Friday, March 11, 2011

TUMESAHAU KUWA NA HISIA?

wapenzi bwana pindi wanapokutana huwa na mapenzi motomoto na kufanyiana mambo ya maraha tele, na kupeana mazawadi kibao na messages za mapenzi hapo ndipo usiseme....

kwa wanaobarikiwa baada labda ya muda fulani huamua kukaa pamoja, kama ni mke na mume ama tu wapenzi wameamua kukaa pamoja, hapa sasa kasheshe ndipo zinapoanza na mara nyingi upande wa pili wa shilingi huanza kuonekana humu.....

wote tunatambua ya kwamba pindi watu wawili waliolelewa kwenye mazingira tofauti na tabia zao tofauti wanapokaa pamoja basi kugombana na maelewano ni kitu cha kawaida popte pale duniani...

lakini unaposhikilia magombano yakae moyoni mwako wakati wote ndio maana wapenzi wengi huachana, na tunawezaje kuyaachilia yasikae moyoni?

wewe kama mwanaume nilini umempeleka mkeo kula chakula cha jioni nje yani kwenye mazingira tofauti na nyumbani mkiwa wawili tu, maana pale ndipo hisia hukutana tena kwa upendo, mkiongea na kucheka pamoja na kukumbushiana mapenzi yenu tokea mwanzo mpaka sasa na kuongea mengine mengi...

ama lini wewe kama mke ukaamua week - end moja mkalale sehemu ya tofauti na nyumbani hotels zipo nyingi sana na nzuri sana siku hizi, muda huu ni muhimu sana kwani mnakuwa peke yenu tu hamna kelele za watoto na majirani na kupata wakati wa kumchunguza vizuri mwenzako(utakuta ana machejo mapya kibao, unaweza kugundua kama anakovu jipya ambalo hulijui n.k ) maana mkiwa na watoto muda wa kuchunguzana huwa hautoshi maana mara mama hivi mama vile baba hiki na ishu kibao....

TUSIJISAHAU SANA ....Reactions:

1 comments:

  1. dada rose hii nimeipenda umeongea kitu ambacho huwa nakifanya mimi na mume wangu mkitoka tofauti na nyumbani mnaleta mapenzxi mapya na kusahau vyote hata kama mligombana

    ReplyDelete