uzazi wa mpango ni jambo muhimu sana katika jamii yetu, lakini kuna njia nyingi sana ukitaka kupanga uzazi na familia nyingi waliotumia uzazi wa mpango wanasema hawajutii kutumia njia hizo....
lakini najiuliza ni njia gani nzuri ya kutumia? kwasababu watu wengine hupendelea kuweka vijiti japo wengine husema vijiti hivyo hutembea mwilini na kuleta madhara ya cancer.
wengine hutumia kitanzi, hiki hukaa muda mrefu wa miaka kumi lakini pia wengine huniambia tatizo la kitanzi style yako kamwe ni kifo cha mende maana ukijifanya unatoa machejo kinafyatuka, na wengine wanasema mwenza wako akiingia kinamtia kero kwa kumgasi...
na wengine wanatumia vidonge, lakini wengine husema ukikosea kumeza kimoja tu na ukacheza basi goli lazima liwe lako, na wengine wamepata ujauzito pindi wanatumia hizi dawa...
ama kutumia condom? sawa kwa mwanzoni mnaweza kutumia condom lakini mpaka lini, maana wanaume wengi wanasema yani mke wangu mwenyewe nimvalie condom???????????? ama kwa wale walevi najua pindi pombe zimekolea nivigumu sana kukumbuka condom....
je wewe umeshawahi kutumia njia za uzazi na ni ipi na je kunamadhara gani uliyokutana nayo???? maana kunawanawake wanaotaka kutumia njia hizi lakini hawajui ipi ni salama maana maneno yanasemwa mengi...

Njia nzuri na salama ni kalenda na kondom, hizi ni njia ambazo hazina madhara yoyote, hapa nikiwa na maana kwamba ikiwa wanandoa watatumia kalenda itabidi siku za hatari watumie condom, na matumizi haya yanatakiwa mwanamke ndo awe mfuatiliaji mkuu,maana mwanamume ni ngumu kufuatilia siku za hatari kwa mkewe. Hizi dawa za vidonge,sindano na vijiti ni nzuri pia lakini zinamadhara makubwa japokuwa tunaambiwa ni madogo, kwasababu sasa hivi wanawake wengi wananenepeana bila mpango na unene wa kupindukia unamadhara makubwa sana,Sasa hivi wanawake wengi wanaongoza kuwa na vitambi kuliko wanaume,hasa jiji la Dar pia kufunga hedhi unapotumia hizi dawa maranyingi damu inafunga, hebu jiulize hiyo dama inatakiwa kutoka lakini haitoki kwakweli wataalamu wanasema hakuna madhara lakini mimi binafsi nadhani yapo. Hivyo ni vema tukarudia mfumo wa wazazi wetu zamani,hapo tutakuwa salama salimini.
ReplyDeleteNakubaliana na mchangiaji wa kwanza hapo juu.Njia salama zaidi ni ya kalenda na condom, ila inategemea sana ushirikiano na ufuatiliaji wa karibu kati ya mume na mke.
ReplyDeletesasa tufundisheni jindis ya kutumia hy kalenda kiufasaha
ReplyDeleteNatumia njia ya kijiti, inanitesa sana maana sijaacha breed for two months now. Njia ya Calender ilinishinda baada ya kijufungua mzunguko wangu ulivurugika kabisa, mume wangu hata kusikia habari ya Condoms. Sielewi nifanyeje kustop breeding.. Nimechoka.
ReplyDeleteMi natumia kitanzi ni mwaka wa nne sasa sijaona madhara yoyote siku zangu nazipata kawaida mwili wangu uko vilevile nipo kawaida kabisa ila mwanzoni kilikuwa kinamgasi Mr. Nikaenda clinic nikauliza wakasema ni kawaida huwa inafika mda kinalainika. Na kweli sasa hskimsumbui tena na tunafanya tendo la ndoa kwa style zote. Pengine madhara ya hizi njia za uzazi wa mpango yanategemea na mtu mwenyewe wengine zinawakubali na wengine zinawakataa.
ReplyDeleteMadhara ya hizi njia inategemea na mtumiaji mwenyewe, wengine zinawakubali na wengine zinawakataa. Mimi natumia kitanzi nina mwaka wa nne sasa siku zangu napata kawaida mwili wangu upo kawaida sina mabadiliko yoyote. Miezi miwili ya mwanzo baada ya kuweka kilikuwa kinamgasi sn mume wangu, nikaenda clinik kuuliza nikaambiwa kwa vile ni mwanzo, siku zitakavyozidi kwenda kitalainika na kuwa kawaida. Ni kweli, sasa hakimsumbui tena na tunafanya tendo la ndoa kwa style zote
ReplyDeleteJamani mimi najiuliza kwanini watoa huduma za hizi njia za mpango hawawi wakweli? Maana mimi nina mwaka moja toka nilipotoa njiti sijapata hedhi na maumivu ya tumbo napata mara kwa mara. Nauliza kwa ambao wamepata tatizo kama langu je walisaidiwa vipi na madaktari,
ReplyDelete