Friday, March 11, 2011

MTOTO WA MWANAMKE MWENZAKO NI WAKO?

kuna msemo unasema mtoto wa mwanamke mwenzako ni wako pia, yani ukimaanisha kwamba kama mwanamke umeshapitia uzazi basi pale utakapomuona mtoto wa mwenzako utamjali kama wako kwani unajuwa kabisa uchungu aliopitia mama yake, kwahiyo pindi mtoto huyu akiwa amekosa unaweza kumuadhibu na akiwa na tatizo ukamsaidia.

lakini je hii ni kweli kwa sasa wewe unaamini nini? ukiangalia jamani sikuhizi sio kama zamani jamani uzazi wa wakati huu ni mgumu sana, kwa mlio pitia uzazi wa sasa nadhani mtaniunga mkono, kwanza wanawake wengine huchelewa sana kubeba ujauzito wanatafuta pande zote na kula vyote sasa baada ya miaka fulani akija beba azae halafu mama fulani ukamchapie mwanae kisa amekosa huyu mama atakuelewa kweli?

ama mama yule aliyebeba mimba miezi kumi na moja kateseka na tumbo lake, muda mrefu na uchungu kibao halafu leo ukamuadhibu mwanaye bila kumwambia yeye kisa mtoto kafanya kosa wewe ukaona umpe adhabu...

jamani tuwe makini sana, kama mtoto wa fulani amekosea na wazazi wake wapo hai basi hebu tuwaeleze hawa wazazi wake kwanza na wakikupa ruhusa ya kumuadhibu ndipo uendelee, na kwa wale wanaokaa na watoto ambao wazazi wao wamefariki basi hebu tuwe makini kuwachagulia adhabu kulingana na uwezo wao..

0 comments:

Post a Comment