wiki mbili zilizopita nikawa najisikia vibaya sana na nikaamua kwenda hospitali kuangalia afya nikapima mengi isipokuwa ukimwi na hakuna nilichokutwa naumwa, nikarudi nyumbani huku bado nikiwa najisikia vibaya baada ya wiki moja nikazidiwa tena ndipo nikashauriwa na mzazi wangu kupima ukimwi....

LOOOOOOOOO.... nikakutwa nimeambukizwa Ukimwi chakushangaza mbona ni mimi tu nilikuwa nauguaugua lakini mke wangu hata siku hakuwahi kuumwa kumbe alikuwa anatumia dawa bila mimi kujuwa ndani ya nyumba yangu mwenyewe na pamoja na kulala naye kitanda kimoja hata sikumoja sijawahi kuhisi anaumwa baada ya kujua ameniambukiza ndipo aliponiambia alikuwa mgonjwa miaka saba sasa na alikuwa anatumia vidonge na ndio maana bado alikuwa anadunda...

sasa jamii nzima inanihurumia na kunilaumu ndugu na jamaa zangu sasa hawataki hata kumuona mke wangu, mimi bado ninamshtuko sana sijui lakufanya wala kumwambia mke wangu nahisi kuchanganyikiwa....

bila kushauriwa nahisi nitafanya jambo lisilo jema, nisaidieni jamani..

PAUL

Reactions:

4 comments:

 1. POLE SANA KWA YALIYOKUKUTA HIYO INAWAKUTA WENGI KWA AJILI YA KUPENDA SANA NAKUSAHAU YAKWAMBA ZAMA TULIYOKO ZAMA ZA HATARI SANA NIKAMA NISHETANI ALIKUPITIA UKASAHAU KUAKIKISHA KWAMBA MWINZIE NAYE ANAPIMA KABLA HAMJAKUTANA NA UKIJARIBU KUFIKIRIA ULIENDA KUPIMA VIZURI TU MWANZONI UKAKUTWA HUNA UNGETAKIWA UNGEKUWA MAKINI TOKA HAPO LAKINI TUWACHE HAYO SASA SIO WAKATI WA KUMTAFUTA MCHAWI NIWAKATI WAKUMTIBU MGONJWA SASA KAKA KWANZA NIKUPE POLE NA HONGERA PIA KWAKUWA MUWAZI NA KUTAKA KUPATA USHAURI MIMI NAKUSHAURI KWANZA JIKUBALI KUWA UNAHALI HIYO USIHUKU USIJE UKAHUKUMIWA WALA USICHANGANYIKIWE MAANA SIO WEWE PEKE YAKO UNAHALI HIYO NA USIFIKIRI UTAKUFA LEO ALIMRADI TU UFUATE MASHARTI YA DAKTA NA HUYO MWANAMKE ANDELEA KUISHI NAYE KITU KINAFANYA WAGONJWA WA UKIMWI WAFE HARAKA NI HOFU NA KUNYANYAPALIWA MIMI MWEWE NINAYOKUSHAURI NINAO HUO UGONJAW NA HAMNA MTU ANAJUA UKINIANGALIA HUWEZI JUA LAKINI SIAMBUKIZI KWA MAKUZUDI MAANA DHAMBI WEWE JIPANGE VIZURI UFUATE MASHARTI UTAMALIZA MIAKA NA MAMIAKA HATA KUZAA UTAZAA VIZURI TU ALIMRADI UWAONE WATAALAM WAKUPE USHAURI NI HAYO TU POLE SANA USIJALI MKO WENGI

  ReplyDelete
 2. Pole sana kaka lkn usikate tamaa ya maisha, vema umeshajua unamaambukizo sasa inabidi uende ukaanze kutumia dawa. isitoshe kuna mzee mwaisapile ameoteshwa dawa huko Rolihondo watu ndio wanaenda huko kupata dawa na wanatoa ushuhuda kuwa wanapona. So nakushauri uwende huko labda mungu ataleta shani yake.

  ReplyDelete
 3. POLE SANA KAKA PAUL KWA7BU NAJUA UPO KWENYE WAKATI MGUMU SANA, KIPINDI HIKI SIYO CHA KUKULAUMU WEWE WALA MKEO KWA KUTOKUPIMA KABLA HAMJAOANA K7BU HIZO LAWAMA HAZITAWASAIDIA KITU,UKIZINGATIA KUWA JANA UWA HAIJIRUDII TENA.NINACHOKUOMBA KWANZA MSAMEHE MKEO KWA KUTOKUKWAMBIA MAPEMA HALAFU NAOMBA UIKUBALI HIYO HALI ULIYONAYO SASA,NENDENI WOTE WAWILI KWA WASHAURI NASAHA HOSPITALINI ILI MSHAURIWE KITAALAM JINSI YA KUISHI NA VVU...FAHAMU KUWA NA VVU SIYO MWISHO WA MAISHA ILA NI MOJAWAPO WA CHANGAMOTO ZA KIAFYA KATIKA MAISHA. NDUGU ZAKO WANAKILA SABABU ZA KUWA NA HASIRA NA MKEO LAKIN BADO HAWATAKIWI KUMTENGA AU KUWATENGANISHA..NDUGU ZENU WA PANDE MBILI WANATAKIWA WAWAONESHE UPENDO NA USHIRIKIANO MKUBWA KATIKA KIPINDI HIKI KIGUMU KWENU...NARUDIA TENA POLE SANA KAKA PAUL, MAISHA YANA MITIHANI MINGI LAKN TUPAMBANE NA TUISHINDE MITIHANI HII,,NAWATAKIA KILA LA HERI KATIKA MAISHA YENU YA NDOA.

  ReplyDelete
 4. HII HABARI LABDA KAMA IMEPIKWA SIIAMINI KAMA IKO REAL!!!!! YAANI MKE WA KUMUOA MIMI ANAKUJA NA DOSE YAKE YA UKIMWI NA AINYWE AKIWA KWANGU NA UKIMWI ANIPE!!!! HALAFU MNASEMA ASAMEHEWE KUNIUA KWA KUKUSUDIA? GOD FORBID MSAMAHA HAPA HAKUNA COZ HUYO NI MUUAJI ANGEKUA HAJUI KAMA MUATHIRIKA SAWA KOSA LA WOTE HAMJAPIMA LAKINI ETI ANAJIBU ALIKUA MGONJWA SIKU NYINGI SO AMEKUJA KUKUUA? NO MSAMAHA PERIOD!!!!!.

  NISEME TU NIMESHINDWA KUSHANGAA HII HABARI!!!

  ReplyDelete