Monday, June 7, 2010

RAFIKI HUNAAIBU......

hii ni kwa marafiki wote wanafiki, marafiki nyoka wanaong'ata na kupuliza jani wewe unajifanya rafiki wa mtu kumbe ukienda pembeni unakuwa adui wake namba moja....
rafiki unayejifanya upo kwenye shida na raha, rafiki uliyeaminiwa kusuluhisha uhusiano wao, rafiki uliye kimbiliwa matatizo yakitokea na wakwanza kualikwa wakati wa starehe, kumbe wewe kujifanya mwema kumbe ulikuwa unamtaka mwanaume wa mwenzako jamani wwanamke huna aibu, unamponda mpenzi wa mwenzio ili ukalale na bwanaake???
jamani kweli nimeamini usimchekee mtu ukadhani ni mwema kumbe hamna lolote, hawa marafiki tunaokuwa nao ni wakuuangalia sana, kumbe wanawivu ile mbaya wasione jema limekutokea rafiki atakusifia usoni kumbe moyoni anachuki, mpenzi wako akikununuali kanga atajifanya anamsifia kumbe moyoni anatamani angepewa yeye..
akisikia mpenzi anakutoa out yeye anakasirika anajitahidi aje tu hiyo sehemu japo na mtu mwengine ili achunguze utakayoyafanya na mpenzi wako hivi wewe rafiki mbona unawachokonoa hao unataka waachane umpate wewe?
kwani wakati wanaanzana wewe hukuwepo sialikuona mbona akakuacha akamfuata yeye? hakutaki bora wapotezee tu maana unaonekana kichekesho utajitahidi kwa lolote lakini kijana kwake ndio ameshakaa habanduki hata kwa mkuki..
unajichekesa, na kujipitisha umeshajulikana wewe wala husumbui mtu kwasababu huna jipya yako yote ya kale..
UTAISOMA HIYO HASWA KWA WEWE RAFIKI MNAFIKI.....

0 comments:

Post a Comment