Friday, June 18, 2010

LOVE BITES....




ni kweli love bites huwa ni alama ya mapenzi? na kwanini kama ni mapenzi mpaka kung'atana jamani hatakama kwa starehe mmmhhh...

sasa kuna kisa kimoja kimetokea nyumba moja sehemu ya sinza, kuna mume wa mtu ni mtu mzima kama miaka 45 hivi, yule baba alikuwa anamwanamke wa nje ambaye ni msichana mdogo tu kwake lakini mke halisi wa huyu baba ni mtu mzima pia nadhani wamelingana umri..

sasa huyu baba siku kaenda kwa nyumba ndogo yake mapenzi ya kanoga kapewa mambo mapya mabusu tele kumbe mtoto yule kampa baba love bite kwenye shingo, baba yeye si mtu mzima enzi zake hayo mambo yalikuwa hamna!! jamaa karudi nyumbani vizuri kwa sababu ilikuwa usiku akaenda kulala na mkewe wala hakumchunguza...

huyu mtu na mkewe wana watoto watano(mapacha 2), sasa huyu wa mwisho anamiaka kumi na tisa baba alipokuwa mezani asubuhi akinywa chai aliyoandaliwa na mkewe na mke wake akiwa pembeni mara huyu dogo akaja na yeye akaketi kunywa chai...

mama kwa bahatia akaona ile love bite kwasababu hajui ni nini akamuuliza baba Andy vipi mbona shingo nyekundu? baba akamjibu sijui labda nimeng'atwa na mdudu, duh akatokea yule mtoto akamwambia mama yake huyo sio mdudu hiyo inaitwa love bite unang'atwa na mtu anayekupenda (mpenzi) sasa mama akazidi kushangaa mbona mimi sijakung'ata na wala sijui kufanya hivyo!!!!!!!

baba akabaki na mshangao wa kuumbuliwa na mwanae, jamani hatakama tunawapenzi wa nje tutakapokutana nao wakati tunaachana hebu tuangalie wasije wakawa wametuachia balaaa za kwenda kugombana na nyumba zetu kubwa...

HII NI KWA WALE AMBAO HATUWEZI KUKAA NA MPENZI MMOJA...

0 comments:

Post a Comment