Monday, June 14, 2010

BABA MKWE ANITAKA KIMAPENZI...

MIMI NI MSICHANA NIPO KWENYE NDOA MWAKA WA TATU SASA, NILIVYOOLEWA WAKWE ZANGU WALINIPENDA SANA NA KUNISIFIA SANA KWA KILA NILILOFANYA HASWA KATIKA KUMTUNZA MUME WANGU, JAPO MAMA MKWE WANGU ALIKUWA AKINIPA SIFA LAKINI NI BABA MKWE WANGU ALIKUWA AKINISIFIA MPAKA MAMA MKWE WANGU AKAWA ANAKASIRIKA MARA NYENGINE LAKINI KWA VILE ALIJUWA NIMEOLEWA NA MWANAYE HAKUTAKA KUHISI VIBAYA..

IKAFIKA MUDA WAKWE WAKIJA NYUMBANI KWETU TUKIWA MEZANI TUNAKULA BABA MKWE ALIKUWA AKINIANGALIA KWA MATAMANIO NA MWARA NYENGINE ANAPITISHA MGUU WAKE CHINI YA MEZA AKINIPAPASA KUASHIRIA KUNITAKA KIMWILI KWA MARA YA KWANZA NILISHUTA SANA NA NIKAMWAMBIA MUME WANGU NAYE ALIKASIRIKA SANA NA KUNIAMBIA NINAMSINGIZIA BABA YAKE KITU AMBACHO KILINIUMA LAKINI NILIJUWA HATA NIAMINI...

SIKU BABA MKWE AKANIPIGIA SIMU NA KUNITAMKIA WAZI KWAMBA ANANITAKA,NILIKATAA NA HAKUCHOKA ALIENDELEA JAPO NILIKATAA HAKUCHOKA ALIPOONA NIMEKUWA NA MSIMAMO WAKUTOMTAKA AKANICHEZEA MCHEZO NA MWANAUME MWENGINE AJE KWETU KUSEMA YEYE NI KIDUMU CHANGU CHA MDA NA KULETA SKENDO KUBWA SANA KWETU KITU AMBACHO KILIMFANYA MUME WANGU KUNIACHA..

NI MUDA SASA SIPO NA MUME WANGU NA HATUKUBAHATIKA KUWA NA WATOTO KWAHIYO HANA ANACHOKITAKA KWANGU, JAPO YEYE AMEAMUA KUENDELEA NA KUWA NA MWANAMKE MWENGINE KWANGU INANIWIA VIGUMU KWANI BADO NAMPENDA SANA MUME WANGU JAMANI NISAIDIENI NIFANYAJE?

5 comments:

  1. pole sana na matatizo yaliyokupata na huku bwana wako hakutaka kukuamini kwakumweleza tabia ya babayakenafikiri hata huyo mume hakuwa na mapenzi ya kweli maana angekuwa na mapenzi ya kweli angeamini uliyomwambia halafu angefanya uchunguzi kabla yauwamuzi kukuacha na sasa tayari anamwanamke mwingine au ilikuwa ni njama wamepanga na baba iliuwachike kwakuwa labda wanaona uzai lakini usivunjike moyo labda ilikuwa haijapangwa kuishi milele tafuta ustaarabu mwingine kwani yeye sio mwaume wa mwisho wa dunia wewe bado mdogo utampata akupendae kutoka rohoni nahuyo baba mkwe umsamehe kutoka rohoni kwani hajui afanyalo

    ReplyDelete
  2. WE VP NA WEWE UTATOKAJE NYUMBANI KWAKO?WAKATI UNAJUA WAZI KUWA HAUNA KOSA LOLTE?KWAKWELI HILO NI KOSA LA KWANZA ULILOFANYA NDO MAANA MMEO AMEPATA UPENYO WA KUOA MWAMNAKE MWINGINE.
    MI NAONA CHA MUHIMU UMWAMBIE HUYO JAMAA ALIYEPANGWA KUJA KUKUHARIBIA NDOA AJE TENA MBELE YA MME WAKO NA BABAMKWE ASEMA ULE UKWELI KUWA ULIKUWA NI MPANGO, HAYO YOTE YANAWEZEKANA IWAPO UNMFAHAMU HUYO MTU NA UNAJUA ALIPO.
    PIA ULIFANYA SANA KOSA WAKATI BABAMKWE ANAKUTONGOZA KWENYE SIMU ULITAKIWA KUMREKODI HAYO MAZUNGUMZO ILI UMPE MME WAKO NDO ATAAMINI.

    PIA LABDA ALIKUWA AKIKUTUMIA MSG PIA?KAMA ALIKUWA AMETUMA MSG HAPO NDO PAZURI NENDA KWENYE KAMPUNI YA SIMU YAKO WAAMBIE WAPRINT CALLZ ZAKO ZOTE NA SMS ALIZOKUWA ANAKUTUMIA NA HIYO HUFANYWA UNDER POLICE, KWAHIYO KAMA UNMAPENDA BADO MME WAKO EMBU NENDA POLICE NA HUKO KWENYE KAMPUNI YA SIMU KWA PAMOJA ITASAIDIA KUVUMBUA UKWELI ULIOJIFICHA.
    POLE SANA SHOST.

    ReplyDelete
  3. Pole sana, lakini chamsingi ungecheza mchezo hata akiuandikie sms na umuoneshe huyo mumeo kama hata aamini tena basi ungempa tu PASS Word baba

    FK

    ReplyDelete
  4. Pole sana dada. Mke au mume ni mipango ya mungu
    Huyo mumeo hana mapenzi ya dhati kwani alitakiwa
    awe upande wako ili kuchunguza kama ni kweli. Pili huyo jamaa aliyetumwa aje kusema wewe ni ulikuwa mpenzi wake angemuuliza ni kwa kipindi gani? Ni wakati uko kwenye ndoa au kabla ya ndoa. Na kama ni kabla ya ndoa hiyo haina nguvu kwani kwa dunia ya sasa hauwezi kuwa na mke au mume ambaye halikuwa hana boyfriend na girlfreand. Kwa vigezo hivyo naona mumeo hakuwa na mapenzi ya dhati. Tulia dada yangu utapata mume atakayekujali na kujua dhamani yako. Mtangulize mungu katika shida yako. POLE SANA DADA.

    ReplyDelete
  5. pole sana dada wanamume niwengi vumilia wako yuko nyuma labda ni mim

    ReplyDelete