Friday, February 25, 2011

MSICHANA WANGU WA KAZI JAMANI SIJUI NI MCHAWI?

Mama Paulsen ni rafiki yangu mzuri sana, juzi alinipigia simu akawa ananihadithia kuhusu vituko vya msichana wake wa kazi, kwamba kwanza huyu dada jamani hapendi wageni ukiangalia mama paulsen yeye ni miezi miwili tu tokea ajifungue kwahiyo bado anawageni wanaoenda kumtizama lakini huyu dada yeye hapendi kabisa yani tena wageni mkiingia na mdomo anavuta mimi nikiwa shahidi..

siku chache tu baada ya mama paulsen kujifungua nilienda kumtembelea nikiwa na mwanangu na ndugu yangu mmoja baada ya kufika pale kwakweli yule dada kwa kumuangalia usoni hakuwa na raha kabisa uso aliukunja tukaagiziwa vinywaji yani kitendo cha kwenda kuchukua hivyo vinywaji kwake ilikuwa kama adhabu...

chakushangaza kila mwanagu alipokuwa akimuona yule dada alikuwa analia hataki hata amsogelee ikabidi tushangae usikute dada sio mzima, sasa imefika mama paulsen analalamika msichana hataki hata kumbeba mtoto wake mdogo hata akilia mpaka koo limkauke, amekuwa na dharau kibao mara hata kumwambia usinipigie simu sitaki kuongea na wewe (kweli boss wako unaweza kumwambia mambo kama haya)na vituko vyengine kibao na kila mama paulsen anapotaka kumfukuza anashindwa yani kama kamchawia...

kwa mliowahi kuwa na wasichana wa kazi hii ni kawaida?

3 comments:

  1. Huyo dada wala sio mchawi wala nini ila dalili zote zinaonyesha kuwa huyo amelala na mumewe kwa hiyo anajiona yeye ndio mama mwenye nyumba na amekwishamdharau huyo mama mwenye nyumba. Ndio maana hata wageni wakija anaona tabu kuwahudumia si yeye ndiye anayemhudumia bwana ukizingatia mama alikuwa mjamzito? Sasa yeye kawa bi mkubwa atahudumiaje huyo mwanamke mwenzie, na mbaya zaidi kiburi cha aina hiyo wanapewa na hawa waume zetu migume gume iliwashinda mitume!

    Ushauri

    Mwambie shoga yako amtimue huyo msichana haraka sana hapo nyumbani, kama mambo yao wakafanyie huko mbele ya safari, kuliko hivyo anavyoishi naye humo ndani ni hatari anaweza kumdhuru mtoto maana anaonekana wivu umemjaa kwanini mwenzie ana mtoto na inawezekana baada ya kupata mtoto mume karudisha mapenzi kwa mkewe na wako beneti kwa furaha ya mtoto, sasa hicho kinamuuna. Heri nusu shari kuliko shari kamili!

    ReplyDelete
  2. Pole sn!ujifunze kusoma alama za nyakati,na pale unapoona dada anabadilika ivyo ujue hakufai,bila kumshtua afungashe kilicho chake umrudishe kwao salama dada hawezi kukujibu hivyo mtu uliemwajiri huko ni kushuka kwa adabu kwa hali ya juu,tunatambua mchango wa madada ila heshima isipokuwepo ndani yao,no!no!timua that iz ur house n mtu wa kupita never alow to distroy your happy family.

    ReplyDelete
  3. POLE SANA,
    MIMI NI MAMA NILIYEWAHI KUPATA MSICHANA WA KAZI MWENYE TABIA HIYO,NILAMVUMILIA KWA MWEZI MMOJA 1 TU BAADA YA HAPO NILIMWAMBIA NIMESHINDWA KUISHI NAYE NIKAAGANA NAYE, BAADA YA WIKI 2 NILIBAHATIKA KUPATA MDADA WA NYUMBANI MWINGINE AMBAYE NINAENDELEA KUISHI NAYE MPAKA LEO KARIBIA MIAKA 5 SASA . LENGO LA MAELEZO YOTE HAYO NI KUMWAMBIA HUYO MAMA MWENYE MSICHANA ANAYEMSUMBUA WALA ASIENDELEE KUISHI NAYE, AMWONDOE KWA UZURI TU KWA KUMPA HAKI ZAKE ZOTE THEN ATAFUTE MSICHANA MWINGINE .KUMBUKA MSICHANA NI MTU WA KARIBU SANA KWA MTOTO HIVYO INATAKIWA UMPATE MWENYE MAPENZI MAZURI KWA MTOTO PIA WAZOEANE NA KUPENDANA NA MTOTO. USIENDELEE KUMVUMILIA ANAWEZA KUKUFANYIA JAMBO BAYA ZAIDI YA HILO...POLE SANA MUNGU ATAKUSAIDIA UTAMPATA MDADA MZURI KWANI SIYO WOTE WADADA WENYE TABIA MBAYA, POLE SANA SANA.

    ReplyDelete