Monday, February 28, 2011

WAMAMA KWANINI HAMJITENDEI HAKI.......

ukiangalia katika jamii yetu ya sasa asilimia kubwa sana ya watu hulizwa na ndoa zao kama sio kuachwa kabisa na wame zao ama wake zao na hii ni kwa nini?????

nitaanza na kina mama na kina baba pia nitaandika swala lao kwenye topic ya peke yao, wewe mwanamke mwenzangu unalia kila siku kwenye ndoa yako mumeo kutwa kiguu na njia, anamahawara, kila siku visa haviishi ni wewe tu kulia (mimi nilishakataa kulizwa kwenye ndoa yangu na sitaki mwanamke yeyote yule alizwe kwenye ndoa yake pia)...

hata waume zenu wakiniona nawafundisha vibaya sijali, inatakiwa wafike kipindi waelewe nini maana ya mke, unajuwa sisi wanawake bwana kabla hujaolewa unajitahidi kweli kujiweka sopusopu na virutubisho kibao yani unaweza kumuona mwanamke kajiremba mpaka ukamtamani mwanamke mwenzako kwa uzuri, lakini pindi apatapo ndoa yake basi anajiachia hatakama atajipamba sio kama vile mwanzo huyo kaka alipomuona akachanganyikiwa....mmhhhh

pili tunapokuwa tunabeba mimba huu ni wakati ambapo wanawake wengi wanajidanganya kwamba siwezi kumpa mume wangu raha kwa kusingizia mimba, ni kweli kabisa sikatai kuna wakati unafika yani hata hujisikii kabisa, lakini kwani kumpa mumeo raha mpaka aingie mule kunaina nyengine nyingi unaweza kumpa raha na akaridhika bila kutumbukia kunako labda kama yeye mwenyewe hataki kaamua akuvumilie mpaka utakapomaliza.....

baada ya kujifungua pia wanaume wengi hutoka nje kwanini kina mama unajuwa bwana unaponyonyesha yale maziwa yanashombo sana je umesha gundua kama bado ndio ulijue, sasa wewe baba kila akija mama unanuka mziwa hata kipafyum kupaka unasahau kisa upo busy kumuongezea kilo mtoto sasa usipojifunza kumpendezeshea huyo baba wa mtoto ukishaachwa raha atakupa mwanao?????? tujifunze kina mama hata kama unanyonyesha hata ukiwa umevaa kanga basi baba asikukute na shombo ya maziwa jamani inanukaga sana basi tu wanaume wanavumilia......

baada ya kujifungua utalishwa sana supu na mitori ili mtoto apate maziwa, kina mama kila mwanamke analengo kwamba baada ya muda gani mwanangu ataanza kutumia maziwa ya ziada ukiacha ya kwako, inamaana ule mda wewe kama mama unaweza kueudi kazini ama kuendelea na shule na mambo mengi na muda huu ndio mzuri wewe mama kupunguza unene wa ile supu na mitori, maana mtoto atakuwa anatumia maziwa mengine pia kwahiyo anashiba kwa hurahisi, lakini wamam wengi bado bwana wanakaa na utakuta wanazidi kuongezeka unene mpaka sasa mumeo anaanza kuona aibu kutembea na wewe kwa wasiokujua hawachelewi kukusalimia wakidhani ni mama yake kwa jinsi ulivyokuwa huna mvuto wa mke.....

wamama kila siku nasema mwisho wa kulia katika ndoa zetu umefika, anachokitafuta nje lazima kiwemo ndani ili asiweze kutoka, akiamua kutoka sio kwamba hujapendeza kuwa mkewe iwe tu sababu nyengine...

1 comments:

  1. dada yangu swala la wanawake kulia lia,lina chimbuko lake.japo kwa leo nita changia ,upande wa mwanamke mwenyewe kujitambua.na hili linaanzia katika kipengere cha huyo mumeo ulimpata wapi kabla ya kuoana.au mlionana wapi kwa mara ya kwanza. bila kwenda ndani zaid ukijiuliza maswali haya mawili,yawezekana ukagundua sababu ya wewe kulia.mfano kama mlikutana kwa mara ya kwanza ,kwenye kujirusha,ukifuatilia utaona kuna kitu kilijificha hakikuwa wazi mpaka mmefunga ndoa ndo una kuja juwa kumbe mumeo ni mtu wa totos na ni mtu asiye kosa kwenda kujirusha,japo haikatazwi ila una kuta yeye ndo zake na akiwa huko utaratibu ni uleule kama alivyo kupata wewe ila tofauti inabaki tayari wewe ashakueka ndani hivyo anaenderea kujirusha, napo unapo kuja kugundua yametokea hayo lazima uanze kulia.vilevile siyo wote wakutanao kwenye kujirusha yana wakuta haya,ila nisababu mojawapo kuangalia kwa makini mmekutana wapi kwa mara ya kwanza.Lingine bila kwenda kwa umbali zaid, ni kati yenu nania alianza kumzimikia mwenzake. hili nalo lina mchango mkubwa tena saingine ina kuwa kote kwa mwaqnamke,au mwanaume. inategemea na nai mtentwa.kwa hiyo hoja yako nimeipenda sana lakini nipana mno ina hitaji muda, kwasababu hapa tuna ongelea uzoefu.na pia mimi nishabiki mkubwa kuona wanawake wanajitambua na siy kujikomboa.? kaka s.

    ReplyDelete