Wednesday, March 2, 2011

MWANAUME HUYU HATA SIMUELEWI.....

kuna dada mmoja amenitumia msg ambayo nimeshindwa kuweka hapa moja kwa moja kwani kuna maneno nilihitaji kuyatoa kabla sijaiweka hapa...

anasema yeye ni msichana wa miaka 24 na anaboyfriend wake wa muda mrefu, anadai yakwamba boyfriend huyu mwanzoni alikuwa mtu mzuri tu na mapenzi yao yalikuwa on fire... cha kushangaza ni kwamba huyu mwanaume akaanza kubadilika mara akaanza kupigiwa simu na wanawake mpaka saa nane za usiku, huyu dada anasema uvuvmilivu ulimshinda na sio kawaida yake lakini ilibidi aanza kuchunguza simu ya mpenzi wake huyu na hapo ndipo akakutana na message za mapenzi kibao za mwanaume huyu akitumiana na wanawake wengine pamoja na mwanamke wake wa zamani akilalamika kwanini alivunja ahadi ya kuwa naye maishani huku huyu mwanaume akimuahidi huyu mwanamke wake wa zamani kwamba yeye ndiye mwanamke anayetaka kumuoa na siyo mwanamke mwengine.

baada ya huyu dada kukuta hizo message kwenye simu ya mpenzi wake huyo akamueleza kwanini imekuwa hivyo huyo kaka akawa hana la kumjibu zaidi ya kujiumauma tu na kuomba msamaha, anasema akajuwa yameisha maana aliamua kufuta namba ya simu ya huyo mwanmke wa jamaa wazamani chakushangaza baada ya muda fulani aliposhika tena simu ya mpenzi wake huyo alikuta ile namba ipo tena kwenye ile simu tena kwa jina la mama fulani......

dada huyu anaomba ushauri afanyeje kuhusu swala hili na kwamtazamo nahisi anampenda sana huyo kaka..

MTAZAMO WANGU......

wewe bado ni msichana mdogo sana kuanza kuumizwa kichwa na mwanaume, huyu ni boyfriend wako tu na sio mume wako uanza kumvumilia na kuumia kila siku, mara uanzishe naye ugomvi wa kuangalia simu yake mara kwa mara ndugu yangu usidhani unasuluhisha bali unaharibu... kwasababu message umeshazikuta na hajaacha hiyo tabia utagombana naye mpaka lini????? na je akiamua kukuacha kwasababu anakuona unapenda kumfwatilia utafanyaje????

najuwa inauma wewe sio wa kwanza kuumizwa na mwanaume na hautakuwa wa mwisho, jipange ukiona huyo haeleweki achana naye asije kukuletea magonjwa na mabalaa mtoto bado mbichi utakutana na mwanaume mwengine atakupenda kiukweli na sio kukuchezea kama huyo boyfriend wako..

ni mume wako tu ndiye unayeweza kumvumilia hata kama akija na kituko gani kwani uliapa kuwa naye mpaka kifo kiwatenganishe, lakini sio boyfriend mpenzi ukiona haeleweki achana naye tafuta mwengine maisha ni mafupi haya kuanza kuumizwa na mtu mliye kutana kimjinimjini.....

Reactions:

1 comments:

  1. ni kweli angeachana nae tu, inaonyesha anampenda huyo msichana wa zamani, kwaiyo bora huyu angeachana nae halafu MUNGU angempa mwanaume mwingine tena mzuri zaidi na mwenye mapenzi ya dhati.

    ni hilo tu namshauri, ingawa inauma ila akaze moyo.

    julie

    ReplyDelete