Monday, June 14, 2010

MATUMIZI YA CONDOM....



wanasema ukimwi unakingika na matumizi ya condom ikiwa moja wapo, lakini je wengi tunaogopa ukimwi lakini mara nyingi kwanini hatukumbuki kutumia condom? na wengi haswa wanaume (samahani kama nitawakwaza) lakini lazima tuliongelee hili jambo, wanaume wengi wao kwa mara ya kwanza wanapokutana na mwanamke wapo tayari kutumia condom na huwa wa kwanza kumkumbusha mpenzi kuhusu condom lakini wanapokuwa wamezoeana tuseme wameshakuwa pamoja kwa labda miezi miwili wanaume wengi hukataa kutumia condom kwa madai kuwa nakuamini na tumeshazoeana....

na wengine utakuta wanasingizia eti condom imepasuka katikati ya mechi, nikafanya utafiti kwa wanaume kutaka kujuwa kama kweli condom huweza kupasuka na wengi wameniambia hamna kitu kama hicho labda huyo jamaa atakuwa amefanya kusudi maana ameona akiomba kavu anaweza atoke doro... wadad mpo hapo shaurilo

magonjwa siku hizi ni mengi sana na unayemuamini sio kwamba mara nyingi kweli yupo msafi kwahiyo tusichoke na wala tusizoee kutembea bila condom kwasababu ya mapenzi tuliyonayo kwa wenzetu hii ni kwa wote wenye ndoa na wasio na ndoa.....

0 comments:

Post a Comment