Saturday, June 5, 2010

MIMBA KURUDI NYUMA MUDA WAKE...

jamani kuna dada mmoja alikuwa na mwanaume wake ambaye wamekaa kwa muda kama miaka mitatu hivi, japo walikuwa wanapendana sana siku huyu kaka akaja kupata mwanamke wa kipemba, huku bado akiwa na huyu dada mwengine ambaye aliitwa sophia..
sophia akashika ujauzito huyu kaka wala hakuukataa akawa anamlea mwanamke wake na kumuhudumia kwa kila kitu, sasa siku moja huyu kaka aliporudi nyumbani wakaketi na mpenzi wake kama kawaida yao sebleni wakitafakari maisha yao, mara simu ikaingia ya yule mpemba, jamaa akawa anaipotezea yule dada akaendelea kupiga sophia akamuuliza mpenzi wake kwanini hutaki kupokea simu? jamaa akamjibu watu wa ofisini tu hao, sasa ile simu ikazidi kupigwa sophia akaichukuwa na kukutana na sauti ya mwanamke akimuomba mpenzi wake, na kukasirika kwa nini mwanamke huyo alipokea simu, kwani hakujua yule kaka anampenzi wake anayeishi naye..
yule mpemba akafanya uchunguzi mpaka akamjuwa yule dada ambaye ni sophia sasa, akawa anamfanyia vurugu kila anapojuwa jamaa yupo nyumbani alikuwa akipiga simu ili amkereheshe sophia, na visa vyengine kibao cha kushangaza.....
sophia alikuwa ni mjamzito wa miezi mnne, lakini gafla mimba ikawa haikui baada yakwenda mbele inarudi nyuma, akienda hospital wanampima na kukuta mimba ina miezi miwili, mara mwezi yani kila akipima badala mimba iende mbele inarudi nyuma, jamani....
sophia aliteseka sana pamoja na kuumwa tumbo sana akawa anatokwa damu kama hedhi kwa muda mrefu sana, mpaka ile mimba kuharibika ikabidi akasafishwe, kwakweli yule dada aliumia sana maana huyo ndio alikuwa mtoto wake wa kwanza...
cha kushangaza yule kaka mara gafla akawa hana mapenzi tena na sophia akimshtumu ametoa mimba yake na kumtaka waachane, sophia akakubali waachane japo akiumia sana miezi sita baadae huyu kaka aliyemkataa sophia eti anarudi akimuomba msamaha nakudai yakwamba alikuwa amelogwa jamani hii kweli inawezekana???????
jamani huyu sophia amechanganyikiwa afanyaje na yeye bado anampenda huyu kaka

1 comments:

  1. embu mwambie asipoteze muda wake kurudiana na huyo mwanaume maana atamtenda hivyo siku nyingine halafu aje kusema amelogwa tena hv hawjui wanaume walivyo? ndo janja yao coz wnaaamini wanamwake siku zote ni dhaifu nha wana huruma hivyo hata akija vp atamsamehe tu, maadamu hawajafunga ndoa nae asikubali kumrudia aombe Mungu atampa alie wa kwake, mi nina uzoefu na hawa wanaume jamani kama mtu akianza hiyo tabia hua kubadilika ni nadra sana, kwahiyo shost we songambele kwani hiyo miezi sita uliokaa bila yeye si bado maisha yamesonga? hivyo itapita miaka na miak na utamsahau kabisa.MUNGU AKUPE NGUVU, BARIKIWA.

    ReplyDelete